Harmonize na Rich Mavoko wadaiwa kuiba wimbo wa ‘Show Me’

KWEZISHO

JF-Expert Member
Jan 29, 2016
7,519
6,517
‘Show Me’ ya Harmonize na Rich Mavoko ni moja kati ya nyimbo ambazo zinafanya vizuri katika sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi, katika kipindi kifupi tangu itoke.

Imedaiwa kuwa, wimbo huo umeibiwa kutoka kwa msanii wa Bongo ambaye anaishi Uingereza ajulikanaye kama PCK. Akiongea na kipindi cha Dj Show cha Radio One, msanii huyo amethibitisha kuibiwa wimbo wake huo, huku akimtaja Ray C kuwa ndio shahidi ambaye alikuwepo siku anairekodi.

“Kabla sijasafiri kuja UK nilienda WCB nikaonana na Laizer, walinicharge hela ya kurekodi pale, shilingi laki tano na nililipa ile pesa tukarekodi. Siku ambayo nilikuwa narekodi Ray C alikuwepo, nilipomaliza nikapewa tarehe ya kuja kuchukuwa nyimbo lakini siku ilipofika nikaanza kupigwa kalenda. Baadae nikaja kuambiwa imecollapse kwahiyo natakiwa kurekodi upya,” amesema msanii huyo.

“Kwenye process ya kurekodi upya nikawa napigwa chenga chenga. Nikawa nimesafiri, ilipofika majuzi kati hapo Ray C aliniambia hebu ingia Instagram ya Harmonize kuna nyimbo ameipost lakini nikisikia beat na melody ni kama ile nyimbo uliyokuwa unarekodi siku ile tulipokuwa studio,” ameongeza.

PCK amesisitiza kwa kusema, “Cha kunishangaza hakubadilisha neno hata moja. Beat ni ile ile na maneno ni, yale yale. Kinachoniuma, nashangaa mtu akilalamika mtu kaibiwa nyimbo yake, kisa tu ni mtu wa WCB kaifanya, unaambiwa unatafuta kiki, hapana.

Siwezi kutafuta kiki kwa mtoto mdogo kama Harmonize, ambaye nina uwezo wa kumlisha miaka nenda rudi nikamuhudumia kila kitu. Nina mawakili wangu ambaowapo Tanzaniawanalifuatilia na
ninafikiri next week hilo swala litafikishwa mahakamani.”


Chanzo: The Choice


My take:
Kama ni kweli, hilo litakuwa funzo kwa wanataka kufaidi kazi za watu pasi kuumiza kichwa!
 
Kama ni kweli now watakuwa wamepress the wrong button.

Lakini ana interectual property ya song lake??
Ana hati milik?
 
Hata beat sample ni wimbo wa 2face unaitwa see me,mtu anae zijua hizi nyimbo atakubaliana na mimi kuwa huyo Laizer na wenzie wamefanya kukopi beat skeleton ya wimbo wa 2baba-See me.
 
Hawa madogo naona wanataka kupoteza umaarufu kama vijana wa bongo muvi
 
wizi mtupu...nini kinasababisha wasanii wa TANZANIA KUKOSA UBUNIFU wa kazi zao?
 
Hata boss wao ..mbagara.nataka kulewa.number one zote wizi mtupu...KCP wafundishe adabu
 
![/QUOTE]
labda kidogo aseme beat inawezekana siwawekei dhamana ila kwa mistarii hii ni ya wcb

au wazee wa kununua.....akina sallam
nyuma ka katoon za masoud...............
saa sita shape vera sidika..........
mmakonde na ndonya...........
kama mpila maradon kichuya kona.......
na wakisema na mawenge waambie werason.....
wakilingisha peremende nitakugawia koni......

hii ni mistari tu imekaa ki wcb, ndo wanaimba kujazia vina bila kuangalia ujumbe na huku wakitupia vimatusi vya mafumbo kidogo
 
Je, kabla hajautoa alishauwekea hatimiliki? Kama ndivyo sivyo, asijisumbue kupoteza fedha zake bure.
 
labda kidogo aseme beat inawezekana siwawekei dhamana ila kwa mistarii hii ni ya wcb

au wazee wa kununua.....akina sallam
nyuma ka katoon za masoud...............
saa sita shape vera sidika..........
mmakonde na ndonya...........
kama mpila maradon kichuya kona.......
na wakisema na mawenge waambie werason.....
wakilingisha peremende nitakugawia koni......

hii ni mistari tu imekaa ki wcb, ndo wanaimba kujazia vina bila kuangalia ujumbe na huku wakitupia vimatusi vya mafumbo kidogo[/QUOTE]
Jamaa aliweka adi sample ya wimbo anaodai umeibiwa yaani ukiusikiliza na kifo na usingiz tofauti kabisa
 
Back
Top Bottom