Hasara za ushauri wa rafiki kimapenzi.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hasara za ushauri wa rafiki kimapenzi..

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by arnolds, Nov 25, 2011.

 1. arnolds

  arnolds Senior Member

  #1
  Nov 25, 2011
  Joined: Oct 10, 2009
  Messages: 105
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Watu wengi wamekuwa wepesi sana kukimbilia kwa rafiki zao ili kuomba msaada wa mawazo ya nini wafanye kwenye mapenzi. Imani iliyojengeka kwa watu wengi katika jamii yetu ni kuwa ushauri ni kitu muhimu sana kwa kila hatua.

  Unapokerwa na mpenzi unakimbilia kushauriwa na wakati mwingine hata unapotaka kuoa au kuachana na umpendaye, unamuomba rafiki yako ushauri.
  Je, umeshawahi kufikiria hasara za kuomba ushauri wa kimapenzi kwa rafiki yako? Hebu tujadili kidogo hasara unazoweza kuzipata.

  UTAKUPOTOSHA
  Ni wazi kwamba kipimo cha uelewa kinatofautiana kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine. Ifahamike kuwa, uhodari wa mambo nao hutofautiana, mtu anaweza kuwa mahiri katika siasa na akaaminika kwenye jamii, lakini ukimpelekea suala la mapenzi anakuwa hajui kitu, hivyo ni rahisi kukupotosha.

  Uchunguzi unaonyesha kuwa, wapenzi wengi sana hupotoshwa na rafiki zao wasiokuwa na uelewa wa kutosha juu ya tatizo au suala husika la kimapenzi. Ni vema kuwa makini unaposhauriwa.


  UTARAHISISHA MAMBO
  Mara nyingi washauri huwa si wao wanaokabiliana na mambo, hivyo ni rahisi kwao kupima vitu kwa juu juu tu na kushauri kirahisi rahisi. “Vipi kakupiga namna hii, aaa huyu si mwanaume kwa kweli ni bora ukaachana naye.” Anasema ni bora kuachana naye kwa sababu haumizwi na kuachana, unayeachana ni wewe anayekushauri.

  “Mkubali tu bwana unalaza damu, hiyo tabia yake ya uhuni atabadilika, shosti unataka kuacha bahati ipite?” Kwa mshauri ni rahisi kusema hivyo lakini kumbuka ukubwa wa tatizo hatimaye utakabiliana nao wewe. Hii ina maana kwamba, unapofikiria kuhusu ushauri ufikirie pia kuhusu kushauriwa jambo kirahisi, ukiuvaa mkenge mwenye kuumia utakuwa ni wewe.

  UTAKUGEUZA
  Ulimwenguni kuna aina zaidi ya 1000 za mapenzi na kila mmoja anatajwa kupenda kwa staili zake. Mapenzi ni kama chembe hai nyekundu zilizopo kwenye damu ya mwanadamu ambazo zinaelezwa na wataalamu kuwa hazifanani hata kidogo. Uzoefu unaonyesha kuwa, washauri wengi hushauri kwa uzoefu wao, lakini je ni sahihi uzoefu huo uwe msaada kwa mtu mwingine?

  Jibu ni hapana, kinachotokea mara nyingi kwenye ushauri ni mtu kumfanya mwenzake awe kama yeye alivyo, yaani apuuze aamue na apende kama staili yake, jambo ambalo haliwezekani kabisa kwenye mapenzi. Vipi Juma ageuke ghafla awe kama Hassan kwenye suala la mapenzi? Ushauri ni muhimu lakini upime kama unalingana na matakwa yako.


  UTAKUONDOLEA UJASIRI
  “Kwa maelezo hayo mumeo ni malaya sana, naona itakuwa vigumu kumbadilisha, ni bora ukaanza maisha yako kwa sababu kuna siku hali itakuwa mbaya.”
  Huu ni ushauri ambao unaweza kumuondolea mtu ujasiri wa kukabiliana na tabia ya mumewe hadi kufikia hatua ya kumsaidia akaachana na tabia zake mbaya.

  Ushauri huondoa ujasiri wa kukabili tatizo hasa pale anayekushauri atakapolipeleka suala lako kwenye njia ngumu isiyokuwa na ufumbuzi. Ikumbukwe kuwa anayeamini kushindwa ni mshauri lakini wewe kama mwanamke unaweza kusimama kutetea penzi lako na kuliweka sawa mpaka jamii ikasema: “Jamani huyu dada kamrekebisha kweli mumewe, hakuwa hivi alikuwa mlevi lakini sasa kaacha pombe.

  UTAKUNYIMA FURSA
  Kwenye mapenzi kuna fursa nyingi za mafanikio ambazo unaweza usizipate ukiwa mtu wa kusikiliza sana ushauri wa watu. Kuna wakati ambao unatakiwa usimame wewe kuamua kumpenda mtu ambaye jamii inaona kama utapotea..
   
 2. mpoleeee

  mpoleeee JF-Expert Member

  #2
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 310
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Darasa tosha hili. Tafanyia kazi.
   
 3. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #3
  Nov 25, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,227
  Trophy Points: 280
  ndo maana ukishauriwa inabidi ukae utafakari, si lazima ufanyie kazi ushauri uliopewa ukiona unakufaa uchukue usipokufaa achana nao by the way asante kwa darasa.
   
 4. kashengo

  kashengo JF-Expert Member

  #4
  Nov 25, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 2,649
  Likes Received: 464
  Trophy Points: 180
  Mshauriwa siku zote huwa kashaamua moyoni...thats why ukimshauri vingine atafanya vingine(hasa katika mapenzi) mfano "achana nae huyo atakuua na maradhi" kesho kutwa unamwona mjamzito unabaki kushangaa sasa mi huwauliza wee waonaje kabla sijakushauri? Maana siku zote anataka umpe go ahead...Utamsikie ujue hata mimi naona hivyo hivyo kama ulikuwa rohoni kwangu...kinyume na hapo anakwenda mwambie mwenziwe "eti kasema utaniua na maradhi" sijui mnalijua hili?
   
 5. Tausi.

  Tausi. Senior Member

  #5
  Nov 25, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 125
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Asante kwa darasa, safi sana.
  Tunaomba utatuwekea na "HASARA ZA KUTOOMBA USHAURI,
  A.K.A KUTOA MAAMUZI BILA KUMSHIRIKISHA MTU.:poa
   
 6. Tausi.

  Tausi. Senior Member

  #6
  Nov 25, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 125
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kweli kabisaaaaaaaaaaaa,
  na hufanya hivyo ili aone wewe utamshauri vipi? Utaendana na maamuzi yake au lah!
  Lakini maamuzi tayari keshaamua mwenyewe.
   
 7. kashengo

  kashengo JF-Expert Member

  #7
  Nov 25, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 2,649
  Likes Received: 464
  Trophy Points: 180
  unatakiwa uwe na busara sana kuwashauri wapenzi na usipende kuwashauri wa break up itakugharimu sana! Kuachana waachane wenyewe we wape moyo tu ..."unajua mapenzi ndo yalivyo" nk lakini ukijifanya we bonge la Hitch itakula kwako
   
 8. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #8
  Nov 25, 2011
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Umenikumbusha wimbo huu wa zamani sana ....

  " .... bibi na bwana wakigombana nyumbani, waache wenyewe mpaka waelewane, lakini usiwaingilieeeeee eheeee wakipatana; utakuja kubaki na aibuuuu eheeeee, mtoto wa mamaaaa! ..."

  Kimsingi ushauri una umuhimu wake, ila kikubwa ni kwa mtu anayetoa ushauri kufikiria beyond the box, na pia kuwa muungwana kwa kutoa ushauri wa kujenga zaidi kuliko kubomoa. Pia unayeshauriwa unatakiwa kuwa na busara, siyo kila ushauri unauchukua kama ulivyo! Akili za kuambiwa, changanya na zako!
   
 9. bryleen

  bryleen Member

  #9
  Nov 25, 2011
  Joined: Jul 28, 2011
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  i lyk da class na ni kweli tupu.ngoja nijipange upya:shock:
   
Loading...