Gangongine
JF-Expert Member
- Dec 31, 2015
- 3,854
- 1,776
CCM ni Chama Kikongwe na kimefanya mengi sana. Yapo mabaya kama ambavyo Chama chochote Duniani( ikiwamo CDM/UKAWA) kinaweza kufanya. Katika miaka ya karibuni kumekuwa na changamoto nyingi kwa vijana kama vile ukosefu wa Ajira, mitaji ya biashara, masoko ya bidhaa za wakulima, pembejeo n.k.
Uchumi wetu unapaswa kuimarishwa uweze kukabili changamoto za makundi yote ya Jamii na kukidhi matarajio ya walio wengi. Mabadiliko yanawezwa kufanywa na Chama Tawala au Chama cha Upinzani chenye nia na uwezo wa dhati wa kuleta mabadiliko ya kweli.mmm wale ndio walete mabadiliko???.....Yule ndiye alete mabadiliko??? Acheni kudanganywa kijinga!! Labda mabadiliko yake mwenyewe kwenye mfuko!
Kwa hali ilivyo na kwa aina ya Wagombea ambao Wapinzani wanatushawishi tuwachague, ni mzaha wa hali ya juu kutuaminisha kwamba wataleta mabadiliko kwa Waanchi badala ya mabadiliko yao binafsi. Na ndio maana watu hao wametumia miaka mingi kuwekeza Fedha kwa njia ya harambee na michango mbalimbali kwa jamii, kwa kuwa wana malengo yao binafsi. Hakuna mtu mjinga apoteze fedha nyingi kuusaka Uongozi wa Nchi halafu eti aje awatumikie Wananchi badala ya kurejesha hesabu zake. Ni aibu kwa kijana kutotambua hili huku akidai ni msomi wa Chuo Kikuu! Usomi wake unamsaidia nini kama anaweza kudanganywa kirahisi mpaka kiasi cha kudeki barabara!
Katika mazingira hayo nasema hata kama ningeichoka CCM namna gani, siwezi kudanganywa kijinga nichague Wagombea wa UKAWA waliopatikana kwa kuokotezwa kutoka kwenye watu waliokataliwa na CCM kutokana na historia yao. Ebu tujiulize kama kweli una lengo la kuleta mabadiliko ya kweli kwa nini ununue uongozi kwa gharama kubwa? Utarudishaje hizo Fedha wakati Ikulu hakuna biashara yoyote? SIDANGANYIKI! SIDANGANYIKI! SIDANGANYIKI!
Nitashawishika na upinzani pale watakapotuletea Sera Mbadala na watakapotuletea wagombea makini ambao kwa kuwaangalia kwa macho tu unaweza kuwa na chembe ya imani kuwa watatumikia Wananchi. Hawa wanaotumia Fedha nyingi kuwekeza kwenye Siasa ni watu wasiofaa na wenye malengo yasiyo na manufaa kwa Nchi yetu. Kama wana Fedha nyingi ni bora wajenge Viwanda, wawekeze kwenye Kilimo, wajenge Vyuo, Hospitali n.k ili watatue changamoto za Ajira, elimu, Afya n.k badala ya kutufanya wajinga kwa kutununua! CCM OYEE! HAPA KAZI TU!!