Hata Chavda, Valambia na Rostam siku wakiamua kugombea urais kupitia CHADEMA watatetewa

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
15,997
Amani iwe kwenu.

Hata Chavda, Valambia na Rostam siku wakiamua kugombea uraisi kupitia CHADEMA watatetewa na washikilia ukuta!

Kuna msemo wa Kiswahili husema ‘’tabia haina dawa’’.Nahii ndio hasa inadhihirisha miongoni mwa viongozi na wanachama wa CHADEMA chini ya Mbowe.kwa wale wenye kumbukumbu ya siasa za Tanzania watawakumbuka Valambia,Chavda na Rostam katika harakati zao kibiashara ambazo kwa kiasi kikubwa zililiingiza taifa hasara kubwa. Kwa Tabia ya CHADEMA Chavda, Valambia na Rostam siku wakitoa fedha kwa dhumuni la kukodi chama ili kugombea Uraisi hakutakuwa na pingamizi. Nina sababu lukuki kuthibitisha hoja yangu;

Mbowe na wenzake ni waongo na huenda wanamiliki kiwanda cha uongo.

Mara kwa mara wamekuwa wakielezea wananchi kuwa wao wanachukia ufisadi na mafisadi kiasi cha kuwaorodhesha kwenye tovuti ya chama kinyume chake kumbe Mbowe huwa na mawasiliano ya karibu na mafisadi hao huku akiingia makubaliano nao kwa malipo kukiwa na ahadi ya kuwauzia nafasi za kugombea uongozi ndani ya chama. Kimsingi CHADEMA wanamchafua mtu ili awalipe pesa,ni walaghai kwa wananchi hawamaanishi wanalolisema.

Umasikini, udhaifu na ujinga wa Bavicha.

Mbowe na genge lake wanatumia umasikini, udhaifu na ujinga wa vijana wa CHADEMA kupitisha ajenda zao. BAVICHA wamegeuzwa’’ mbwa koko’’ leo wanaambiwa wamtukane Lowassa kasha wanaambiwa msifieni. Vijana wengi wanatumika sababu ya kutotaka kufanya kazi za kujitafutia kipato. Wamedanganywa kuwa nchi hii kuwa wezi hao wakishinda uraisi watawapa ajira na huduma bure za afya elimu nk. Kwa kuweka rehani vitalu vya gesi. Utasikia wakisema ‘’ Lowassa akishinda shule bure kwa watoto wetu chekechea hadi chuo kikuu’’, waliokuwa wakulima, biashara, kazi nk wameacha na kusuburi muujiza wa Lowassa na kundi lake ambalo kwa muda mrefu waliwatuhumu kuiba rasilimali na kuwatia umasikini. BAVICHA imejaza vijana waanoridhika kwa malipo ya kuwasifia viongozi na wabunge washikilia ukuta kwenye ‘’FB wall’’ zao na wanafurahia kwa hiyo siku Mbowe akiwapa malekezo ya kumsifia Chavda, Valambia au Rostam tutashuhudia ngonjera na mashairi matamu ya kuwasafisha. Ukitaka BAVICHA wakusafishe mlipe Mbowe na ukitaka wakutukane mnyime hela.

Itikadi ya CHADEMA chini ya Mbowe ni pesa na sio siasa safi.

Kwa sasa nafasi za uongozi CHADEMA zitagawiwa kwa wenye fedha, wanaoweza kulipa uongozi na sio wenye itikadi ya kutoa huduma kwa wananchi kupitia siasa. BAVICHA hawawezi kukemea uozo ambao unasababishwa na rushwa inayomea ndani ya chama ambayo kimsingi inaziba fursa ya wao kuwa viongozi baadaye sababu ya matumizi ya pesa kuwanzisha kampeni zisizo na kichwa wala miguu. Mbowe na wenzake walipongundua tu vijana watahoji kuhusu mpango wa maendeleo ya chama kaja na kampeneni ya kushikilia ukuta kwa nia ya kuwafumba wasione yanayotendeka nyuma yao. Kalagabaho!!! Wajinga ndio waliwao!

CHADEMA wanapenda sana siasa za ramli na miujiza.

Huu ni udhaifu ambao umewajaa viongozi na wanachama wa CHADEMA, ikitokea mtu akaleta propaganda ya uongo kama Lowassa alivyowadanganya kuwa yeye ni kila kitu wamwachie mipango yote ya kura za uraisi, kwa sababu akili zao zimegeukia ukuta hawakuangalia nyuma woote wakamwamini, na alivyoshindwa uchaguzi amewaamuru washike ukuta wasielewe linaloendelea anawadanganya kaibiwa kura angali alijitapa yeye ndiye nguli wa wizi wa kura za uraisi. Hivyo kwa mwanasiasa mwenye mbinu za kuajiri ‘’waganga’’ na ‘’manabii’’ maarufu watoe ujumbe kuwa miungu yao imesema wao ndio wameitwa kuwa raisi vijana walizungusha mikono kama ishara ya mabadiliko lakini kwa hili agizo walilopewa kushikilia ukuta viungo pekee watakavyoweza kuzungusha/kukatika ni kiuno na shingo…hivyo tutarajie BAVICHA wakiambiwa na kina Valambia….ukutaaaaa….wao wanaitikia wataitikia huku wamenyoosha mikono mbele mithili ya kibinda nkoi….huku wakizungusha kichwa/shingo na viuno…hizi ndio hathari za kushikilia ukuta.

Kibwagizo cha kufikirisha.
‘’Akili za Mbowe mshikiliaUKUTA zimegonga UKUTA, mwisho wa kufikiri….bila maono CHADEMA UKUTA wamegonga UKUTA hawajui pa kwenda wamebaki kushika UKUTA, Lowassa mshikilia UKUTA kawawekea UKUTA wasijue linaloendelea, wakati UKUTA!.Wabunge washikilia UKUTA wana njaa ya posho wameanza kubomoa UKUTA

‘Siasa ni sayansi’ Dr.Slaa (1.9.2015)

Nawasilisha.
 
waelezeee waelewe maana wanafikiri siasa ni kufanya operations tu, hawakujifunza jinsi wanavyopoteza hela nyingi kwenye hizi operations. Ukiangalia nguvu waliyowahi kuweka kwenye operation sangara na m4c kanda ya ziwa matokeo yake wameangukia pua vibaya sana kanda ya ziwa.
 
Ni hatari, kila siku wanakuja na hoja kuwa watanzania wanauelewa wa siasa,tatizo lao wanafikiri watanzania hao hao hawawaoni wanayoyafanya kuwa ni kinyume cha wanayoyahubiri bado fimbo zaidi zaja.
 
Mimi sioni ajabu kwa chadema kufanya hayo..sababu kama walituaminisha kwa miaka nane kuwa lowasa hasafishiki na wakamsafisha kwa siku moja..kwao hakuna kinachoshindikana..wao kwao unakuwa mchafu ukitofautiana nao kiitikadi..ila ukiungana nao we ni mwenzao
 
Hakika mkuu,akitokea mshikilia ukuta yeyote mwenye uwezo wa kupinga hoja hii atapewa zawadi nono......wengi wanachungulia na kuguna.
 
kuna kampeni inaanza kesho inaitwa 'Shituka' mahususi kkuwang'ofoa wote mlioshikilia ukuta....lazima tukuokoe na udhalimu unaofanyiwa.
leta kejeri kama bado hujaolewa jamaa yangu anatafuta mke bora ni pm

swissme
 
Nukuu nzito hii.

Siku walipotiwa Mbaroni Kitilya na Mkwewe Lowassa Sioi Sumari kwa Ujambazi wa fedha za Umma kwa kutumia Madaraka na usomi wao, Gazeti la Mbowe la Tanzania Daima lilikuja na Headline hii 'MASIKINI MZEE KITILYA'.
Wakati wa JK watu wakifikishwa Mahakamani kwa tuhumza za wizi na kuachiwa huru walikuwa wakipiga kelele kuwa Mahakama zimejaa Rushwa lakin sasa wakati wa Dr. Pombe wanaona Jamaa zao hawatachomoka kwny kesi za Rushwa na Ufisadi wanadai eti Magufuli anaingilia Muhimili wa Mahakama na wanaomba kupitia katika Moja ya Hoja za UKUTA eti Mlalahoi akaandamane avunjwe Mguu kisa kuna kitisho cha kuwa Mafisadi safari hii watafungwa kwa shinikizo la Mh. Rais.
Kama Chadema ilimpokea Lowassa pamoja na Kashfa walizomtupia hakuna Mwana CCM atakaekataliwa kujiunga ikiwa ataonesha dhamira ya kulipa Dau stahiki na nene la kununua Uanachama na hatimae kuwania Nafasi za Uongozi.
 
Peleka ujinga wako Dodoma,hao wote uliowataja ni wafadhili wa Chama Cha Mang'ombe
Unadhani nani alikuwa mweka hazina wenu aliyesimamia upatikanaji wa fedha za kuwaingiza wabunge wenu wote na Mkapa na Kikwete madarakani?
Unajitoa ufahamu kuwa hujui Kagoda ni nini enh!
Ukumbi wa mikutano wenu Dodoma umejengwa kwa fedha za nani? Kwani ulichangia wewe na biashara zako za mihogo ya kuchoma barabarani?
Baki na upumbavu wako ukingoja kuongozwa na remote ya Baba Nanii
Huna uwezo wa kufikiri zaidi ya ukasuku wa yale yale ya siku zote
 
Siku walipotiwa Mbaroni Kitilya na Mkwewe Lowassa Sioi Sumari kwa Ujambazi wa fedha za Umma kwa kutumia Madaraka na usomi wao, Gazeti la Mbowe la Tanzania Daima lilikuja na Headline hii 'MASIKINI MZEE KITILYA'.
Wakati wa JK watu wakifikishwa Mahakamani kwa tuhumza za wizi na kuachiwa huru walikuwa wakipiga kelele kuwa Mahakama zimejaa Rushwa lakin sasa wakati wa Dr. Pombe wanaona Jamaa zao hawatachomoka kwny kesi za Rushwa na Ufisadi wanadai eti Magufuli anaingilia Muhimili wa Mahakama na wanaomba kupitia katika Moja ya Hoja za UKUTA eti Mlalahoi akaandamane avunjwe Mguu kisa kuna kitisho cha kuwa Mafisadi safari hii watafungwa kwa shinikizo la Mh. Rais.
Kama Chadema ilimpokea Lowassa pamoja na Kashfa walizomtupia hakuna Mwana CCM atakaekataliwa kujiunga ikiwa ataonesha dhamira ya kulipa Dau stahiki na nene la kununua Uanachama na hatimae kuwania Nafasi za Uongozi.
Hii ni kumbukumbu nzuri mkuu.
 
Back
Top Bottom