Hata Mugabe wakati anaharibu uchumi wa nchi yake alishangiliwa sana na kuitwa mzalendo,leo wanalia!

chinembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
5,559
2,000
Mugabe wakati anaivuruga Zimbabwe ,alishangiliwa na kusifiwa sana kwa kuitwa shujaa,kila aliyemuonya alionekana mbaya,leo tunavuruga uchumi kwa sababu za kupika na tena zinapikwa na wanasiasa,tunasahau kwamba robo ya mapato au karibu robo ya mapato ya TRA hutoka ACACIA(kwa mwaka),hatuangalii kesho tutapata dawa hospitali na tumeamua kutofata utaratibu wa sheria ili maisha yaendelee,nchi imehamishiwa kwenye TV.

Hugo Chavez naye wakati anavuruga uchumi wa Venezuela alishangiliwa sana,leo hata chakula hakuna katika nchi hiyo!

Akina kambona wakati wanaupinga ujamaa,walionekana wabaya sana mpaka baadae Nyerere alipoona ujamaa ni mfumo mfu, akarudi kwenye ubepari ulioungwa mkono na kambona,lakini kipindi hicho kambona aliimbwa kwa kila jina baya, nchi ikafilisika watu wakawa masikini kwelikweli,

Hata leo, tunaibomoa nchi huku tukishangilia,tutayaona matunda ya kuibomoa nchi hii ndani ya miezi michache ijayo,kama tulivyoona pale bandarini,kwenye sukari na sekta nyingine na mpaka sasa kuna baadhi ya ofisi za umma hasa dispensary,zimebaki na wafagizi tu,watumishi wengine tumefukuza
 
chinembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
5,559
2,000
Yaani watu munaombea balaa tu! sijui ni kwa faida ya nani?
Sio mabaya,nchi hii ina taratibu za kushughulikia migogoro,zikiwemo mahakama za kodi,mahakama za kawaida,kama kulikuwa na hoja ipelekwe huko,tuangalie maslahi mapana ya nchi,wawekezaji wote wamesita kuja nchini kwa sababu ya makelele ambayo yalikuwa na yana sehemu ya kusikilizwa(mahakamani)bila kuleta taharuki katika dunia ya wawekezaji

Uzalendo ni pamoja na kufata sheria na kushughulikia masuala kwa mujibu wa sheria na sio kelele za siasa
 
Mapya Yaja

JF-Expert Member
Feb 8, 2013
560
500
Mugabe wakati anaivuruga Zimbabwe ,alishangiliwa na kusifiwa sana kwa kuitwa shujaa,kila aliyemuonya alionekana mbaya,leo tunavuruga uchumi kwa sababu za kupika na tena zinapikwa na wanasiasa,tunasahau kwamba robo ya mapato au karibu robo ya mapato ya TRA hutoka ACACIA(kwa mwaka),hatuangalii kesho tutapata dawa hospitali na tumeamua kutofata utaratibu wa sheria ili maisha yaendelee,nchi imehamishiwa kwenye TV.

Hugo Chavez naye wakati anavuruga uchumi wa Venezuela alishangiliwa sana,leo hata chakula hakuna katika nchi hiyo!

Akina kambona wakati wanaupinga ujamaa,walionekana wabaya sana mpaka baadae Nyerere alipoona ujamaa ni mfumo mfu, akarudi kwenye ubepari ulioungwa mkono na kambona,lakini kipindi hicho kambona aliimbwa kwa kila jina baya, nchi ikafilisika watu wakawa masikini kwelikweli,

Hata leo, tunaibomoa nchi huku tukishangilia,tutayaona matunda ya kuibomoa nchi hii ndani ya miezi michache ijayo,kama tulivyoona pale bandarini,kwenye sukari na sekta nyingine na mpaka sasa kuna baadhi ya ofisi za umma hasa dispensary,zimebaki na wafagizi tu,watumishi wengine tumefukuza
Huu ndo ukweli wote, wapuuzi wasioelewa wanashangilia bila kujua matokeo yajayo ni mabaya kuliko wanavyofikiri. Hata nchi tajiri zilizopiga hatua hazifanyi maamuzi kwa kiburi na sifa kama hizi sembuse Tanzania ambao hata Vyandarua bado tunategemea msaada wa wahisani.
 
lusungo

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
20,841
2,000
Hizi Kamati za Magufuli Sio za kwanza zilianzia kwa kina Mkapa, JK na kwake...

Hadidu za rejea kwa Kamati ya Mboma, Bukuku, Masha, Bomani zinalingana na hizi za Ossoro na Mruma....

Mpaka findings na recommendations zinawiana isipokua data tu za Ossoro na Mruma ziko too overrated ukilinganisha na kwa Bomani
 
M-mbabe

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
10,787
2,000
Mugabe wakati anaivuruga Zimbabwe ,alishangiliwa na kusifiwa sana kwa kuitwa shujaa,kila aliyemuonya alionekana mbaya,leo tunavuruga uchumi kwa sababu za kupika na tena zinapikwa na wanasiasa,tunasahau kwamba robo ya mapato au karibu robo ya mapato ya TRA hutoka ACACIA(kwa mwaka),hatuangalii kesho tutapata dawa hospitali na tumeamua kutofata utaratibu wa sheria ili maisha yaendelee,nchi imehamishiwa kwenye TV.

Hugo Chavez naye wakati anavuruga uchumi wa Venezuela alishangiliwa sana,leo hata chakula hakuna katika nchi hiyo!

Akina kambona wakati wanaupinga ujamaa,walionekana wabaya sana mpaka baadae Nyerere alipoona ujamaa ni mfumo mfu, akarudi kwenye ubepari ulioungwa mkono na kambona,lakini kipindi hicho kambona aliimbwa kwa kila jina baya, nchi ikafilisika watu wakawa masikini kwelikweli,

Hata leo, tunaibomoa nchi huku tukishangilia,tutayaona matunda ya kuibomoa nchi hii ndani ya miezi michache ijayo,kama tulivyoona pale bandarini,kwenye sukari na sekta nyingine na mpaka sasa kuna baadhi ya ofisi za umma hasa dispensary,zimebaki na wafagizi tu,watumishi wengine tumefukuza
mkuu, tatizo letu Watanzania liko hapa....tumo kwenye 10 hovyo katika nchi ambazo raia wake wana IQ ndogo duniani.

Zimbabwe wamo kwenye kundi moja na Tanzania - so that should explain why Zimbabweans allowed Mugabe to do what he did while themselves ending up where they are today!

Mchimba Chumvi

JF-Expert Member
May 19, 2016
1,326
2,000
Watanzania ndo tulivyo unafiki tuu
Cjajua kama mjukuu wangu. Naye atakuja kuona tz ya viwanda!!!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom