Harambee Stars vs Taifa Stars official thread

bulletface

JF-Expert Member
Jul 14, 2017
287
250
Afcon 2019 most anticipated game ni Kati ya watani wa jadi Kenya na Tanzania. Je ni Nani atambwaga mwenziwe chini?

Leo haki ya Nani Harambee ikitwanga Taifa Stars, hakuna lolote Mtzee atawahi niambia joto la jiwe , MOTOCHINI mkorinto REDEEMER. Geza Ulole game over ichoboy01 tuusan
Watz yanayotuponza ni Mengi mno, kwa mtazamo wangu binafsi moja ni lishe duni ya wachezaji wetu uwanjani wanapwaya sana, pili ni mfumo mbovu wa upatikanaji wa wachezaji wa timu ya taifa, tatu ni tatizo la lugha au communication barrier kati ya wachezaji na kocha inawezekana wanashindwa kumwelewa kocha, nne watz tunapenda maisha ya short cut mno hatupendi kuhumiza kichwa tunapenda sana kubebana na kubebwa bebwa , tano watz tunahamini sana ushirikina yaani kila jambo tunataka kumshirikisha mganga wa jadi mpaka mpira tunatumia miti shamba wakati mpira ni hesabu tu, ndio maana raisi wa dar kaomba kwenda misri apeleke dawa zake ili tushinde, mambo mengine ambayo ni kama minor issues kwangu ni pamoja na ufisadi kuanzia kwenye vilabu vyetu mpaka TFF, wizara n.k, nyingine ni ufinyu wa budget japo hii sio sababu ya msingi kwani nchi kama Zimbabwe wana njaa lakin wanafanya vizuri au nchi kama Burundi utasema wanabudget kutuzidi? Hii nimeiongezea kwa kigezo cha wizara kushindwa kutenga budget I ya kushiriki mashindano ya AFCON wakati inayo calendar ya FIFA ya mwaka mzima huu ni uzembe mkubwa sana alafu tunakuja kuchangishana hapa. Hebu fikiria timu zitakazo fuzu mpaka mwisho zitaingizia fedha kiasi gani nchi zao.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom