Baraghash
JF-Expert Member
- Dec 18, 2012
- 2,713
- 1,789
Katika tukio la kihistoria,Wanachi wa Uingereza wameungana kuurejesha Uhuru wao uliopotezwa kwa kisingizia cha Muungano wa nchi za Ulaya, EU.
Kiongozi wa chama cha kisiasa, UKIP,Nigel Farage alisema tarehe 23 June kila mwaka iadhimishwe kuwa ndio " Indipendence Day" ya UK
Waziri Mkuu David Cameron,pamoja na kutaka nchi yake ibaki kwenye EU,alisema kauli/ maamuzi ya wananchi ya kutaka ijitoe lazima yaheshimiwe.
Nilimkumbuka Jecha wangu wa Zanzibar, na nikajiuliza nchi kubwa kama UK inawezaje kukosa Jecha? Kumbe wenzetu haki, usawa na demokrasia ni tunu ya Taifa lao
Brexit ni kifupi ya harakati zenye lengo la kisiasa UK ambalo lilikuwa likitafutwa na watu tofauti, makundi ya watu watetezi wa haki na wanasiasa ima kubaki EU au kujitoa. Harakati hizi zimeamsha ari iliopotea kwa nchi zilizokuwa zinakadhia inayolingana ya kutawaliwa.
Wana siasa wetu wa Zanzibar waje na kitu kama hiki,Znexit,idai kufanyika kura maoni sambamba na kura ya maoni ya Katiba mpya, kuulizwa hasa Wazanzibari kama wanaona kama kuna haja kusalia chini ya himaya ya Tanganyika kwa kisingizio cha Muungano au kujitawala tena. Pamoja na kuwa wazanzibari walishaamua Serikali wanayoitaka ya Mkataba kwa zaidi ya asilimia 60% lakini maamuzi yao yalibezwa.
Inatuumiza matumbo kuiona kisiwa/nchi kama Cape Verde, kisiwa kama Zanzibar, sote tumewahi kutawaliwa na mreno, sote visiwa vyetu vilitumika katika biashara ya Utumwa, sote tumevumbua lugha zetu Cape Verdean Creole/ Swahili, sote tuna uchumi unaoweza kuimarishwa na idadi ya watu ya wenzetu ni laki sita tu mara mbili ya Zanzibar lakini wako huru na GDP yao per capita ni US$ 4,000, sisi tunadaiwa baada ya kuburuzwa kwenye Muungano.
Leo Zanzibar haiwezi hata kujiunga na EAC wakati kabla hatujamezwa tulikuwa wanachama kamili na tuna kura. Hongera UK kwa kutuamsha.