Hataki kuachana na ex wake

Hataki kuachana na ex wake

Kama una Gari hatua hazikuhusu ila kama huna hata usafiri kuchukua hatua ni safari inayohusisha miguu.
 
Ukiendekeza mahaba niue utaumia tu... we piga chini uumie maumivu yakipoa unaangalia mengine au waache waendelee uwe unapiga kama kiburudisho tu ila usimuweke akilini wala kumfatilia
 
pole kaka. cha kufanya kama yeye hataki kuachana na ex wake wewe anza kwa kuachana naye. huyo dada hana upendo wowote kwako anakuchukulia kama mnyonge wake yakibuma huko ndo aje kwako, wewe endelea na maisha yako utapata mwingine huyo fyekelea mbali. all the best
 
hakufai huyo fanya hamsini zako...hakunaga awali mbovu so mwenzio bado anaikumbuka awali yake....shtuka mangi.

Amefanikiwa kukuwekea dawa ya kukupumbaza akili.

Hivi akili za wanaume wa aina yako zinapatikanaje? maana najiulizaga sana kung'ang'ania janamke la hovyo kama hivyo unafaidika na nini hasa?mbona wanawake wanaojitambua wako wengi.
 
Kwa upande wangu ningempa makofi na kipigo then nachukua simu yake. Pumbavu
 
Pole na hongera kwa kujaaliwa moyo mgumu kama chuma cha pua...
 
Jamani habari za asubuhi,nimejikuta kwenye mgogoro wa kimawazo juu na huyu mpenzi /mchumba wangu


Ni mwanamke kutoka mkoa wa kagera tulikutana mwaka mmoja uliopita tukaanzisha mahusiano naye

Kipindi tukiwa kwenye mahusiano mara kwa mara nimekuwa nikimfumania anawasiliana na ex wake,na nilivyofuatilia ex wake ana mwanamke mwingine

Nikamuonya akawa anasema wanawasiliana kawaida,kirafiki maana waliachana bila kugombana

Mimi nikakataaa hayo mawasiliano yao,nikataka yavunjike,ila baada ya miezi kadhaa nikakuta meseji ya kugombana na ex wake akimtuhumu kuwaweka wanawake kwenye dp yake

Nikagomba,na nikavunja mahusiano maana hakunielewa na ,ila baada ya wiki akaja akaniomba msamaha ,akakiri kosa,na akaahidi mbele ya dada yake kuwa hatarudia tena kuongea na ex wake

Juzi nikatumiwa sms kutoka kwa mwanamke wa jamaa huyo ambaye ni ex wa mpenzi/ mchumba wangu kuwa mbona mke wako ananisumbua ,anakuwa anawasiliana na mpenzi wangu,anataka nini?

Hapa nimekaa nawaza nichukue hatua gani kwa huyu mwanamke maana ,sijui kwa nini wanawasiliana na ex wake?
Mkuu mtu wa hovyo wala hupaswi kuwaza mara mbili mbili ni kutemana nae na we kuangalia hamsini zako,mbona wapo wengi tu tena utampata mzuri anaekuheashimu na kukusikiliza
 
Mjinga hata umchukue ukamsaga pamoja na ngano, ujinga wake hautamtoka, achana nae huyo.
 
Back
Top Bottom