Harufu ya utapeli juu ya ununuaji gari mtandaoni

Harufu ya utapeli juu ya ununuaji gari mtandaoni

Sio matapeli hao ila wanakera. Nimewablock namba zao kwani wanakupigia kila siku. Hat ukiwaambia ushanunua gari hawakati tamaa. Just block the numbers. Wana assume kila mtu ni dealer wa magari kwa hiyo utakuwa unanunua kila wakati.
 
hahahha SBT ndo walivyo
mie nilikua naongea nao kila kukicha..nikichoka nampa dogo aongee nao..
wanajali sana..

tukiweka na home address hawa jamaa watakua kutwa wanabisha hodi makwetu
Mimi nilikosea nikaweka physical address ya ofisi yangu.

Mara hao alikuja mjapani mmoja na mswahili mmoja wakaanza kunielezea ubora wa gari zao na jinsi walivyo fasta kufanya delivery kwa mteja pindi ukamilishapo details zote.

Ila sikununua kwa kipindi kile kwa sababu nilikuwa nimeshaagiza phoenix yangu kutoka China.
 
Wanajamvi katika harakati za maisha nikaona kea sasa kutokana na shughuli zangu basi si vibaya kumiliki gari ili kuweza kwendana na kasi ya hili jiji na maisha kwa ujumla.

Basi nikaanza kupitia pitia mitandaoni ..ndipo nilipokutana na mtandao mmoja wa sbt japan.kwa kuwa nilivutiwa na bei zao na nikaona kuna sehem ya kujisajili basi nikajisajilia na kwa bahati mbaya nikaandika namba yangu ya sim.

Haikupita siku mbili nikapokea sim kwenye namba hii +81 45-290-9485 na jamaa akajitambulisha kwa majina ya kijapan amabayo siyakumbuki na kusema kaona mim natafuta gari na kuniuliza aina gani ya gari nahitaji.nikamtajia huku akiongea kiengereza kibov kwa lafudh ya kijapan .

Kikubwa nilichowaambia kwamba kwa sasa sina mpango wa kununua gari ila mwezi ujao ndio nitanunua.

Wakasema sawa basi kwenye email yako nimetuma picha za hiyo gari

Haikupita wiki wakapiga tena sim na kusema kwamba kuna offer kwa sasa na magari ni bei rahisi zaid kwa hiyo bora ninunur sasa na safar hii alikuwa mwanamke niliyeongea nae kwa kiingereza tena ...nika mwambia sawa ila mimi kwa sasa sina hela .akakata sim haikupita siku nyingi akkapiga sim nikaona ni usuumbufu sikupokea ...ikawa anapiga mara kwa mara nokawa sikupokea mara kuna siku akabadili namba na kupiga namba inayo anzia na +255 na namba zingine kupokea akajitambulisha yule jamaa wa kwanza kuwa anapiga sim kutoka japan...ikabidi nikate sim na kuangalia vizur labda macho yangu yalinidanganya lakin nikaona ni code za tanzania

Basi akapiga nikawa nakata mara kwa mara ..

Ikapita kama miezi mi 4 leo wakapiga tena safari hii ni. sauti tofauti naa zile za mwanzo kwanza akasalimia kwa kiarab ..kisha kwa kiswahil halaf kwa kingereza ....mi nikamjib kwa kiswahili ..kwamba sema shida yako..nikaona kaongea kwa kiswahili..hapo hapo nikaanzaa kumtukana mpaka kakata sim.
Siyo matapeli ni kwamba umezoea customer care za kibongo wale wko serious na biashara.
Utapokea emails na simu zao wakikutaarifu magari waliyo nayo kila mara kwakuwa ulitengeneza acc kwenye mtandao wao.
Narudia siyo matapeli ni custimer care and marketing ya kiwango cha juu wanakusawishi ununue tofauti na biashara za kitanzania mteja atakuja mwenyewe.
 
Ok nimewaelewa wakuu ahsanteni kwa ufafanuzi huuu
 
Back
Top Bottom