Hatari inayoikabili Kambi ya Upinzani Bungeni

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,996
Nilikuwa ni mmoja wa Watanzania wakati wa kampeni ambao tulipenda wapiga kura wawachague wabunge wengi wa wapinzani ili wakaisimamie kikamilifu serikali ya Rais Magufuli kwa kujadili hoja kwa umakini wake, uzito wake na umuhimu wake kwa nchi.

Ni kweli wabunge wa kambi ya upinzani wameongeza mpaka kufikia zaidi ya 117 kwenye bunge lenye wabunge almost 380. Hata hivyo nimeanza kupatwa na wasiwasi kama idadi hii itakuwa imeongeza fikra mpya, pana na mbadala katika bunge la Tanzania.

Ninachokiona kwa sasa ni uwingi wa kambi ya upinzani kimwili badala ya uwingi wa fikra mpya na pana. Kwa mtu asiyeangalia masuala kwa makini anaweza akadhani kambi ya upinzani kwa sasa imeongeza nguvu kifikra lakini kiuhalisia imeongeza tu idadi ya wabunge kimwili ambao kuongezeka kwake hakuwezi kuzuia hoja na miswaada ya serikali kupitishwa na wabunge wa tiketi ya CCM.

Mikutano saba ya bunge imedhihirisha na kuonyesha kambi ya upinzani haiwezi kusimama kwa nguvu za hoja kamaTundu Lissu na Zitto Kabwe watakosekana bungeni!

Ni aibu kwa kambi ya upinzani kutegemea wabunge wawili katika kuisimamia serikali kwa makini hasa ikichukuliwa katika siasa za demokrasia ya vyama vingi ni wajibu wa kila mbunge wa chama kilichoko madarakani kuiwezesha Serikali ya chama chake kutekeleza majukumu yaliyoahidiwa katika ilani ya uchaguzi ikiwa ni pamoja na kutumia uwingi wao kuidhinisha maombi ya bajeti na kubadilisha sheria yanayoletwa bungeni na Serikali ili kuiwezesha nayo itimize ahadi zilizotolewa kwa wananchi kupitia Ilani ya Uchaguzi ya chama.

Inaeleweka kazi ya wabunge wa upinzani siyo kuisimamia serikali pekee bali pia kuidhoofisha katika macho ya wananchi ili wapate uwanja chanya wa kisiasa(political gain).

Kwa sasa wabunge wa upinzani zaidi ya 117 wanabebwa kihoja na wabunge wawili ambao wameonekana kuisimamia serikali kikamilifu. Mpaka sasa ni hoja za Tundu Lissu na Zitto Kabwe zinazoifanya serikali kurudi kwenye msingi wa utendaji kama zilivyo taratibu, kanuni na sheria za bunge/nchi.

Wabunge wengine wakisimama kutoa hoja wanachofanya ni kutoa viroja na vichekesho. Tumewaona wabunge wenye elimu za hapa na pale kama Saed Kubenea, hawezi hata kusoma kanuni mpaka apate msaada wa Tundu Lissu. Joseph Mbilinyi, anadai uwingi wa kura alizopata zaidi ya wabunge wote anatakiwa awe Waziri Mkuu. Jesca Kishoa akidhani bunge ni kijiwe cha kisiasa ambacho hakina kanuni na sheria, to name but a few.

Kwa ujumla, wabunge wengi wa upinzani wanatimiza namba na siyo fikra pana. Utegemezi wa wabunge wawili ni udhaifu mkubwa katika kambi ya upinzani na hatari kwa mapambano ya kutumia nguvu za hoja bungeni.

Kambi ya upinzani ijitathmini upya katika majukumu yake bungeni!

Nadhani hata Mbowe atakuwa ameliona hili tatizo ndio maana kwa sasa anafanya kila linalowezekana ili Zitto awe sehemu ya UKAWA!
 
Hawezekani wachezaji wote 11 Wa mpira wakawa nyota, Wa 2 au 3 wakiwa nyota haina maana kuwa hawa wengine hawastahili kuwepo.Rudi ukafikirie tena
 
Tatizo kwa wabunge wenyewe, tatizo liko kwetu wapiga kura. Siku tukiacha tabia ya kuchagua vyama na tukachagua watu wenye sifa mambo yataenda vizuri. Lakini kwa sasa hatuwezi kufanya lolote, ni shida tuliyojizoesha wenyewe kukumbatia vyama. Nusura Kingwengu, Uwoya nao waingie mjengoni. Tuache uvyama tuchague watu wenye sifa. Leo kafulira yuko nje kibajaji yuko ndani. Haaahaaa, kwenye siasa za kibongo-bongo bado tutasumbuka sana
 
Nakubaliana na wewe kwamba ipo haja ya kujipanga kwa kambi ya upinzani bungeni. lakini nadhani hujawatendea haki katika uchambuzi wako. tunawajua wabunge kadhaa wa upinzani ambao ni vinara bungeni. wengi ni mahiri katika maeneo fulani zaidi. Halima mdee na Mchungaji Msigwa kwa mfano. huwa wanaibuka pale maeneo yao yanapoguswa. Saidi Kubenea pamoja na kwamba anayo madhaifu yake, lakini hana woga kabisa, na ni mpambanaji mzuri. hizo ni kete moja muhimu sana. kuna ambao ni wasomi wazuri lakini wana mapungufu makubwa. ni waoga, au wana mipango mingine ya baadae. kwa hiyo la msingi ni kwa kambi hiyo kujipanga. hata katika timu ya mpira, kuna golikipa, kuna safu ya ulinzi, kuna ma-straika, ambao wewe kazi yako ni kuwalisha mipira tu ili wafumanie nyavu. wakati Straika yupo katika mpambano wa kufunga goli, golikipa hawezi kufanya lolote zaidi ya kutazama. lakini ni timu moja . zinahitajika timu za ndani na nje ya bunge, ili kufanikisha. kila mbunge ana karama zake. hizo ziangaliwe na kuchongwa na kuboreshwa ili zitumike vizuri. hata Tundu Lissu alipoanza ubunge alifanya makosa hapa na pale. ndio kujifunza. michakato ya kisiasa ni mirefu na complicated, inaweza kutuletea watu wa aina fulani. mfano Saidi Kubenea anaweza akawa na umaarufu mkubwa zaidi kuliko mtu mjenga hoja, na akapata wingi wa kura. ukicheza hapo unapoteza jimbo. kwa hiyo katuletea jimbo la ubungo, tumtengeze na tumsaidie badala ya kumbeza
 
Hawezekani wachezaji wote 11 Wa mpira wakawa nyota, Wa 2 au 3 wakiwa nyota haina maana kuwa hawa wengine hawastahili kuwepo.Rudi ukafikirie tena
Siasa siyo mchezo wa mpira!

Hakuna sehemu niliyosema kuna wabunge ambao ni nyota!
 
Khaaaaaa zitto msaliti kaacha usaliti na kujipendekeza ccm ama naelewa vibaya si tuliambiwa hivyo kuwa mwami ni msaliti kweli chadema shkamoo
 
hauwezi ukawatathmini wabunge kwa vikao saba wakati wengine bado hawajapata hata nafasi ya kuzungumza, kwani wingi wa wabunge wa ccm bungeni kuna tija gani zaidi ya vijembe na mipasho? je wingi wa ccm kupitisha hoja za kijinga kunatunufaisha nini sisi wananchi? hata kama cdm wangekuwa wanapinga hoja (kitu ambacho wanakifanya) haiwezi kubadilisha mambo kwa sababu mambo yanapitishwa kwa kura ambazo ccm watashinda tu.

mimi nadhani hoja yako ingekuwa na mashiko kama ingekuwa imelenga kubadili mind set za wabunge wa ccm wajione kuwa wao siyo mali wala sehemu ya serikali bali ni mhimili unaopaswa kuisimamia serikali, na hili ndiyo tatizo lililotufikisha hapa kuwa na wabunge bila bunge.bunge limekuwa dhaifu kiasi cha kufuata maelekezo ya serikali na linakubali kupigishwa magoti bila huruma na mtu ambaye linapaswa kumsimamia.

kuwarundikia mzigo huu wapinzani peke yake bungeni ni kuwaonea tu, hauwezi ukategemea wabunge wote wa upinzani wazungumze kwa wakati mmoja huenda ni mkakati wao wa kutanguliza wajenzi wa hoja na wao kuwaunga mkono, kuwashambulia kuwa hawana uwezo wa kujenga hoja ni fallacy of generalization. mkuu
 
Tatizo kwa wabunge wenyewe, tatizo liko kwetu wapiga kura. Siku tukiacha tabia ya kuchagua vyama na tukachagua watu wenye sifa mambo yataenda vizuri. Lakini kwa sasa hatuwezi kufanya lolote, ni shida tuliyojizoesha wenyewe kukumbatia vyama. Nusura Kingwengu, Uwoya nao waingie mjengoni. Tuache uvyama tuchague watu wenye sifa. Leo kafulira yuko nje kibajaji yuko ndani. Haaahaaa, kwenye siasa za kibongo-bongo bado tutasumbuka sana
Tatizo haliko kwenye wapiga kura, tatizo liko kwenye vyama vya siasa kwa sababu vinatuletea wagombea ambao ni viazi!

Kwa mtaji huu, tunahitaji sheria ya wagombea huru(independent candidate)!
 
Nakubaliana na wewe kwamba ipo haja ya kujipanga kwa kambi ya upinzani bungeni. lakini nadhani hujawatendea haki katika uchambuzi wako. tunawajua wabunge kadhaa wa upinzani ambao ni vinara bungeni. wengi ni mahiri katika maeneo fulani zaidi. Halima mdee na Mchungaji Msigwa kwa mfano. huwa wanaibuka pale maeneo yao yanapoguswa. Saidi Kubenea pamoja na kwamba anayo madhaifu yake, lakini hana woga kabisa, na ni mpambanaji mzuri. hizo ni kete moja muhimu sana. kuna ambao ni wasomi wazuri lakini wana mapungufu makubwa. ni waoga, au wana mipango mingine ya baadae. kwa hiyo la msingi ni kwa kambi hiyo kujipanga. hata katika timu ya mpira, kuna golikipa, kuna safu ya ulinzi, kuna ma-straika, ambao wewe kazi yako ni kuwalisha mipira tu ili wafumanie nyavu. wakati Straika yupo katika mpambano wa kufunga goli, golikipa hawezi kufanya lolote zaidi ya kutazama. lakini ni timu moja . zinahitajika timu za ndani na nje ya bunge, ili kufanikisha. kila mbunge ana karama zake. hizo ziangaliwe na kuchongwa na kuboreshwa ili zitumike vizuri. hata Tundu Lissu alipoanza ubunge alifanya makosa hapa na pale. ndio kujifunza. michakato ya kisiasa ni mirefu na complicated, inaweza kutuletea watu wa aina fulani. mfano Saidi Kubenea anaweza akawa na umaarufu mkubwa zaidi kuliko mtu mjenga hoja, na akapata wingi wa kura. ukicheza hapo unapoteza jimbo. kwa hiyo katuletea jimbo la ubungo, tumtengeze na tumsaidie badala ya kumbeza
Kwa kiasi fulani ninakubaliana na wewe, hata hivyo siku njema huonekana asubuhi!

Hii mikutano sita ya bunge imetupa picha inayotoa majibu kuhusu uwezo wa wabunge wetu!
 
Tatizo haliko kwenye wapiga kura, tatizo liko kwenye vyama vya siasa kwa sababu vinatuletea wagombea ambao ni viazi!

Kwa mtaji huu, tunahitaji sheria ya wagombea huru(independent candidate)!
Nakubaliana na wewe kwa kiwango fulani. Lakini kwa kivilaumu vyama vya siasa sikubaliani na wewe. Vyama vya siasa ni taasisi zinazojiendesha kibiashara, wao wanaangalia nani ANAUZIKA kwa watu na si nani ANAWAFAA watu, haka ni ka ugonjwa ka muda mrefu sasa. Kwa hiyo ni swala la sisi wapiga kura kuangalia nani ANATUFAA na si nani kaletwa na chama gani. Hii itakuwa njia sahihi ya kupata wawakilishi wa kweli watakaokuwa na wajibu wa kutumikia wapiga kura na si kutumikia vyama.
 
MsemajiUkweli kikao kimoja tu mkuu unaweza kutoa analysis ya kuwa na mashaka na Bunge wa upinzani, wape muda mpaka kwenye Bunge la Bajeti............
 
Back
Top Bottom