Wakuu embu tujadili huu msemo, kuna mdada wa makamo alikuwa anasumulia jinsi alivyotoka mbali na
Mumewe, na jinsi alivyoteswa na huyo mume kiasi cha kuondoka home kwa mda wa mwaka na kwenda
kuishi na mwanamke mwingine
Baada ya mwaka huo akarudi akaomba msamaha kwa mkewe, wakabariki na ndoa maisha yakaendelea
ila uhuni ukaendelea kama kawaida, mara harudi kwake hata siku tatu, mke akaamua kuvumilia tu
sasa imepita miaka kibao na wana watoto watano, yule mwanaume kabadilika amekuwa yeye wa kumfata
mkewe hata salon na kumsubiria nje mpaka amalize, ofisini anaweza enda msubiria kuanzia saa tisa yuko
nje mpaka saa kumi na nusu......
Tatizo linakuja yule dada alishakufa ganzi moyo akawa anaishi maisha yake, wakati mume sasa hivi ndio
anajifanya kumuhitaji kuliko kitu chochote kile, ndio mwisho wa maongezi mdada mwingine akaibuka na huu
msemo eti hata shatani akizeeka anakuwa malaika.......Eti wakuu mnakubaliana na huo msemo???
Nawakilisha
Mkewe kamsamehe ila ku corp na hali ya sasa anashindwa, yaani mbanano, alishazoea hata simu hapigiwi, wala haulizwi yuko wapi, na yeye alimfatilia mumewe akashindwa hivo akawa hamuulizi kabisa hata asiporudi home...ndio hivyo tena jamaa kajirudi kawa anajaliHapana shetani ni shetani wala muda hauwezi kumbadilisha. Ila kwa ishu ya huyo mbaba inawezekana amebadilika tu na ameona sio vyema kuendelea kumtesa mke wake na amejirudi kwa nafsi yake na kurudisha majeshi nyumbani. Mke kama vipi amsamehe mume wake na waendelee na maisha.
Kama ni watoto basi asingekuwa anamfata nyuma mkewe kihivi, kilichofanya asimulie na mimi nikiwepo alimfata dada angu pale mlimani city tukawa wadada kama watano hivi ikabidi yule baba akakae pembeni amsubiri mkewe, wale wadada wakawa wanamshangaa ni huyuhuyu au mwingine, maana wanamjua shemeji yaoKama nimesoma vizuri, huyu bwana sio kwamba kabadilika - watoto ndo wanamtaiti. Siku akipata upenyo atatembea tu. Kunguru hafugiki ndg zangu tambueni hilo.
Kweli Mungu ni mkubwa mtu wa kuhama nyumba na kulala nje leo kawa hiviNi kweli yawezekana huyo baba amebadilika maana hakuna lisilowezekana kwa Mungu. Ila pia kwa ushauri tuu, kama walikuwa hawapo wote kindoa ni bora wakapime kwanza ndo waendelee na maisha. Wanaume bwana, anaweza kujua anaumwa then akaja kumuua dada wa watu. Ni hayo tu.
Mbona malaika anaweza kuwa shetani?Hapana shetani ni shetani wala muda hauwezi kumbadilisha. Ila kwa ishu ya huyo mbaba inawezekana amebadilika tu na ameona sio vyema kuendelea kumtesa mke wake na amejirudi kwa nafsi yake na kurudisha majeshi nyumbani. Mke kama vipi amsamehe mume wake na waendelee na maisha.
Kuna mwinginekamshauri wakapime labda kaukanyaga maana wazee wakishakanyaga wanatulia ili wauguzwe vizuriwatu hubadilika wakiwa na sababu za kufanya hivyo,inawezekana kabisa akziacha njia zake mbaya kwa msaada wa Mungu asiyeshindwa jambo!
Kweli Mungu ni mkubwa mtu wa kuhama nyumba na kulala nje leo kawa hivi