Ubumuntu
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 14,316
- 10,782
Hasheem ana muda mwingi wa kufanya vizuri, walipomchukua walijua kuwa ni long term project. Sasa hivi Rockets wanacheza vizuri so hawawezi kumpa Thabeet muda na kuvuruga timu ili dogo apate experience. Kwa kifupi unless aumie au awe na nidhamu mbaya sana (hakuna habari yoyote ya kukosa nidhamu) Thabeet atakuwa NBA kwa miaka mingi ijayo, kwasababu ya urefu tu.
Mkuu kumbuka huyu dogo wetu ana umri mdogo sana na anatakiwa kujituma katika hiyo age aliyo nayo wenzake waliingia wakiwa na age ndogo kuliko hiyo yeye anachopaswa ni kufanya workouts sana na sio mchezo sasa tatizo lake wakati wa mapumziko dogo anakuja Dar kula raha wakati wenzake wanajifua, check hao ma super star kama Lebron James ukiangalia jitu liko huko juu lakini workouts zake usipime sasa dogo wetu yeye ameridhika nini sasa hakuna wa kumshauriiiii watu wanajiuliza ni kulikoni au hana hama na hiyo game kajilazimisha au?
HT sasa ana miaka 25. Angalia Blake Griffin ana miaka 23; Kevin Durant ana miaka 24; Serge Ibaka ana miaka 23; Derrick Rose ana miaka 24; James Harden ana miaka 23; Brandon Jennings ana miaka 23; O.J Mayo ana miaka 25 (tena huyu alikua nae Grizzlies).
Hawa ni baadhi ya wachezaji vijana wanaotamba vibaya mno NBA.
Sasa kusema HT bado ni mdogo sana na muda mwingi, mnakua mnakosea. Lebron tayari ana miaka 28, na hao vijana hapo juu wanatishia utambaji wake; sasa kwa mtizamo huu, HT akiendelea kuwa katika kiwango alicho sasa, hakika hana muda mwingi ataondoka NBA.