Haramu ya Lowasa siyo halali ya Magufuri

Mbase1970

JF-Expert Member
Jun 11, 2015
6,054
4,601
Lowassa.jpg

Mwandishi Luqman Maloto

Kumbukumbu ya nusu muongo uliopita ni kuharibiwa kwa mchakato wa Katiba Mpya katika hatua ya Bunge Maalum la Katiba. Chama Cha Mapinduzi (CCM) na vyama vya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kwa pamoja wanastahili lawama.
Bunge Maalum la Katiba, lililoongozwa na aliyekuwa mwenyekiti wake, hayati Samuel Sitta, ndilo ambalo lilisababisha Rais wa Awamu ya Nne, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Jakaya Kikwete, aondoke madarakani pasipo kupatikana kwa Katiba Mpya.
Hali hiyo, imekuwa kinyume na ahadi ya Rais Kikwete ambaye katika hotuba yake ya kuzindua Bunge la 10 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Novemba 2010, aliahidi kuwa muhula wake wa pili, 2010-2015, ungekuwa wa kupatikana kwa Katiba Mpya ya Watanzania.
Sababu kuu ya kutopatikana kwa Katiba Mpya ni Ukawa kugoma na kususia vikao vya Bunge la Katiba, kisha waliosalia bungeni, wengi wao wakiwa CCM, walipuuza umuhimu wa maridhiano.
Bunge Maalum la Katiba mwaka 2014, lilipitisha Katiba Inayopendekezwa. Hata hivyo, imekuwa vigumu kuruhusu mchakato wa kuipigia kura ya maoni, ama ipitishwe au ikataliwe, kutokana na kile kinachoonekana ni aibu kutokana na mazingira yaliyojitokeza bungeni.
Kimsingi, Katiba Inayopendekezwa ilipoteza uhalali mapema kabisa. Kitendo cha wajumbe zaidi ya theluthi moja kususia vikao vya Bunge la Katiba, kilijenga picha kuwa Katiba haiwezi kuwa ya wananchi.
Sababu nambari mbili ni kiburi cha wajumbe waliobakia bungeni. Kitendo cha wao kuamini kuwa wangeweza kuketi na kupitisha Katiba Inayopendekezwa pasipo maridhiano na waliosusa, kilikuwa hakijengi.
Katiba ya wananchi sharti iwe na maridhiano. Kwa maana kwamba Katiba ni vizuri iwe na sura yenye kukubalika na jamii kwa upana wake. Wengi wanaposusa, maana yake hiyo siyo Katiba ya wananchi bali ni Katiba ya kikundi fulani.
Makosa ya Ukawa kwenye Katiba
Bunge la Katiba mwaka 2014 lilithibitisha kuwa wapinzani Tanzania ni waoga, wanadeka na dhaifu ukilinganisha na wenzao wa Kenya. Wakati Ukawa wanasusa Bunge la Katiba, ilikuwa imepita miaka tisa tangu wapinzani Kenya walivyoikataa Katiba iliyokuwa chapuo la watawala.
Mwaka 2005 Kenya walipokuwa wanataka kufanya mabadiliko ya Katiba yao, mchakato uliendeshwa mpaka Bunge la Katiba liliketi. Ndani ya Bunge, sauti ya wajumbe wengi walikuwa upande wa maoni yenye kubeba fikra za aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, Mwai Kibaki na timu yake.
Kiongozi wa chama cha ODM, Raila Odinga, aliongoza timu ya watu ambao waliikataa katiba hiyo. Akina Raila pamoja na uchache wao hawakususa Bunge la Katiba, walibaki ndani yake, walipambana mpaka mwisho.
Kura za wajumbe wa Bunge la Katiba zilipopigwa, akina Raila walishindwa kutokana na uchache wao. Katiba inayopendekezwa kwa Wakenya ikawekwa hadharani, ikatangazwa tarehe ya kura ya maoni.
Raila na wenzake baada ya kushindwa bungeni, walijielekeza katika kuelimisha umma kuhusu ubaya wa Katiba iliyokuwa inapendekezwa. Matokeo ya kura ya maoni iliyofanyika Novemba 21, 2005, sauti za akina Raila zilisikika na wananchi wa Kenya kwa asilimia 58 waliikataa Katiba hiyo.
Wakati huo Kibaki, wabunge wengi na Serikali kwa upana wake walisimama imara kufanya kamapeni wakiwataka wananchi kupiga kura ya “ndiyo”, lakini matokeo yakawa, waliochagua “hapana” walishinda.
Ukawa walipaswa kuonesha ukomavu wa aina hii, kushindana kwa hoja bila kukata tamaa. Mnazidiwa nguvu bungeni kisha mnahamia mtaani kuelimisha wananchi waikatae Katiba Inayopendekezwa. Wao suluhu ikawa kususa vikao vya bunge.
Hali hiyo ndiyo ambayo hufanya wapinzani wa Tanzania waonekane sawa na mtoto anayedeka kwa mama au baba yake wa kambo. Je, ni matarajio kweli mzazi wa kambo anaweza kumdekesha mtoto ambaye si wake? Hutokea wawili kati ya elfu.
Upinzani na chama tawala lazima kuwe na msuguano wa kimawazo, hoja kwa hoja, mikakati kwa mikakati. Lile ambalo chama tawala wataona linawafaa kwa mbinu zao za kubaki madarakani watalitumia tu. Wapinzani wa Tanzania hutaka CCM yenyewe ilegeze kamba kisha wao washinde dola kwa urahisi kabisa.
Mtoto wa kambo huwa hasusi chakula, maana akifanya hivyo ataambulia mkong’oto kisha atashinda au atalala na njaa. Wapinzani wanatakiwa kujielimisha kuwa kuwasusia CCM ni sawa na kuridhia wafanye mambo yao bila bughudha. Wanashika tu ule msemo; ukisusa wenzio tunakula.
Tujadili haramu ya Lowassa
Humphrey-Polepole-300x200.jpg

2015 ni mwaka wenye historia ya mapambano makali ya kisiasa kwa Waziri Mkuu wa kwanza katika Serikali ya Awamu ya Nne, Edward Lowassa. Alipambana mno kuingia Ikulu, uongozi uliokuwepo wa CCM ulihakikisha ndoto hiyo Lowassa hatimizi.
Dk Kikwete alicheza mpira mgumu kumdhibiti Lowassa. Yeye na wenzake walimkata jina miongoni mwa waliokuwa wanawania nafasi ya kupeperusha bendera ya chama kama mgombea urais, kisha wakaenda kupambana naye alipohamia Chadema na Ukawa.
Lowassa baada ya kujiunga na Chadema kisha kupata baraka za vyama vya Ukawa, ndipo uharamu wake kuhusu kuharibika kwa mchakato wa Katiba Mpya ulipoelezwa. Mshereheshaji wa hoja hiyo, alikuwa aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Humphrey Polepole.
Wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu 2015, Polepole alijiweka wazi kumpinga Lowassa. Hoja kubwa ambayo aliitumia ni kuwa Lowassa na genge lake ni sababu ya Rasimu ya Katiba kama ilivyoandikwa na wao kwenye tume, kuvunjwavunjwa na kutolewa maoni tofauti kabisa.
Polepole alisema kuwa sababu iliyofanya Lowassa na watu wake waipinge Rasimu ya Katiba, maarufu zaidi kama Katiba ya Warioba ni hoja ya Serikali Tatu. Kwamba Lowassa alikuwa ameshajiandaa kuongoza nchi, kwa hiyo aliona Serikali Tatu zisingempa nafasi nzuri ya kuwa Mkuu wa Serikali, Mkuu wa Nchi na Amiri Jeshi Mkuu kwa wakati mmoja.
Alichokisema Polepole ni kuwa Lowassa na watu wake waliipinga Rasimu ya Katiba kwa sababu za uchu wa madaraka. Kwamba walitaka awe na mamlaka yote na sivyo kama ambavyo yalikuwa yamegawanywa kupitia Rasimu ya Katiba ya Warioba.
Kwa mujibu wa Polepole, Watanzania hawakutakiwa kumchagua Lowassa kwa sababu aliwaharibia mchakato wao wa kupata Katiba Mpya na bora. Pamoja na kasoro nyingine ambazo Polepole alizieleza kumhusu Lowassa, shambulio kubwa lilihusu Katiba.
Kabla ya Lowassa kukatwa jina CCM kisha kujiunga Chadema na Ukawa, Polepole katika harakati zake za kusambaza uenezi wa namna mchakato wa Katiba Mpya ulivyovurugwa, aliwahi kutamka: “Kama uchaguzi utakuwa huru na haki, CCM ijiandae kukabidhi nchi kwa wapinzani.”
Lowassa alipohamia Chadema, Polepole akarejea kuitetea CCM (chama chake) kwa nguvu kubwa na aliyekuwa mgombea wake wa urais, Dk John Magufuli. Tamko lake kuwa CCM ijiandae kukabidhi nchi kwa wapinzani akalisahau.
Tuione hali ya Magufuli
Ufafanuzi wa Polepole ni kuwa Lowassa kupitia mtandao wake, aliathiri Rasimu ya Katiba kwa sababu ya kupinga mgawanyo wa madaraka kupitia muundo wa Serikali Tatu. Eneo la Serikali Tatu ni sehemu tu ya Rasimu ya Katiba.
Novemba 4, mwaka huu, Rais Magufuli alipokuwa anazungumza na wahariri wa vyombo vya habari nchini, alisema wazi kuwa Katiba siyo kipaumbele chake, akasema aachwe kwanza ainyooshe nchi.
Je, unaweza kumlaumu Lowassa aliyeathiri Katiba kwa sababu kipengele cha Serikali Tatu kisha kumkubali Rais Magufuli ambaye hata mambo yenyewe ya Katiba hataki kuyasikia?
Kwa sasa Polepole ni Katibu wa Halmashauri Kuu (Nec) ya CCM, Itikadi na Uenezi, mwenyekiti wake ni Rais Magufuli. Kwa Polepole anaona sawa kufanya kazi na mtu ambaye hataki kusikia mambo ya Katiba Mpya, wakati huo aliyeathiri kipengele kimoja tu cha Serikali Tatu kwenye Katiba alimuona ni hatari kwa nchi.
Je, Polepole anaingia kufanya kazi na kiongozi kwenye chama ambaye anapishana naye mtazamo kuhusu suala la Katiba? Maana alihubiri kuwa Katiba Mpya ni muhimu kwa sasa, Magufuli ametamka kuwa kwake Katiba si kipaumbele chake.
Kwa hali hiyo, ni rahisi kupata jawabu kuwa msimamo wa Polepole na mashambulizi yake kwa Lowassa kuhusu Katiba zilikuwa tofauti tu za kisiasa na siyo maslahi ya kikatiba kama alivyokuwa anajenga hoja. Maana kama ingekuwa hivyo, basi kwake Rais Magufuli angempinga zaidi.

Luqman Maloto
 
Makosa ya Ukawa kwenye Katiba
Bunge la Katiba mwaka 2014 lilithibitisha kuwa wapinzani Tanzania ni waoga, wanadeka na dhaifu ukilinganisha na wenzao wa Kenya. Wakati Ukawa wanasusa Bunge la Katiba, ilikuwa imepita miaka tisa tangu wapinzani Kenya walivyoikataa Katiba iliyokuwa chapuo la watawala.
Mwaka 2005 Kenya walipokuwa wanataka kufanya mabadiliko ya Katiba yao, mchakato uliendeshwa mpaka Bunge la Katiba liliketi. Ndani ya Bunge, sauti ya wajumbe wengi walikuwa upande wa maoni yenye kubeba fikra za aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, Mwai Kibaki na timu yake.
Kiongozi wa chama cha ODM, Raila Odinga, aliongoza timu ya watu ambao waliikataa katiba hiyo. Akina Raila pamoja na uchache wao hawakususa Bunge la Katiba, walibaki ndani yake, walipambana mpaka mwisho.
Kura za wajumbe wa Bunge la Katiba zilipopigwa, akina Raila walishindwa kutokana na uchache wao. Katiba inayopendekezwa kwa Wakenya ikawekwa hadharani, ikatangazwa tarehe ya kura ya maoni.
Raila na wenzake baada ya kushindwa bungeni, walijielekeza katika kuelimisha umma kuhusu ubaya wa Katiba iliyokuwa inapendekezwa. Matokeo ya kura ya maoni iliyofanyika Novemba 21, 2005, sauti za akina Raila zilisikika na wananchi wa Kenya kwa asilimia 58 waliikataa Katiba hiyo.
Wakati huo Kibaki, wabunge wengi na Serikali kwa upana wake walisimama imara kufanya kamapeni wakiwataka wananchi kupiga kura ya “ndiyo”, lakini matokeo yakawa, waliochagua “hapana” walishinda.
Ukawa walipaswa kuonesha ukomavu wa aina hii, kushindana kwa hoja bila kukata tamaa. Mnazidiwa nguvu bungeni kisha mnahamia mtaani kuelimisha wananchi waikatae Katiba Inayopendekezwa. Wao suluhu ikawa kususa vikao vya bunge.

Luqman Maloto
Pamoja na hoja yako nzuri umesahau kuwa kura ya maoni juu ya katiba ya Tanzania ingeendeshwa na Tume ya uchaguzi ambayo si huru maana inateuliwa na huyo ambaye katiba ililenga kumpunguzia madaraka. Kwa vyovyote vile kulikuwa na uwezekano mkubwa hata matokeo ya kura ya maoni kuchakachukliwa, na hicho ndicho wapinzani walikiona wakaona afadhali wajitoe mapema wasije kuonekana walikuwa sehemu ya katiba mbovu.
Utakumbuka kuwa katika sheria ya kwanza ya kura ya maoni, ilikuwa tume ya katiba (ile ya Warioba) ndiyo iendeshe kuara ya maoni lakini kwa sababu waliokuwa na dola waliona itakuwa tishio kwao maana watasema ukweli wa matokeo (kama walivyokuwa wameandika ukweli kwenye rasimu), sheria ilibadilishwa ghafla na kuweka tume ya uchaguzi iendeshe kura ya maoni, Ni ghiliba hii ambayo wapinzani waliikataa,
Kenya ni tofauti, ile tume iliyosimamia kura ya maoni ilikuwa huru.
 
Kama shida ni tume, kwa nini hawasusii uchaguzi?
 
Ukweli ni kuwa Ukawa waondoe kabisa deko. Wajitolee kupigania haki za binadamu. Bila kujali wengine wanasema nini.
Ona madaktari Kenya watu wanakufa lakini mgomo unaendelea. Wakati mwingine ni bora kujitolea ili taifa lidumu na democrasia.
 
Back
Top Bottom