Harusi ya Messi sasa kufanyika Juni 30, kocha wake wa zamani Luis Enrique hajaalikwa

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,692
2,000
messi-salehjembe.jpg

Harusi ya mshambuliaji nyota wa Barcelona, Lionel Messi sasa ni uhakika itakuwa Juni 30 na itafanyika kwao Rosario, Argentina yeye akifunga ndoa na mzazi mwenzake na mpenzi wake tokea wakiwa shule, Antonella Roccuzzo.

Awali ilielezwa, beki Gerard Pique rafiki wa Messi hakualikwa kwa kuwa mkewe Shakila haelewani na bibi harusi mtarajiwa.

Lakini kinachoonyesha kuwashangaza wengi ni kutoalikwa hata kwa Kocha Luis Enrique ambaye ameamua kuondoka Barcelona lakini madaktari wa Barcelona na kocha mpya, Joaquin Valdes ni kati ya waalikwa.

Sherehe za harusi hiyizo zitafanyika katika hoteli ya Pullman ambayo tayari vyumba 250 vimelipiwa na baadhi ya wageni wamekuwa ni siri.
Pia imeelezwa viongozi wengi wa klabu ya Barcelona hawajaalikwa na Sergio Aguero ni kati ya walioalikwa.

Taarifa nyingine zimeeleza jumla ya watu 21 kutoka katika kikosi cha Barcelona wamelikwa na tayari maandalizi ya “kufa mtu” yameishaanza.

Chanzo: Salehe Jembe
 

nankumene

JF-Expert Member
Nov 12, 2015
5,916
2,000
kama akialika wote wanaofahamiana zitahitajika hotel za mji mzima,wengne wabak nchin kwao wafny kazi..hapa kazi tu
 

GREGO

JF-Expert Member
Apr 3, 2014
4,152
2,000
Labda alipewa kadiya mchango akaingia nayo mitini..........Hii hali ya ugum wa kuchangia harusi kumbe haipo kwetu tu
 

Atwoki

JF-Expert Member
Aug 22, 2015
491
250
Oyo,oyooooo naskia mond ,mzee chibu Platnumz ,yupo nae pia kaalikwa jamani , wapi kiba aah ah chali
 

nkuwi

JF-Expert Member
Feb 11, 2013
3,850
2,000
Huyu andunje kumbe ana roho mbaya kama faru John WA tz!!!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom