Tatizo la kuwa na harufu mbaya kinywani (bad breath) - Chanzo, dawa za kuzuia na ushauri

Rejea kwenye title husika hapo juu

Habari zenu wana jf
Leo nimeona kuna tija ya kujulishana tips mbalimbali za kuweka kinywa kiwe safi ili kuepuka harufu mbaya


Kutosafisha kinywa vizuri
Kwa kawaida unatakiwa kusukutua kinywa chako angalau mara mbili kwa siku - asubuhi na usiku kabla ya kulala. Wakati wa kusafisha kinywa, hakikisha umesugua vizuri ulimi. Meno na fizi havina tatizo sana, bali ulimi ndio sehemu kubwa ambapo bakteria wanajijenga. Vilevile, ni ulimi unaosababisha kinywa kunuka. Ni vizuri kama utasafisha vizuri ulimi ili kuondoa harufu.

Ni vizuri kufahamu kuwa mswaki unatakiwa kubadilishwa kila baada ya muda - angalau kila mwezi. Usitumie mswaki kwa muda mrefu, maana hauwezi kusafisha kinywa chako kwa ufasaha kama inavyotakiwa maana wengine wanatumia mswaki kwa mwaka na zaidi. Je utaacha kunuka kinywa?

Kutokula chakula vizuri
Harufu ya kinywa inaashiria kutokula chakula na kinywaji kwa muda mrefu. Kuwa na njaa husababisha mdomo kuwa mkavu. Mara nyingi harufu mbaya ya kinywa hupotea mara tu baada ya kula chakula kizuri na mdomo ukiwa una mate ya kutosha. Acha kutumia vyakula na vinywaji vinavyoongeza harufu kali mdomoni na kukupunguzia maji mwilini – mfano pombe, viungo kama kitunguu maji au kitunguu saumu.

Kinywa kikavu
Bakteria hushamiri kwenye kinywa kikavu. Kama hupendi kunywa maji mengi na kinywa chako kinakuwa kikavu mara nyingi basi jua kuwa kunuka kinywa kwako ni jambo la kawaida.

Jinsi ya kutatua tatizo

Hakikisha mdomo haukauki

Kwa kawaida mdomo mkavu hutoa harufu mbaya. Hii ndio sababu kuwa kinywa chako kinanuka sana asubuhi sababu mdomo wako unatengeneza mate machache sana ukiwa umelala. Mate ni adui wa harufu mbaya mdomoni siyo tu sababu inaondoa bakteria na masalia ya chakula, bali mate yana vimengenyo vinavyoua na kuzuia kuzaliana kwa vijidudu kwenye kinywa. Ili kuzuia kunuka, jaribu kufanya haya

Kunywa maji mengi ili kuondoa masalia ya chakula na bakteriaTafuna bazoka, sababu bazoka inasababisha mdomo kuwa na mate mengi. Kuwa makini katika kuchagua bazoka zisizo na sukari. Sukari ni adui mkubwa wa kinywa chenye afya.

Piga mswaki kabla ya kulala
Kupiga mswaki ni muhimu, lakini wengi tunasahau kuwa mswaki ni lazima kupiga angalau mara mbili kwa siku haswa usiku naasubuhi. Kupiga mswaki asubuhi ni muhimu ili kuondoa uchafu uliojijenga usiku kucha na hivyo harufu mbaya - lakini siku nzima mdomo unatengeneza mate na kuwa laini. Hii ni tofauti na usiku. Usiku mdomo hubaki mkavu na mate kidogo, hivyo kuwa rahisi kwa vijidudu kuzaliana na kuharibu mazingira ya mdomoni kwako. Hivyo, ni afya zaidi kupiga mswaki usiku ili kuzuia kushamiri bakteria waharibifu wanaosababishwa na masalia ya bakteria kwenye kinywa chako. Njia hii itasaidia kuzuia bakteria kuharibu meno na fizi, hivyo kutokuwa na harufu mbaya ya masalia wakati ukiamka.

Kula ndizi au apple
Ndizi au apple husaidia kuondoa harufu mbaya kinywani, lakini ni kwa muda mfupi sana. Ukiwa unahisi mdomo unanuka na unahitaji njia ya haraka, tafuta ndizi au apple, na hapo utakuwa umetatua tatizo kwa muda.

Kula Tango
Maji ya tango yana kemikali zinazozuia kukua kwa bakteria kwenye kinywa. Baada ya mlo mzuri wenye viungo vyenye harufu kali, kata kipande kidogo cha tango, kigandishe kwenye ukuta wa juu wa mdomo wako kwa sekunde 30 huku ukikandamiza na ulimi. Zoezi hili litasaidia kuua bakteria na kuacha kinywa chako kikiwa na afya na harufu nzuri.

Jenga Tabia ya Kupia Mabusu (Kissing)
Ni ukweli kuwa ukifanya kitu chochote kinachosababisha kutoa mate basi unazuia kunuka kinywa. Kissing ni mojawapo ya njia mbadala za kuzuia harufu mbaya mdomoni. Kiss mara nyingi uwezavyo ili kufanya mdomo wako uwe na mate mengi, na hivyo kuzuia kunuka kinywa.

Harufu ikizidi, kamuone daktari
Je harufu yako ya kinywa ni ugonjwa? Basi kamuone daktari. Wakati mwengine harufu ya kinywa hutokana na kuwa na matatizo mwilini na huwezi kuondoa kwa kutumia njia tulizozieleza hapo juu.

1459682281132.jpg
 

Attachments

  • 1459682195701.jpg
    1459682195701.jpg
    6.9 KB · Views: 214
Asnte kwa ufafanuzi mzuri
Karibu mkuu,
Naona watu wengi kinywa wanakisahau sana,wakati kinywa kikiwa na harufu unaweza hata kunyimwa mahaba, kuna mwana jf mmoja leo asubuhi ameleta uzi akilalama mwenza wake mdomo unatoa harufu kali.
 
Karibu mkuu,
Naona watu wengi kinywa wanakisahau sana,wakati kinywa kikiwa na harufu unaweza hata kunyimwa mahaba, kuna mwana jf mmoja leo asubuhi ameleta uzi akilalama mwenza wake mdomo unatoa harufu kali.
Watakuja kuipitia, c unaona muda wenyewe sa ivi wako viwanja wanafurahia wkend
 
Usiogope kumwambia mwenza wako anatoa harufu kinywani na mpe njia bora hizi za kutunza kinywa...
 
Samahan sana doctor mm Nina tatizo LA kutoa harufu mdomon hata nikila chakul nisipo kula hari n ile ile naomba msaad wako n dawa gan nitumie niondokane na tatizo hili?
 
Wanaume mtatuua jaman chaaa!yaan kwani ulivyompenda alikuwa hanuki huo mdomo mpka ujisajili jamii forum kuja kuleta madhaifu yake huku?kwani huko ndo kuna hospital?
Kuna MTU nimemsaidia yeye alikuwa anaona aibu n Rafik yangu sana
 
Kuliondoa Tatizo hili waone madaktari wa kinywa na meno, ili wakague kama una jino lililooza ,na kulifanyia tiba
Sio wote wanaotoa harufu mdomoni ni kwa sababu ya kutokua na usafi sahihi wa kinywa
 
Kuna watu wananuka midomo jamani, nilikua nimekaa siti moja na mkaka hivi yaani mdomo wake unatoa hewa kama chemba za vyoo, kidogo nimuulize oyaa hupigagi mswaki.

Yaani alikua akipumua mpaka nageuza kichwa upande mwingine, nashukuru nimefika nakokwenda maana hali ilikua mbaya aisee.

Jamani tupigwe mswaki na kama una tatizo kamuone daktari wa meno uchunguze meno.

MAONI YA MDAU

Harufu mdomoni ni tatizo kubwa na linaleta changamoto kwenye utatuzi wake Kitaaalamu inaitwa HALITOSIS. Hili tatizo linaweza kuwa linachanzo mdomoni ama jino limetoboka hvyo kuwa kama hotpot na kuwa chanzo cha harufu mbaya ama matatizo ya fizi yaani plaque ama calculus ama ugaga ambao unaweka maambukizi ya bakteria na kudababisha harufu mbaya mdomoni ama upiga mbaya wa mswaki usiozingatia taratibu nzuri.

Chanzo kingine ni kwenye koo endapo kuna maambukizi kwenye njia za hewa nasopharynx ama kwenye mapafu. Vyooote hivyo huweza sababisha harufu mdomoni.

Jinsi ya kuepuka.

1. Kupiga mswaki kwa usahihi yaani sehemu zote za meno nje ndani na sehemu ya kutafunia kwenye ulimi mbele na nyuma chini ya ulimi ndani ya mdomo sehemu ya juu-palate Ili kuondoa ute mzito wenye harufu
2. Kupunguza vyakula vyenye sukari kwa wingi na vimiminika kupunguza mapishi yenye vitunguu kwa wingi..
3. Kufanya mazoezi ili kusafisha mfumo wa hewa na upumuaji
4. Kwenda kwa wataalamu wa afya ya kinywa na meno ili kupata tiba na ushauri bora wa jinsi ya kuepukana na tatizo hili

Kwa ufupi haya ni baadhi ya mambo yanayoweza kufanyika pindi unapohisi harufu mbaya mdomoni

Maledhi
 
Mmmhh inapendeza sana kila baada ya kipindi flani mtu ukachekiwe afya ya kinywa na meno. Kuna baadhi midomo inanuka kwa ugonjwa lkn wengine ni uchafu.

Mmhh kama unajijua unatatizo hili ni bora utafune hata bubblish zenye mint ili kupunguza harufu
 
Mtu ambaye hapati haja kubwa kama inavyotakiwa kitaalamu mara nyingi huwa na hili tatizo, akihema utafkiri panya kafia mdomoni hata apige mswaki mara mia kwa siku bado hali itakuwa hiyo hiyo.

Usiombe sasa ukutane na dada mwenye hilo tatizo.
Hahahahaha nmejikuta nacheka kwa nguvu utadhani mazuri
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom