Sukari Yenu
JF-Expert Member
- Dec 8, 2014
- 1,698
- 1,261
Habari wakuu,
Mada tajwa hapo juu yahusika. Nazungumzia harusi sio ndoa, naomba kueleweka na kuweka wazi hilo.
Mimi ni kijana ambaye bado sijaingia kwenye ndoa lakini hali ya ndoa ambapo harusi hufuata ninavyoiona sijui itakuwaje siku nitakapofikiria kuowa. Nina sababu zangu. Nifuatilie hereunder.
Mtazamo wangu upo kwenye hali ya harusi za miaka ya nyuma na miaka ya sasa. Zamani, sherehe za harusi zilikua kitu chenye kuheshimika, kuogopwa, chenye element za kiibada na/au kiimani zaidi. Harusi zilikua kitu kinachomtofautisha mtu na mazingira ya kawaida. Harusi zilikua harusi kweli kweli. Kulikua na haja na mahitaji kweli kweli ya kufanya sherehe za harusi. Miaka ya 1990s nilikua bado nasoma shule ya msingi, lakini nilikua nikiona sherehe za harusi na mazingatio yake bado ninayo kichwani. Nilikua nikiona, kwa mfano, mabibi harusi hata wakidondosha machozi kuonesha namna gani wameguswa na harusi kufuatia ndoa yao.
Siku hizi harusi hazina maana tena, bwana na bi harusi wamechangamka mno tena kupita kiasi kama mchuzi wa sato uliotiwa limao ya Ukerewe. Yaani wahusika wahusika wakuu wa harusi wanakua hovyo utafikiri wako disko la shule ya boys na girls zinapokutana. (Enzi zangu Tosa boys na Iringa girls). Wanataka sifa zaidi na hufanya sherehe isiwe na ladha. Sijui ni kwa sababu bwana na bi harusi wamejuana muda mrefu, sijui.
Wazo langu ni nikifikia kuoa, nitafunga ndoa bila harusi. Upande wa mke wangu na yeye pia wajiandae kwa hilo kisaikolojia.
Ni mtazamo tu.