Hata huyu shetani akifa leo watu watamkumbuka na Kum miss

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,860
24,647
Imekuwa kawaida kila mara anapoondoka mtu mmoja anapoondoka wengine kumkumbuka. Si jambo geni kabisa katika utamaduni wa Binadamu. Kuna wanaomsifu Hitler mpaka leo hii, kuna wanaomkumbuka idd amin, bokassa na waovu wengine waliopata kuwepo dunia hii. Hatushangai hata kidogo watu kuanza kumsifia marehemu mwizi,mzinzi,fisadi na aliyetenda aina na aina ya uovu katika jamii. Kwenye kundi la watu zaidi ya 10 si rahisi wote wakakupenda au kukuchukia

Hatushangai haya katika jamii watu wanapokumbuka misri, hatushangai haya katika jamii watu wanapokumbuka kurudi kwenye shimo ambalo huko walikuwa wanakula mizoga kwa kuwa sasa baada ya kutolewa shimoni wanajikuta wanapaswa watafute chakula chao wenyewe. Wanasema ni bora tulipokuwa shimoni kule walikuwa wanakula mizoga ya wanyama iliyodondokea humo.

Amini usiamini katika ulimwengu huu ni wengi wanafaidika na shetani kuliko unavyodhan. Na ikitokea shetani akafa leo. Wengi watalia na kuomboleza wakilalamika utawala wa malaika kuwa si mzuri. Na wataandamana na kulalamika kuwa bora shetani aliwapa uhuru na waliamua kufanya walichotaka.

Haya ni mambo ambayo yapo na yataendelea kuwepo. Shetani naye ana watu na watu hawa tunaishi nao jamii hii hii . tunakula nao, tunaswali nao, tunafanya mengi nao lakini ni wafaidika wa shetani.

Msidhani huyu shetani hana ndugu, marafiki na jamaa, msidhani shetani hana watoto, wajukuu na watu wa karibu. Subirini siku akifa mtakapoona watu wanalia na kuomboleza.

Kwa wewe unayesema unamchukia shetani mchukie shetani na matendo yake.

Ni aibu kukumbuka maisha ya shimoni kwa kuwa tu kule watu walikuwa wanakula mizoga bure tu, kwa kuwa kule watu walikuwa wanaruhusiwa kulana nyama ikiwa mmoja atafariki. Ni jambo la kuogofya kumkumbuka na kumtukuza shetani kwa vile amekufa na watu wanakosa nafasi ya kutenda uovu wao.

Aliye na sikio ayasikie maneno haya. Safari bado ni ndefu kuelekea nchi ya ahadi nani atakuwa Mussa wetu?
 
Mi nine elewa ila kwa kutumia nadharia ya umuundo Leo ambapo maana ya kilongo IPO kwa msomaji,hivyo nilivyo ielewa Mimi si sawa na utakavyo elewa wewe. Shetani=awamu ya 4, malaika=awamu ya 5
 
Leo umeandika article nzuri sana aisee, na umeeleweka mno.

Sijui utakuwa umeiandika wewe mwenyewe au umeikopi mahali??

Ila big up sana kwa uzi huu.
 
Back
Top Bottom