Happy Women's Day

Mema Tanzania

Verified Member
Feb 23, 2020
48
125
Happy Women's Day

Mema Tanzania inawatakia kila la kheri katika siku hii ya mwanamke duniani. Siku hii iwe ni yenye tija, ufanisi, uwajibikaji, utendaji na kuweza kuwa chachu ya maendeleo kwa mwanamke, jamii na taifa endelevu.

Yafaa itumike kwa yaliyokuwa chanya na bora kwa kizazi cha sasa na kijacho, utumie siku hii kufanya mapinduzi yatakayoiwezesha jamii kuwa bora na yenye nguvu madhubuti katika ukuaji wa nyanja mbalimbali kuanzia elimu, teknolojia, sayansi, sanaa, siasa, uchumi, familia, jamii na dunia kwa ujumla.

Utumie siku hii kukamilisha mipango uliyojiwekea, tengeneza nia taadhia na kusambaza upendo pia. Tengeneza mikakati na mifumo imara ya fikra endelevu kuweza kuitengeneza kesho isiyokuwa na kadhia.

Siku hii ikufanye kuwa daraja kwa wengine, kichocheo kwa ustawi, maarifa na taifa. Iangaze dunia kuwa yenye nuru na tabasamu kwa upendo imara.

Heri ya Siku ya Mwanamke Duniani!

IWD DAY.png
 
Top Bottom