Hata hivyo, hatutaogopa!

Hata hivyo, hatutaogopa!

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
25,938
Reaction score
41,100
Kumuua binadamu mwenzio asiye na hatia Kisha kumtia kwenye kiroba na kumtupa Ili umma ujue ,inalenga kuwatisha wananchi waone kwamba ninyi ni wa kuogopeka.


Ninasema waliouwawa ni wasio na hatia sababu kuu ni kuwa, Mahakama ndio sehemu pekee ambayo nchi na katiba yetu imeelekeza kutoa hukumu kwa watu wote, sasa kuua watu na kuwaita Katika viroba ni kujaribu kutisha watu.

Taratibu umma umeanza kuzoea jambo hili, na kuzoea ni kuota usugu.


Zamani waliogopa kusema kuhofia kutiwa kwenye viroba, sasa wanaongea wakiwa wamejiandaa kukabiliana na wauaji kwa namna mbalimbali.

Somo hapo ni kuwa, JAMII inazidi kubadilika na taratibu mbinu za watekaji kuteka watu zitabainika na JAMII itakabiliana nayo kwa kadri watakavyokuja.

Kitu pekee watekaji wamefanikiwa, ni kuwafanya watanzania kuzoea vitendo vya utekaji, hivi sasa SI kitu kigeni Tena kwao.

Na kitu ambacho watekaji wameshindwa ni kuzuia wananchi kuongea. Wameshindwa kutuogopesha, kutunyamazisha. Sisi wananchi ni wengi kuliko ninyi.

Mwanzoni waliogopa na kwenda kusemea chooni wakiogopa kutekwa, saizi wanasema peupe kwenye mitandao mbalimbali kwa namba zao wazi na sura zao wazi wazi.

Hatutaogopa, Hadi pale haki itakaposimama Katika taifa letu.

Haki haiombwi, inadaiwa, na ina Gharama zake ambazo watanzania tuko tayari kulipa.

NRNE 💪 🔥

EE MUNGU, ibariki nchi YANGU nzuri niipendayo Tanzania 🇹🇿

Nawasilisha 🙏
 
Ukipata janga waliokua wanakushangilia watajitenga na wewe na kuendelea na mishe zao.

Mfano MDUDE NYAGALI hadi leo haijulikani yupo hai ama amekufa.

Watanzania tuache unafiki
 
die or alive 💪🏾💪🏾💪🏾💪🏾
 
Ukipata janga waliokua wanakushangilia watajitenga na wewe na kuendelea na mishe zao.

Mfano MDUDE NYAGALI hadi leo haijulikani yupo hai ama amekufa.

Watanzania tuache unafiki
Wewe ndiye mnafiki uliyejusahaulisha kuwa wanachadema mbeya walikusanyika kudai waambiwe alipo, usiku eneo la ofisi lilimwagiwa sumu Ili kuwatawanya,

Kama unadhani ukimya wao ni unafiki.

Siku yaja.
 
die or alive 💪🏾💪🏾💪🏾💪🏾
Kumbe kuua watu wasio na hatia ni ksawa na kupanda mbegu ambayo ikichipua,

Hatozuilika Tena.

Wanaanzia walipoishia wale waliotangulizwa
 
Wewe ndiye mnafiki uliyejusahaulisha kuwa wanachadema mbeya walikusanyika kudai waambiwe alipo, usiku eneo la ofisi lilimwagiwa sumu Ili kuwatawanya,

Kama unadhani ukimya wao ni unafiki.

Siku yaja.
Na wakakubali kutawanyww hakuna reaction nyingine ilifanyika?
 
Na: Malisa GJ

Ndugu zangu waandishi, hivi mmesahau taaluma? Mbona hamuulizi “inquisitive questions” kuhusu suala la Mpina kuliwa kichwa? Ngoja niwasaidie notes kidogo. Iko hivi, Mpina ameenguliwa kwa mujibu wa kifungu cha 20(6) na (7) cha Kanuni za Maadili za mwaka 2025. Kanuni hizi zilitangazwa kupitia Tangazo la Serikali Na.86 la tarehe 14/2/2025.

Tume iliita vyama vya siasa kusaini kanuni hizo. Chadema tulikataa kusaini kwa sababu zilikuwa na mapungufu mengi. Na tukashauri vyama vingine vigome kusaini pia, mpaka pale kanuni hizo zitakapofanyiwa marekebisho kwanza (Na hiyo ndio maana ya No Reforms No Election). Lakini wazee wa “project” wakaenda kusaini kwa mbwembwe. Kusaini means walikubaliana na yote yaliyopo.

Sasa kanuni zilezile walizosaini ndiyo zimetumika kuwala vichwa. Sasa waandishi, kwa nini hamuulizi hili swali? Muulizeni Ado analia nini wakati alisaini kanuni mwenyewe? Chadema tuliposema kanuni zina mapungufu walitutukana na kusema tumekimbia uchaguzi. Leo yamewakuta, wanarudi kwa wananchi kulia. Ndiyo maana Boniyai amesema hawa watu wanapenda michezo ya “kubakwa”. Bata, Wahed.!
 
Ukipata janga waliokua wanakushangilia watajitenga na wewe na kuendelea na mishe zao.

Mfano MDUDE NYAGALI hadi leo haijulikani yupo hai ama amekufa.

Watanzania tuache unafiki
Kwa hiyo baada ya kuchangia hivi unajiona una akili
Yani mtu anatekwa unasema ni janga
Mtu anapotezwa unasema ni janga
Haya tsunami utasema ni nini
Hebu acha unafki
 
Kwa hiyo baada ya kuchangia hivi unajiona una akili
Yani mtu anatekwa unasema ni janga
Mtu anapotezwa unasema ni janga
Haya tsunami utasema ni nini
Hebu acha unafki
Tuleni mtekwe hadi akili zitakapo kaa sawa
 
Back
Top Bottom