Harambee ya Lowassa yazoa milioni 400 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Harambee ya Lowassa yazoa milioni 400

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mizambwa, Jun 8, 2012.

 1. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #1
  Jun 8, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  Harambee ya Lowassa yazoa milioni 400

  Thursday, 07 June 2012 19:46


  James Magai

  WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu wadhifa huo Edward Lowassa amechangisha kiasi cha Sh.400milioni kutoka kwa wadau mbalimbali wa Maendeleo ya Elimu kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya Elimu katika Kata ya Kipawa jijini Dar es Salaam.

  Lowassa ambaye pia ni mbunge wa Monduli aliwezesha kuchangwa kwa kiasi hicho cha pesa wakati wa harambee iliyoandaliwa na diwani wa Kata ya Kipawa Bonnah Kaluwa iliyofanyika juzi usiku Dar es Salaam, ambapo yeye alikuwa mgeni rasmi.

  Kabla ya kuendesha haramabee hiyo Lowassa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ulinzi na Usalama alisema kuwa kuchangia uboreshaji wa elimu nchini ni jambo la heshima na linawezekana kuondoa changamoto zinazozikabili shule mbalimbali.

  Lowassa alisema mjini ambako maisha ni nafuu kulinganisha vijijini shule zinakabiliwa na matatizo makubwa ya miundombinu, kwa vijijini shule nyingi ziko katika hali mbya zaidi.

  "Kila kata sekondari zilizoanzishwa na serikali baadhi hazina vyumba vya madarasa vya kutosha, maabara wala nyumba za walimu. Watanzania tukiamua na tukiongozwa vizuri tunaweza kuzichangia' alisema.

  Aliongeza kuwa Wakuu wa Mikoa, Wakurugenzi wa Manispaa, Maofisa Elimu wa mikoa wanaweza kufanya haya, na kwamba Kipawa wameonesha njia.

  "Tuhimizane kwa hili. Madiwani na wabunge wote Tanzania tuige hili," alisisitiza Lowassa.Awali Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Slaa alisema ili kukabiliana na matatizo ya miundombinu katika Manispaa hiyo iliyomo kata ya Kipawa zinahitajika zaidi ya Sh.300bilioni.
  Meya Slaa ambaye Manispaa yake ilichangia Sh.10milioni, alitoa wito kwa serikali kuangalia namna ya kugharimia elimu nchini.

  Katika harambee hiyo Lowassa alichangia kiasi cha Sh.10miloni huku Benki ya Uwekezaji (TIB) ikivunja rekodi kwa kuchangia madawati 50 yenye thamani ya zaidi ya Sh.300milioni, wakati kampuni ya Maersk Sealine ilichangia Sh.90milioni ikifuatiwa na Lions Club iliyochangia Sh.70milioni.

  Baadhi ya makampuni mengine na watu binafsi waliochangia katika harambee hiyo ni pamoja na Home Shopping Centre iliyochangia Sh.22milioni, mfanyabiashara Yusufu Manji Sh.15milioni, aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini kabla ya kuondolewa katika wadhifa huo hivi karibuni William Ngeleja Sh.10milioni.

  Pia Chama cha Mapinduzi (CCM) kilichangia Sh.20milioni sawa na kampuni ya Simon Group, wakati Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) kikichangia Sh.10milioni huku kampuni ya madini ya Barrick Gold Mine ilichangia dola za Marekeni 10,000.

  Akitoa shukrani mbunge wa jimbo la Segerea ambapo imo kata ya Kipawa ambaye pia Naibu Waziri Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana Dk. Milton Makongoro alisema mbali na michango hiyo kuna watu wengine ambao wamechukua fomu za kuchangia ambazo bado wanaendelea kuzikusanya.

  Source: Gazeti Mwananchi - 08/06/2012
  ...................................................................................................
   
 2. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #2
  Jun 8, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  Binafsi sina budi kumpongeza Mh. Lowasa na wote walioshiriki katika kuchangia maendeleo ya Jamii.

  Na viongozi wengine waige mfano huu, na siyo kuleta mambo ya kisiasa kila sehemu hadi katika majumba ya ibada.

  Kwa hapa nampongeza.  MIZAMBWA
  NABII MTARAJIWA!!!
   
Loading...