Hashiki mimba nataka kumtimua

mansnipe

Kuwa mvumilivu, mzee .. Kuna rafiki yangu ameishi na mke tangu 2005, na kabla ya hapo walikuwa wapenzi tangu mwaka 2000. Wamekuja kupata mtoto mwaka jana 2014 .. Kuwa na huruma, kama watoto tayari unao wawili, presha ya nini? Vipi kama hilo tatizo lingekuwa kwa upande wako?
 
Last edited by a moderator:
ILO tatizo ndo KM linalomsumbua wife wangu Mimi,,,tunataka mtoto wa pili,mirija imeziba sababu ya sindano za uzazi,,tulienda kupima kwa KAIRUKI HOSPITAL kwa garama km ya laki mbili ndo tukaambiwa hayo ya kuziba mirija,,,,kwa DOKTA MWAKA JUZI TUSHATOA LAKI TATU KAPEWA DAWA anatumia kujaribu pia,,,,KIUKWELI IZI NJIA ZA KUZUIA MIMBA WANAZOTUMIA KINA MAMA,,HAZIFAI KABISA KABISA
 
wew timua tu mkuu..ucckilize manemo ya humu
 
Poleni sana.
Njia pekee salama ni kalenda...mkishindwa condom.... bahati mbaya wanandoa wengi kula pipi na maganda hushindwa.

Njia nyingine zilizobakia ni majanga....ila msiache matibabu



 
Tatizo la ndoa zetu hizo

Mke anaolewa na ndugu jamaa na marafiki

Kutwa kuulizia kama tayari au bado

Utafikiri watawasaidia kulea
Ukiangalia yatima wanavyoteseka mtaani utadhani hao wazazi wao hawakuwa na Ndugu , napata kichefuchefu sana kusikia eti Ndugu wanafuatilia ndoa ya mtu mwingine kisa hawajabahatisha mtoto.
Ndugu wengine utasikia wawili tu ? Hawatoshi hao.
Duh! Hivi wanawahusu nini?
 
Hapana mkuu sindano au vidonge vya uzazi wa mpango haviwezi kusababisha mirija ya mayai ya mwanamke (fallopian tubes) kuziba.
Kitu pekee kinachosababisha hiyo ni kuvilia kwa mirija baada ya kupata maambukizi ya bakteria ( Pelvic inflammation disease) , hivyo njia ya kitanzi nayo huweza kupelekea kusababisha PID...... Google itakusaidia vizuri.
 
Inaelekea wewe ni mtu mwenye roho mbaya kama sura yako. Je ungependa itokee hivyo kwa dadaako au mwanao?

Mkuu chukua tano! we unadhani huyo anaetaka kumwacha mwanamke kisa kamtumia kamchoka halafu anasingizia hampendi ataelewa maumivu ya mwanamke atakae achwa kisa hazai?
 
Mtoa mada kuzaa majaliwa.Na kazi ya mungu hiyo mpe support wife muombeni mungu atawajibu tu.
 
Je miezi 18 tangu aache sindano za uzazi wa mpango imepita? Km imepita kuna tatizo ambalo jitahidi kuwaona wataalamu
 
Huyo dada kuna ambalo Mungu anamuepusha kuzaa nawe.
Ukute huna siku nyingi za kuishi so mke asijekusumbuka na watoto wawili.
Nimewaza tu.
 
manSniper

Aisee wewe ni mdhaifu sana ni mapema mno kuzaa nje ya ndoa angali mkeo anaendelea na matibabu
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…