mzeemkavu
JF-Expert Member
- Dec 3, 2017
- 552
- 474
Dogo kawadhihirishia uwezo wake na kipaji alichotunukiwa na Mungu. Alikuwa lebo kubwa East Africa, WCB, na alifanya makubwa na hakuna mtu aliyetengemea kuwa anaweza kujitengemea mwenyewe alivyotangaza kuvunja mkataba na iliyokuwa lebo yake.
Wengi walimtabiria mabaya kwakuwa Rich Mavoko alianza kutoka kundini na kuangukia pua. Kondeboy kaonesha kipaji chake kikubwa baada ya kutoa nyimbo aliyoitoa chini ya lebo yake ya Kondeboy Worldwide. Uno ni best song now. Ni kama boss wake wa zamani (Diamond) baada ya kutoka kwenye mikono ya mtu na kufungua lebo yake (WCB) na kutoa wimbo wake wa Moyo Wangu. Ilikuwa kubwa sana hiyo ngoma.
Kondeboy kaonesha uwezo wake wa kuandaa show yake mwenyewe Bongo, kwenye uwanja wa mpira. Hiki kitu ni kikubwa sana kwani Wabongo tumezoea kuwaona wasanii wengi kwenye jukwaa moja. Konde kajiamini na kuandaa show yake mwenyewe na kujaza na bado anaandaa show ya Muleba na show ya Tandahimba, na zote zinatangazwa kama ya Shinyanga tu, jukwaani mwenyewe tu.
Haya ni mapinduzi ya muziki Tanzania. Harmonize anajitoa na kuonesha WCB hawakukosea kuwekeza kwake na pia WCB nao wanafarijika kuona kile walichokitengeneza kinavyofanya vyema East Africa na Africa pia kwa kizazi hiki.
Harmonize ni msanii wa kwanza kufanya show peke yake kwenye uwanja wa mpira na watu wakaitikia kwa wingi na show ikiwa ni ya kiingilio. Hapo ndo nilipojua Kondeboy ana kipaji, hakubebwa na lebo kama wengine.
Kwa leo naishia hapo.
Sent using Jamii Forums mobile app