Hard Blasters crew" H.B.C " - Tuko nyuma

Hard Blasters crew" H.B.C " - Tuko nyuma

NGAYANIMO

Member
Joined
Feb 17, 2026
Posts
36
Reaction score
55
1772402640884.jpg
HARD BLASTERS CREW FT. LB GENIUS
( TUKO NYUMA)

Chorus.

Tuko nyuma kimaendeleo
Sababu ya Rushwa , ubadhilifu na upendeleo

Tuko nyuma

Tuko nyuma Tu na kichocheo
Mambo ni ovyo hatuna Dira wala muelekeo...

Chorus.

Tuko nyuma kimaendeleo
Sababu ya Rushwa , ubadhilifu na upendeleo

Tuko nyuma

Tuko nyuma Tu na kichocheo
Mambo ni ovyo hatuna Dira wala muelekeo...

VERSE..1 ( FANANI )

Tuko nyuma tumechoka hohehae/
Wa Bongo wa leo tulipotoka natamani niwe kipepeo /
Maisha ya shoka ili kushinda yataka upeo/
Ni ma nyoka ma nyoka na twasubiri ni matokeo/
Sijui nchi imeuzwa hatuna dira wala muelekeo/
Tunapuuzwa wazalendo hatuna maendeleo/
Tuna nyanyaswa na wenye vyeo/ wanajifanya madondi malipo ya kodi wananywea vileo/
Lini tutafika usawa huu mwapiga kumeo/
Saa tatu taya mbili za koromeo /
Kweli tuko nyuma bila rushwa hakuna huduma/
Pesa mbele hakuna usawa wala huruma/
Yaani ubaya ubaya kama hauna sogea nyuma/
Kunja ndita kinoma noma rushwa ya chuma/
Kaa mwasibu aone Aibu kula cha Umma/
Haoni hatari kuwa na hekaluu la kifahari/
Yenye ana twaga ana pepeta hana habari/
Ni kazi kwetu walala hoi tusiokuwa na hali/
Kwani macho upima tangu kitambo watu ni chali/
Hatuna makali ya kufanya uzushi kulamba Asali/
Kumbuka wa Bongo pata maono ona kwa mbali/
Na hii ni Bongo nchi safi kwa wenye mali/
Bado na matongotongo mikono juu tumekubari/
Huu sio uongo hapa nchini ni kama Ajali/
Aah natia huruma wa tanganyika roho inauma/
Tuko nyuma kimaendeleo
Sababu ya Rushwa, ubadhilifu na upendeleo /
Tuko nyuma
Tuko nyuma..

Chorus.

Tuko nyuma kimaendeleo
Sababu ya Rushwa , ubadhilifu na upendeleo

Tuko nyuma

Tuko nyuma Tu na kichocheo
Mambo ni ovyo hatuna Dira wala muelekeo...

Chorus.

Tuko nyuma kimaendeleo
Sababu ya Rushwa , ubadhilifu na upendeleo

Tuko nyuma

Tuko nyuma Tu na kichocheo
Mambo ni ovyo hatuna Dira wala muelekeo...



LB GENIUS ' HARB BLASTERS CREW - TUKO NYUMA

Hapa tulipo wabongo tupo nyakanyaka/
Nyakanyaka...!!
Na bado tunapelekwa mchakamchaka/
Kila kona ni Rhumba kali wabongo hatuna hali/
" LB GENIUS" nawaza mbali kudada meli/
shika mtutu Vunja maduka night kali/
Night kali..!!
Tunapotoka ni mbali na bado tunasaga Lami/
Ndani ya jua kali/
Tulowapa madaraka sasa wanaponda mali/
Matatizo kibao na bado hawatujali/
Jali...!!
Kila mtu anapenda kuwa na mali/
Sisi kwa wadosi bado hatuna nafasi/
Ipo siku tutachoka tutapigana Risasi/
Risasi..!!
Madeiwaka hatuna pesa na bado mapolisi wanatutesa/
Kwenye mitaa ni zeke zeke na karaha/
Karaha..!!
Maajabu na machokoraha/
Watanganyika tupo ndani ya nyika/
Tunapokwenda ni lini tutafika sisi watanganyika/
Tuko nyuma toka siku za nyuma mpaka leo/
Mpaka leo..!!
Wabongo kwa wadosi bado ni vibaraka Hatuna vyeo/
Huu ni ukoloni mambo leo/
Tunapelekwa kama picha za video/
Maofisini hatuna Raha kila siku ridadasi/
Vyeo wanapeana wao kwa wao/
Na kabla ya kifo chako hupati mafao/
"LB " napandisha mzuka wa mizuba/
Wazawa tumechoka Bongo hatuna penzi la huba/
Kila siku ni dhuruba/
Kilichobaki tusari Sala za Toba/
Aaah..!!
Tupo nyuma kimaendeleo Sababu ya Rushwa ubadhilifu na upendeleo Tuko nyuma/
Aaah

Ukwaju wa kitambo
0767 542 202

( katika picha ni marehemu Lb genius)

 
View attachment 3550822HARD BLASTERS CREW FT. LB GENIUS
( TUKO NYUMA)

Chorus.


Tuko nyuma Tu na kichocheo

Tuko nyuma Tu na kichocheo

Tuko nyuma Tu na kichocheo
Kwa haraka haraka, nimeona nirekebishe hapo,

'Tuko nyuma hatuna kichocheo'

Jamaa walikuwa conscious sana, big up kwao 🙌🏽🙌🏽
GOD bless the dead
 
Inasikitisha sana M.A.P LB GENIUS ,2000 nilinunua Album ya H.B.C Funga kazi ,kumbe jamaa alishafariki sikujua.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom