Hataki kuolewa na mimi msaada tafadhari

ngakotecture

JF-Expert Member
Dec 30, 2014
2,449
2,576
Habari wakuu,

Ni hivi nina msichana wangu wa kitambo kidogo na mimi ndio nilimtoaga usichana sasa alihama mitaa yetu kuna mahali anaishi.

Sasa kipindi hiki nimempa ofa ya ndoa amegoma kuishi na mimi na nadhani hata tabia zake ni za ajabu kwani avai nguo za stara mimi nilitaka nimbadilishe but anaonesha kureact.

Msaada wakuu nifanyaje na mimi nahitaji kuoa.
 
Habari wakuu ni hivi nina demu wangu wa kitambo kidogo na mimi ndio nilimtoaga usichana sasa alihama mitaa yetu kuna mahali anaishi,sasa kipindi hiki nimempa ofa ya ndoa amegoma kuishi na mimi na nazani hata tabia zake ni za ajabu kwan avai nguo za stara mimi nilitaka nimbadilishe but anaonesha kureact msaada wakuu nifanyaje na mimi naitaji kuoa.
Nadhan hufaham ndoa ni nin otherwise usingemlazimisha.
 
Mkuu wala usilazimishe ndoa sbb huyo sio wako mpaka hapa. Tayari ana mwingine anayempenda sana na anatamani aolewe naye ila sio ww. Mtu anayekupenda kwanza ukimwambia suala ndoa anafurahi sana na hawez kukataa hata kusita kwa sekunde. Zaid ya kusema YES
Huyo muache tu, wala usisumbuke naye. Mapenz hayalazimishi. Wanawake wapo wengi tu mkuu japo unaumia lkn jikaze kiume utayashinda mapenz ndiyo yalivyo.
Tafuta binti mzuri kuliko yy uoe kbsa
 
Hicho kiherehere cha kulazimisha ndoa isipotakiwa,kitakutokea puani. Kama hataki, ni kipi unachoendelea kukitafuta kwake? Achana nae na uendelee na mambo ya msingi,eti umbadilishe,umekuwa Baba yake? Huyo hakupendi na haoni kuwa una vigezo anavyotaka,tafuta mwingine,mbona wako wengi?
 
Pole mkuu. Nasikitika kusema huyu atakuwa ameipata mwingine. Suluhisho kwa sasa ni wewe kukubaliana na hali na kuanza kumtafuta mwingine.
 
Habari wakuu ni hivi nina demu wangu wa kitambo kidogo na mimi ndio nilimtoaga usichana sasa alihama mitaa yetu kuna mahali anaishi,sasa kipindi hiki nimempa ofa ya ndoa amegoma kuishi na mimi na nazani hata tabia zake ni za ajabu kwan avai nguo za stara mimi nilitaka nimbadilishe but anaonesha kureact msaada wakuu nifanyaje na mimi naitaji kuoa.
Mtafute mwingine! Kama mwanamke hataki usimlazimishe, atakusumbua!!!
 
Mnunulie kagari. Atakupenda fasta. Yani moyo wake utafunguka kama kabyureta ya boxer Bm 150 na mwendo utakuwa ni spidi 120!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom