Hatari iko mbele yetu watz

  • Thread starter Mwamba Usemao Kweli
  • Start date

Mwamba Usemao Kweli

Mwamba Usemao Kweli

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Messages
745
Likes
51
Points
45
Age
99
Mwamba Usemao Kweli

Mwamba Usemao Kweli

JF-Expert Member
Joined Oct 5, 2012
745 51 45
Matukio yanayoendelea kutokea ndani ya Tanzania ni hatari iliyoko mbele yetu na hakika hapa tulipo si salama tena. Wenzetu wenye dhamana ya kusimamia usalama wa watanzania wanatupa mashaka na hofu kwani wamekosa mbinu za kugundua mipango ovu inayopangwa kabla ya utekelezaji wake na kuizuia kwa usalama wa nchi. Ikumbukwe kuwa usalama wa nchi ndio usalama wa raia.

Kumbukumbu yangu ya matukio yaliyotokea ktk kipindi cha miaka isiyozidi 3 toka sasa ni hii ifuatayo: -

1. kupigwa risasi kwa padri zanzibar.
2. kuuwawa kwa risasi padri mwengine zanzibar.
3. kumwagiwa tindikali kwa sheha wa zanzibar.
4. kutekwa, kupigwa na kuumizwa vibaya ikiwemo kung'olewa kucha na meno kwa kiongozi wa madaktari nchini.
5. kutekwa, kupigwa na kuumizwa vibaya ikiwemo kung'olewa kucha na meno kwa kiongozi wa jukwaa la wahiriri nchini.
6. kurushwa kwa bomu kanisani olasiti arusha na kuuwa watu zaidi ya 3 na wengi kujeruhiwa vibaya na kubaki vilema.
7. kurushwa kwa bomu mkutano wa Chadema arusha na kuuwa watu zaidi ya 2 na wengi kujeruhiwa vibaya na kubaki vilema.
8. kuchomwa kwa makanisa mbagala dar es salaam.

Swali ni kwamba: -

1. Je watanzania kweli kama tumeshindwa kuzuia matukio haya kwa kutumia wanausalama wetu je ni kwanini tunashindwa hata kuwatambua wahusika wa matukio haya?

2. Je mustakabali wa nchi yetu ni upi?
3. Je kama tumeshindwa kujilinda wenyewe ni nini kifanyike sasa ili tuweze kujinusuru na matatizo yanayojitokeza sasa?

Ndugu zangu tutafakari yote haya kwa umakini wa hali ya juu sana ikiwa ni pamoja na kuanza kujadili kwa umakini sana matukio haya kweli hayana mahusiano ya karibu na baadhi ya wanasiasa wanaojitahidi kwa makusudi kujinadi kuwa ni wagombea kupitia chama fulani cha siasa kama mbinu ya kutaka kudhoofisha washindani wao wakati huohuo wakijaribu kuwaonyesha watanzania kuwa chama fulani hakifai kupewa dola kwa kuwa kinafujo?

Tafakari Chukua Hatua...
 

Forum statistics

Threads 1,273,431
Members 490,382
Posts 30,481,413