Harmorapa; Juma Nature hajanifanyia poa

brave one

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
4,879
7,382
Baada ya kusaidiwa kwenye nyimbo yake ya kiboko ya mabishoo na mkongwe Huyo, Harmorapa ameanza kumpiga vijembe juma nature




Harmorapa%252Bna%252Bnature.jpg


Msanii Harmorapa amewaomba wasanii wakubwa waliopo kwenye 'game' ya muziki kuacha tabia ya kuwapiga mkwanja mkubwa 'underground' wakati wanapoenda kuwaomba kufanya nao 'collabo'

Hayo yamekuja baada ya msanii huyo kuombwa pesa ya mavazi na Juma Nature kwaajili ya kufanyia ‘shooting video’ jambo ambalo kwa upande wake limemkwaza kwa namna moja ama nyingine.

“Haipo sawa kwa wasanii wakubwa kutudai sisi ‘underground’ pesa ya kufanyia collabo wakati wanajua bado hata hatuanza kufaidika na muziki wenyewe”. Alisema Harmorapa kwenye kipindi cha eNewz ya EATV.

Aidha Harmorapa amesema muda mwingine wasanii wakubwa wanatumia njia ya kutaka pesa ndefu ili mradi wa kwamishe kufanya kazi nao.

Kwa upande mwingine mzee wa kiki za mjini amesema mashairi aliyoyatumia katika wimbo wake amefanya kumjibu ‘dansa’ Mose Iyobo kutoka WCB kwa kile alichokifanya awali cha kumfananisha na sokwe.


Chanzo: eatv.tv
 
WCB acheni fitna, mmefungua IDs huko instagram zenye jina la harmorapa then mnaitumia kutukana wasanii wengine ili kumshusha Harmorapa-kiboko ya mabishoo.

Lakini mkumbuke mmeshindwa kabla hamjaanza
hahahaha! mkuu harmorapa kiboko ya nini vile???
 
hahahah huyu kijana hata simuelew aisee anajikuta star swaga zenyewe hana basi shida tu
 
ofcoz bado sijamuelewa vzuri lkn si ajabu akatoboa kiutani utani huyu jamaa
 
WCB acheni fitna, mmefungua IDs huko instagram zenye jina la harmorapa then mnaitumia kutukana wasanii wengine ili kumshusha Harmorapa-kiboko ya mabishoo.

Lakini mkumbuke mmeshindwa kabla hamjaanza
Acha kuleta ujuaji nenda kaangalie hata eatv wameipost wenyewe
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom