Maoni yangu kuhusu gari aina ya Harrier maarufu "Tako la Nyani"

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,794
images (6).jpeg

Ni model ya gari ya Toyota Harrier kizazi cha vvt-i (umeme mwingi mafuta kidogo).

Huku kwetu tunaita new model lakini kimsingi sio new model kwa huko Japan.

Kwa kawaida Harrier ni gari zinazosifika kwa ulaji mbaya wa mafuta lakini model hii TAKO LA NYANI ni tofauti na model nyingine

Uundwaji wake umezingatia starehe zaidi, kasi, nguvu na ulaji mdogo wa mafuta. Hivi vigezo vimewavutia wa bongo wengi mpaka kuifanya ndio gari ya kuuzia sura kwa sasa yani ndio gari inayouza.

Huwezi kukaa dakika kumi mahali yanapopita magari bila kuiona hii gari mpaka sasa inaelekea kuwa kama sare ya taifa

Neno TAKO LA NYANI limetokana na hii gari taa zake za nyuma zilivyo.Yani zimekaa kama makalio ya nyani gendaeka yule mwenye makalio mekundu.
images (4).jpeg


Lakini ni wangapi wanajua hatari za hii gari gumzo la jiji? Kwa taarifa yako ndio gari zinazoongoza kwa ajali zikifuatiwa na Alphard.

Unaweza kudhani zina tatizo lakini shida ni sisi wenyewe. Hatujazoea gari zenye take over kubwa na mwendokasi wa fasta.

Hivyo ndugu zangu kama kuna mwenye mpango wa kununua hii gari azingatie haya wepesi, mwendokasi na nguvu ya hii gari

Jr
 
Mkuu, nimenunua hii kitu kwa mtu miezi sita iliyopita ikanishinda nikauza niliyemuuzia kapiga mzinga maeneo ya senkenke kwa mbele mwezi uliopita, nilipata mshituko sana nikahisi kama ilikuwa inanitafuta.
.....
Ila jamaa mzima
 
Ni model ya gari ya Toyota Harrier kizazi cha vvt-i (umeme mwingi mafuta kidogo)... Huku kwetu tunaita new model... Lakini kimsingi sio new model kwa huko Japan..
Kwa kawaida Harrier ni gari zinazosifika kwa ulaji mbaya wa mafuta lakini model hii TAKO LA NYANI ni tofauti na model nyingine
Uundwaji wake umezingatia starehe zaidi, kasi, nguvu na ualji mdogo wa mafuta... Hivi vigezo vimewavutia wa bongo wengi mpaka kuifanya ndio gari ya kuuzia sura kwa sasa yani ndio gari inayouza...
Huwezi kukaa dakika kumi mahali yanapopita magari bila kuiona hii gari mpaka sasa inaelekea kuwa Kama sare ya taifa
Neno TAKO LA NYANI limetokana na hii gari taa zake za nyuma zilivyo... Yani zimekaa kama makalio ya nyani gendaeka.. Yule mwenye makalio mekundu...
Lakini ni wangapi wanajua hatari za hii gari gumzo la jiji? Kwa taarifa yako ndio gari zinazoongoza kwa ajali zikifuatiwa na Alphard. Unaweza kudhani zina tatizo lakini shida ni sisi wenyewe... Hatujazoea gari zenye take over kubwa na mwendokasi wa fasta...
Hivyo ndugu zangu kama kuna mwenye mpango wa kununua hii gari azingatie haya... Wepesi, mwendokasi na nguvu ya hii gari

Jr
Nilichoelewa tu ni tako la nyani a.k.a tako jekundu...halafu linakuwaga limenona

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom