Mwene chungu
JF-Expert Member
- Nov 12, 2016
- 915
- 752
Hadi sasa sina uhakika kama kuna mtanzania asiekuwa na na dini au ambaye haamini uwepo wa Mungu.
Kwa bahati mbaya sana kwa kawaida wanadamu na hususani Watanzania ni wakati wa kampeni tu ndio utaskia wachungaji na mashekhe wakiombanakufanya makongamano ati ili kumpata RAIS -ambapo akipatikana huwa wanaamini Mungu amejibu maombi yao nakukaa kimya.
Lakini mim niwakumbushe kitu kimoja;kama tunavyohitaji kula kila kila siku,vivyo hivyo hata Taifa linavyohitaji chakula cha kiroho na kimwili kila iitwayo siku.
Tumekuwa na kasumba ya kumkumbuka Mungu wakati wa kampeni(SHIDA NA MATATIZO) tu na baada ya hapo tunajua tunamaliza kazi..NA HATA KAULI ZETU HUBADILIKA KANA KWAMBA YOTE YALIYOTENDEKA SISI NDIO SABABU , makongamano ya kuliombea taifa hayaskiki tena...Ni mungu gani huyo wa msimu?...AU KWA SASA TUMEPATA MUNGU MWINGINE?
Binfsi kwa bahati mbaya sana sio mkristo wala muislam na mbaya zaidi dini yangu haina waamuni wengi sana hata kuwa na impact kitaifa,hasa kwa misingi ya kuto jihusisha na siasa.lakini kila mtu kwa imani yake akiliombea taifa halitaugua kipindupindu wala njaa,halitapata maafa wala ukame,hata viongozi wataheshimiana na kuwaheshimu wanaowaongoza
Tunatakiwa kujua kuwa Mungu atatusaidia kwa msimu pia kwa sababu tunamkumbuka kwa msimu vilevile....
Kumbukeni hata rais sasa hasemi tena "niombeeni"kama alivyokuwa anaskika akisema mara kwa mara alipoingia tu madarakani,badaala yake anasema "anajiamini"(hamwamini tena Mungu);hasemi tena "msema kweli ni mpenzi wa Mungu"badala yake anasema fomu alichukua mwenyewe,tumuache afanye anachotaka tusimuingilie uhuru wake....tofauti na. alivyokuwa anasema kila asimamapo jukwaani hii inamaana gani?
Kuwa Mungu sio kipaumbele tena kwake....najua kama kuna ibada zisizizo za hadharani lakini kadili mtu unavyokuwa mbali na Mungu matokeo yake huonekana tu ..
Kwa sasa Taifa letu lina(Umwa) homa,na homa hii inahitaji madakatari wa kimwili(wasomi,watu wenye busara na hekima,wanasiasa,viongozi),na madakatari wa kiroho( Mashekhe,wachungaji,nk) kulitibu taifa hili..kila mtu kwa nafsi yake..
Dalili za wagonjwa wengi ni kufanya mambo tofauti na utaratibu wa kawaida,Taifa letu linapitia hatua hii...sio lazima kuumwa kila kiungo mwilini ndio ukiri unaumwa..hata ukiugua kicwa,au jicho tu mbele ya dakatari wewe mgonjwa...na hata wewe mwenyewe utakosa raha..
HAKUNA TAIFA LILIPIGA HATUA YA MAENDELEO DUNIANI KWA WATU(RAIA) WAKE KUISHI KWA UOGA NA SINTOFAHAMU MUDA WOTE.