MIXOLOGIST
JF-Expert Member
- Mar 1, 2016
- 14,727
- 37,030
Wahenga wanasema JITIHADA HAZIZIDI KUDRA YA MWENYE-ENZI MUNGU
Sawa kwanini sasa anataka nimuombe ? Kwani yeye hajui mimi nachostahili kukipata?Madam, kwanza sijui unaelewa nini khs riziki?
Riziki ni jumla ya neema ambazo Allan anatupa, hata mvua nayo ni riziki, pigia mstari hapo, hata hela au kipato nayo ni riziki.
Sasa kwa taarifa yako,lau Allah angempa kila mtu riziki anayotaka basi tambua watu wangejawa na kiburi Sana na huenda pasingekalika kabisa, ebu angalia mfano tu wa watu wachache walio fanikiwa kimaisha, naamini baadhi umeshawahi kuona vituko na dharau zao,je ingekuwaje kama watu wote tungekuwa nazo?
Aliyetuumba anatujua vzr Sana kuliko ss tunavyojijua, anafanya kila jambo kwa hekima zake, natumaini walau kidogo umepata mwanga
MadamSawa kwanini sasa anataka nimuombe ? Kwani yeye hajui mimi nachostahili kukipata?
Sawa sawaMadam
Anajua unachostahili kukipata ndio maana hutupa riziki kwa wakati sahihi, mfano huenda ww au mm tukataka kipato kizur kwasasa lkn huenda ndio ikawa maangamizi yetu,kwanini nasema hivyo? mathalan mm ni mwanaume huenda nikiwa na kipato cha kutosha kwasasa huenda nikabobea ktk anasa na atimaye nikapata ya kuyapata, kuepushwa na hayo nitapunguziwa riziki na kupata mahitaji muhimu tu.
Lkn huenda huko baadae baada ya kuwa nimekomaa kifikra na kuwa na maamuzi sahihi nikazidishiwa zaidi.
Kwanini tunamuomba Mungu?
Ni kuonyesha sisi ni wahitaji na katu hatumiliki chichote kwani hakika yote tuyapatayo ni kwa neema zake.
Na
Allah atawaadhibu watu ambao wamepinga ibada yake ya kuomba kwasababu wanajifanya wana kiburi mbele ya mola wao