Hatari! Dada aibukia kwa RC Makonda na kudai ametelekezwa na baba yake ambaye ni Mzee Edward Lowassa

Kila kitu kiwe na kiasi, hata siasa kuwe na kiasi maana tukiendekeza siasa kuliko uhalisia uliopo tutaharibu taifa, tukumbuke mchezo wa siasa ni mbaya, unaweza ukawa maarufu au kuaibika.
 
Hukumsikia baada tu ya kuwahoji wachache, akatoka fasta na idadi ya watuhumiwa "wabunge na viongozi wa dini"? Bashite anaweza kuwa ana list yake tayari. Anajiamini yeye hawezi kuzushiwa kwa kuwa anajijua uwezo wake maeneo hayo upoje
Hahahaaa...nyumbani kwa kibogoyo waupataje mfupa...
 
Kwa mujibu wa tangazo la RC, aliyetakiwa kuja ni mama yake au ni huyu mtoto? Kama ni kweli lakini.

Kwa kuwa huyu binti hajamtaja huyo mama yake wala kutaja jina lake, lakini tayari wameshamchafua baba wa watu, na huyo mama anaweza asipatikane kama alivyokuwa yule kada wa ccm aliyemuokoa na kumsaidia Nondo, naanza kuingiwa na mashaka na hili zoezi zima.
Mkuu nilisha predict matokeo ya hili zoezi kufeli kabla ya kuanza the Same kama issue ya madawa ya kulevya kuchafua watu matokeo yake waulize watu mbaazi na choroko wanajua manji nani
 
Cha ajabu ni kipi hapa, waulizeni watu waliopita vyuon na shule za boarding kazi yao ni kuacha watoto. Usikute Lowassa wakati anasoma kasababisha mimba mtoto kazaliwa tena ni mkubwa tu
 
Kwa mujibu wa tangazo la RC, aliyetakiwa kuja ni mama yake au ni huyu mtoto? Kama ni kweli lakini.

Kwa kuwa huyu binti hajamtaja huyo mama yake wala kutaja jina lake, lakini tayari wameshamchafua baba wa watu, na huyo mama anaweza asipatikane kama alivyokuwa yule kada wa ccm aliyemuokoa na kumsaidia Nondo, naanza kuingiwa na mashaka na hili zoezi zima.
Si DNA ipo, lowassa si yupo.Mimi nadhani mtoto kumtafuta baba yake sio lazima mama ahusishwe, Huyo mtoto ni mkubwa sana kuweza kureasons. Wakapimwe na kama ni kweli apewe haki yake
 
Shida moja ya makonda ni mkulupukaji sana haya mambo yakutajana haya ngoja tuendelee kukuona hii movie inaendaje na itaishaje
 
Yajayo yanafurahisha sana. Ati yuko tayari kupima DNN ni kipimo gani hiki!?
Ndio madhara ya kutelekezwa hayo.... anaonekana kakulia uswahilini na shule hana. Kama assingalitelekeza angalikwenda shule na anelijua tofauti kati ya DNN ana Deoxyribo Nucleic Acid . Angalia pua zake, angalia kidevu chake,angalia macho yake halafu fananisha na ya mzee
 
"A litle knowledge is dangerous thing"

Why wanakubali kudharirishwa hivi!!?
Mdada mmoja ameitikia wito wa Mkuu wa Mkoa Dar, Paul Makonda kuhusu wanawake waliotelekezewa watoto kufika ofisini kwake ili kupata msaada wa kisheria. Dada huyo amejitokeza na kudai yeye ni mtoto wa Mzee Edward Lowassa.

Amesema..
''Nimetokea Kigamboni, nimekuja hapa, nimekuja kusikiliza wito wa mkuu wa mkoa, Makonda kwamba watu ambao wametelekezwa. Sasa mimi ni mmoja wa mtoto ambaye niliyetelekezwa, ambaye baba yangu ni Edward Lowassa. Nimeanza kumtafuta toka nikiwa darasa la sita na mama ananambia ni kweli baba yako ndio huyo huyo. Sasa nimefuatilia kila sehemu lakini sioni mafanikio kwa hiyo nimekuja hapa kwa mkuu wa mkoa Makonda anisaidie kwa hali na mali kwa vyovyote vile itakavyokuwa kama nipo tayari nipimwe DNA na huyo mzee Lowassa ili nisaidiwe nijue nakaa wapi. Kwasababu mama yangu mzazi yupo hata akija atatoa ushahidi na atasema kwamba itakuwaje kama DNA nipimwe basi.''
 
Aaahh....yn makonda huwezaji kifanya mambo yako bila kutengeneza suicide mission kama hizi kwa opposite side. Shenzi!!!
 
Mi nilitegemea haya yote..!! Zoezi haliwezi kuanzishwa na Makonda alafu likaenda kwa usiri na mizania ya haki!
Anyway.. Kwa kuwa wamelianzisha liende hivi hivi hadi watakapotajwa na wakuu wa malaika na wale wavaa mavazi ya kijani!!
 
Hawa wawakilisha wa Rais kama Huyu RC ni mizigo kwa kweli, kila jambo analianza na kuishia kati Shisha,Mashoga, Drug users and dealers, Walimu waanze kutolipa Nauli za daladala within these fucking things which one he had Accomplished??? Kiki ni Ugonjwa mbaya sana na ni addiction zaidi ya madaraka.
 
Si DNA ipo, lowassa si yupo.Mimi nadhani mtoto kumtafuta baba yake sio lazima mama ahusishwe, Huyo mtoto ni mkubwa sana kuweza kureasons. Wakapimwe na kama ni kweli apewe haki yake
What if sio kweli ?
 
Back
Top Bottom