Mbona taasisi za dini zinayafanya hayo yote "Mungu kakupa akili na maalifa bule, kuvitumia ni hiari yako mkuu"Alafu serikali ifanye kazi gani CHADEMA kama chama cha upinzani kazi yake ni kuisukuma serikali kutekeleza ilani yake,CHADEMA hawakusanyi kodi,kama CCM wameshindwa ku-deliver wakae pembeni alafu tuone kama CHADEMA hawatatekeleza hayo yote unayoyasema
Yaani CHADEMA wajenge hospital kwa hizi mia mbili wakati CCM wanakula kodi yetu na hawafanyi chochote!!
Tujadili vitu vya maana tuache masikhara
,Bado nina kadi ya CHADEMA
Maada
Naipenda hii nchi kuliko Vyama na siasa zake, Kabla ya mifumo ya vyama Tanzania ilikua na wakazi na waliishi kwa taratibu na misingi yaliyojipangia wakati huo
CCM wameshindwa kuwawezesha watanzania kupata hata yale mahitaji muhimu (food, cloth, and shalter), ni masikitiko makubwa sana.Wameiba kila kinachoibika na kutuachia MAPANKI. Miaka Hamsini ya utawala wao (huku wakibadili majina ya CHAMA kama ile hoteli maarufu ya jijini DAR "SERENA") Imekua ya machozi jasho na damu.ANYWAY Mungu yupo na sote tunaamini hivyo.
Tatizo langu ni CHADEMA, huu ukombozi tunao uubili tena tukimuingiza muumba "TUMEANZA NA MUNGU, TUTAMALIZA NA MUNGU" unamashaka makubwa sana.Leo kama IKIRUHUSIWA TAASISI ZA DINI KUSIMAMISHA WAGOMBEA kisiasa Kanisa KATORIKI litaibuka mshindi bila shaka. Wamejenga MASHULE, HOSPITALI, VYUO VIKUU, VYUO VYA UFUNDI, HOSTELI, tena vijijini kwa wale waliosahaulika na kadhalika. SI maanishi taasisi nyingine hazijatoa huduma hizi la! ila kanisa hili linaongoza toka enzi hizo.
Kinachonitoa JASHO ni jinsi gani niitofautishe CHADEMA na CCM, Kwani maneno wanayoyatumia sasa hata MAFISADI wa CCM huyatumia wanapoomba kura.Je hizi lugha tamu tamu za ukombozi ntajuaje kua hazitageuka kuwa shubili kama sioni mifano thabiti sasa. Kila kukicha Chadema tunachangishana eti kughalimia uendeshaji wa chama (KWELI!!!!). Kama nia ni ukombozi kwa nini tusianze sasa kutumia michango na ruzuku kujenga hata dispensary vijijini, kununua madawati, kulipia karo watoto wa maskini, kuamasisha watu kujitolea kujenga miundombinu vijijini na nk..
Hatuwezi kujitofautisha na CCM kwa sela za midomoni na kwenye vitabu tu..Tuanze utekelezaji kwa kile kidogo tulichonacho KAMA TAASISI ZA KIDINI ZIFANYAVYO VILE...Kama tunaweza kuhamasisha watu kuunga mkono maandamano yetu (ambayo yana tija pia) tuhamasishe pia wakusanyike na kufyatua matofali ili kujenga dispensary vijijini..Mambo ya HELKOPTA ni anasa kubwa sana kwa mkurya wa kibhancha bhancha, au msukuma wa SAYUSAYU. tunahubili ukombozi wa maskini kwa display ya anasa..Kuna ulazima gani kutumia helkopta katika mikutano ya kawaida kabisa??
Ni muda wa kujitofautisha na CCM kwa Vitendo na si maneno na sela, la sivyo itakuwa ni POROJO tu za kutaka madaraka then BUSINESS AS USUAL. (Mungu kakupa akili na maarifa bure, kuvitumia ni hiari yako)
Hitimisho
Sijahama chama
Mbona taasisi za dini zinayafanya hayo yote "Mungu kakupa akili na maalifa bule, kuvitumia ni hiari yako mkuu"
SONGOKA
,
kama unayo nimapenzi yako, vinginevyo unaficha unafiki wako kwa kauli hii, eleza dukuduku lako badala ya kujishuku nini kitatokea unajihami.
Maada inasema Hata chadema niporojotu - Namimi nasema hata wewe SONGOKA niporojo tu hata title unaibadiliha hapahapa tukuamini kwa lipi
Hili linaeleweka wazi kwamba ccm imeshindwa, watoto, vijana na wazee wanatambuwa fika licha ya kutukata kodi mbalimbali, madin, maliasili na utalii, ccm wameishia kuchakachuwa mapato na kutuacha watanzania tukitaabika
kama tatizo ni chadema jikite kuikosoa chadema mambo ya imani na dini za watu usituchonganihe hapa na siasa zenu za majungu na propaganda.
Mkuu hapa umeniacha hoi umeshindwa kuitofautisha chadema na ccm
1. CCM ni chama tawala na mwenyekiti wake ndiye rais na amirijehi mkuu - Chadema ni chama cha upinzani wala kiongozi wake sio rais
2. CCM ni chama kinachosimamia taifa la tanzania kiutawala - Chadema hakihusiki na usimamizi wowote
3. ccm inamiliki serikali na dola kwa ujumla - Chadema haimiliki serikali wala dola
4. Ccm kupitia serikali yake inamiliki makusanyo yote ya kodi - Chadema haimiliki mfumo wowote wa mapato
Tuangalie hayo machche hasa no 3 na 4 kwanza..........
1. Unataka chadema ifanye maendeleo kwa mapatogani? kwa fungu gani? hiyo nauli wanayoombaomba waitumie kujengea shule watatufikiaje huku vijijini na mikowani kutufungua vichwa vyetu ilikuzifahamu haki zetu za msingi?
2. Unataka chadema ifanye maendeleo ya wananchi jukumu la chama tawala ninini na kwanini tuwape kodi zetu nk, chama tawala wanawajibugani katika kutekeleza haki za wananchi? Je hili pia jukum la upinzani?
Tatizo siyo kuhama bali maamuzi yako tu, democrasia inakuruhusu kuhama, kubakia hata kuanzisha chama chako kama
Mtikila. Sisi haituhusu demokrasia ya maamuzi yako.
Inahitaji akili na utashi wa kumuelewa mtoa maada na maada yake.Ni ngumu kwa mshabiki wa chama kukuelewa bali kwa mtu anayefikiri na kuwaza kwa kina hoja yako ina nguvu mtoa maada.ULIYOYASEMA INAWEZEKANA BILA KUJALI UPO MADARAKANI AU LAH.
mkuu umenisaidia sana kufikisha ujumbe (bila kujua): Je ni kweli kwamba CHADEMA INASUBILI KUSHIKA DORA ndo iwasaidie wananchi?? Je ghalama za kurusha helcopta ni kiasi gani?? Kama mwanachama makini lazima nikikosoe chama.
mkuu umenisaidia sana kufikisha ujumbe (bila kujua): Je ni kweli kwamba CHADEMA INASUBILI KUSHIKA DORA ndo iwasaidie wananchi?? Je ghalama za kurusha helcopta ni kiasi gani?? Kama mwanachama makini lazima nikikosoe chama.
mkuu umenisaidia sana kufikisha ujumbe (bila kujua): Je ni kweli kwamba CHADEMA INASUBILI KUSHIKA DORA ndo iwasaidie wananchi?? Je ghalama za kurusha helcopta ni kiasi gani?? Kama mwanachama makini lazima nikikosoe chama.
Wa TZ wamechoka Sela na maneno...tuanze utekelezaji wa ilani kwa kidogo tulichonacho....(muda wa porojo umekwisha)unataka kusemaje songoka? kwamba tuiache ccm iendelee kutawala kwa kuwa hata cdm watakuwa au wako kama ccm? kwanza hawako kama ccm, hapo juu umefafanuliwa vyema, ccm inamiliki resources zote za nchi na wanapaswa kuleta maendeleo yanayofanana na resources zetu na sio ziingie mifukoni na kuwanufaisha wachache.
yaani hiyo gharama ya kurusha helikopta wewe ipige kila ukiamka, kama wameweza ni big up kwa cdm. ulitaka wawafikieje majority ya watanzania waishio sehemu tofauti tofauti? watembee kwa miguu? sehemu zisizo na barabara wafike vipi?! hizo cost haziepukiki, kuna muda pia unaohesabiwa kama sehemu ya gharama, ukiweza kutumia muda mfupi kufanikisha jambo ambalo lingekugharimu muda mrefu sana kwa utaratibu wa kawaida ni faida.
mbona ccm wameiga last time helikopta? au hukuwaona japo wala hawakuwa na sababu ya kwao zaidi ya kufikiri kuwa cdm kutumia helikopta ni swaga tu, kwa hiyo usijaribu kuwaambia watz kuwa cdm wanafuja kwa kutumia helicopta, zaidi cdm wamefanikiwa kuwafikia watanzania wengi zaidi na ndio unaona kabisa matokeo yake, watu wengi wamejitambua na wamebadilika
Mkuu, subiri wafia chama waporomoshe matusi dhidi yako