Hata Bibi aliwahi kuwa Mwali

Kichwa Kichafu

JF-Expert Member
Apr 13, 2017
44,574
188,785
Habari,

Hivyo ndivyo ilivyo kwa kila kitu mara nyingi mwanzo huanza kuwa bora na kizuri ila kadri muda unavyokwenda itafika wakati hukoka na kuchakaa/ kukongoroka kabisa.

Napenda kuwakumbusha vijana wa kike/ mabinti/ wasichana na wanawake wenye miaka around 20's (20 - 2) kuwa kuna msemo usemao Hata Bibi Alikuwa Mwali.

Usipende kuishi bila malengo, nakukumbusha kuna wakati utakuwa katika peak ambayo kila mtu atagundua upo kwenye ubora na thamani kubwa.

Hapo hapo ni kipindi kizuri kufanya makubwa kama umejitambua vyema.

Ila ukipitiwa na usingizi na kusahau misingi ya nini wazazi na jamii husimamia hakika utapotea na baadae tutakumbusha kwa huu msemo huo.

Napenda kuwaasa kwa wote ambao mpo kwenye kundi hilo kuweni makini na kushika yote ambayo jamii kwa kipindi cha nyuma ilikuwa inaimba.

Nawasilisha Mzee Mkoloni

Cc: Kichwa Kichafu
 
Back
Top Bottom