Harufu ya ubingwa yatawala Jagwani, TFF yaipora Azam pointi tatu

Casuist

JF-Expert Member
Jul 23, 2014
1,189
2,970
Habari wakuu,
Leo shirikisho la mpira wa miguu nchini(TFF) limetangaza kuwapokonya timu ya Azam pointi tatu kwa kosa la kumchezesha Erasto Nyoni aliepaswa kutumikia adhabu kutokana na kuwa na kadi tatu za njano hivyo hakupaswa kucheza kwenye mechi waliocheza dhidi ya Mbeya.

TFF imeitunuku timu ya jiji la Mbeya(Mbeya city) pointi tatu za mchezo huo na kutoa onyo kwa klabu ya Azam.

Nyoni L.jpg

Timu ya Azam FC imenyang’anywa pointi 3 na mabao 3 baada ya kupatikana na hatia ya kumchezesha Erasto Nyoni aliyekuwa na kadi 3 za njano katika mchezo namba 156 baina ya Azam FC na Mbeya City uliofanyika uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

Kwa mujibu wa ofisa habari wa TFF, licha ya Mbeya City kupewa pointi 3 na mabao 3 kwa mujibu wa kanuni za TFF, benchi la ufundi la Azam FC limepewa onyo kali na kuelekezwa kuwa yasiji rudie tena makosa kama hayo

Kwa uamuzi huu sasa ni rasmi Yanga ni bingwa VPL kwa msimu wa 2016/2016, vile vile kuna uwezekano mkubwa kwa Simba SC kuwa washindi wa pili.
 
amna shida c wataenda shirikisho bhana,
 
Itakuwa Yanga walitoa pesa ili Azam imchezeshe Nyoni wapokwe point 3. Sio bure maana kila kitu ni Yanga. Teh teh teh
 
amna shida c wataenda shirikisho bhana,
Shirikisho anakwenda bingwa wa FA cup, kwa kuwa Simba alishatolewa basi Azam ana uhakika wa kucheza Shirikisho kuliko Simba. Kwa Yanga wanabadiri gia na kuongeza nguvu ili wachukue vikombe vyote viwili - FA na VPL.
 
Itakuwa Yanga walitoa pesa ili Azam imchezeshe Nyoni wapokwe point 3. Sio bure maana kila kitu ni Yanga. Teh teh teh
Yanga haihitaji kusaidiwa na TFF ili ichukue ubingwa. Ina advantage kubwa sana hadi hapa.
 
Huko kusaidiwa ndiko kulikoifikisha hapo. Watu hawazungumzii kubebwa katika mechi zijazo, bali katika mechi zilizopita.
 
Back
Top Bottom