Harufu mbaya ya mkojo - Msaada

Ningelikushauri uende tena Hospitali Kuu ya hapo ulipo hata kama Hospitali ya kulipia itakuwa ni bora ukapimwe ili ijulikane una matatizo gani kwenye hicho kibofu chako cha mkojo. Mkuu Njaa
 
Wakuu nilileta uzi wangu wa kuomba msaada kuhusu harufu mbaya ya mkojo wangu, lakini sijui ilienda wapi? mambo yapo hivi

Kwa muda wa miezi kadhaa sasa nimekuwa nakujoa mkojo mchafu sana tena wenye harufu mbaya mno, mambo yanakuwa mabaya zaidi hasa asubuhi maana mkojo unanuka kama mfereji wa maji machafu ya chooni.

Nimetumia dawa kadhaa za hospital bila mafanikio, nimebadili vyakula bila mafanikio, nimejaribu kunywa maji ya madafu bila mafanikio......Najua kuwa humu ndani kuna kila aina ya watu, please nipeni msaada juu ya hili

Nawakilisha

Chukuwa mdalasini iliyosagwa unga vijiko vitatu vya chakula, vijiko vitatu vya asali mbichi vya chakula, weka kwenye glass au kikombe cha maji ya moto, koroga, kunywa kama chai, kutwa mara tatu namna hiyo halafu baada ya wiki moja njoo hapa ulete jibu.
 
Maji,
Hiyo ni dalili ya dehydration. Kunywa maji angalau lita tatu kwa siku, mkojo hautanuka.
Punguza alcohol, caffeine, nyama (urates) na kama unavuta msuba, punguza kidogo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom