Happy Holidays 2008-09...

kazi nzuri mzee,kweli na wewe uko kwenye maandalizi mana sasa hata mjini foleni zimesha anza pungua watu kujiandaa na sikukuu
 
....kuna angalizo limetolewa ni muhimu kulitekeleza. Kwamba kuepuka ubaguzi ni vizuri na Sikukuu za Eid, JF ibadilishe muonekano kama ilivyokuwa sasa.
Mkuu, siku ya Eid kulikuwa na mabadiliko japo tulichelewa kujiandaa. Kwa wenye kumbukumbu nilishtuka na kuuliza "Eid ni lini" angalia hapa:

Swali nililiuliza hapa:

https://www.jamiiforums.com/333898-post2.html (just click and see what I wrote)

Na kuhusiana na sikukuu za kiislam rejea maeneo haya:

https://www.jamiiforums.com/295143-post35.html (just click and see what I wrote)

https://www.jamiiforums.com/336530-post43.html (just click and see what I wrote)

Na wala haikuchukua muda baada ya kuwepo changes kwenye logo ya JF kuaanzishwa topic hii:

A question to the jamiiForums administration (Isome uone nilijibu nini)

Kumradhi kwa wanaokuwa offended.
 

Kwa mawazo yangu ninafikiri ni katika kusheherekea sikukuu ya Iddi.




Wakuu, kabla ya X-mas huwa kuna sikukuu ya Kiislam. Sijaijua ni tarehe ngapi (hata kwa kukadiria) lakini kuna kitu nilihitaji tukifanye kuanzia sasa. Can anyone gimme a clue?

8th Dec Eid el Hajj

Lakini depending on the sighting of the moon mzee.

MJ

Ahsante, nilichotaka tufanye kinaanza mara moja. Ahsante sana mkuu

Eid Mubarak!

عـــيــد مــبـــارك

Invisible

Nadhani kwa kuyanukuu hivi nakuwa narahisisha usomaji.

Ahsanteni na sikukuu njema...
 
Mbona music hazionekani tena! Night kali hii nilikuwa nina tabia ya kula songs za dini mpaka morning. Sasa hivi father christmas kama ndiyo inakuja at the expense za zile clicks za musics, better remove. Unless I dont know how to access the nyimbos.
Nadhani ukiangalia kwenye Navigation bar utaona hii:

 
Merry Christmass and A Happy New Year To All JF Members!
 
Thank You Invisible for Good work and Happy Festivals. Kwa wale ambao xmas imetukalia vibaya tunaweza at least kuburudika ndani ya JF.
 
Mkulu Invisible,

- Respect, heshima mbele kwa yote ya mwaka huu tuombe Mungu ya mwakani yawe safi,

- Heshima mbele kwa wana-JF wenzangu wote, kazi nzuri ya kuhabarishana na kuelimishana, na tuongeze juhudi zaidi ili iwe kali na nzito zaidi Mwakani,

- Kwa wale tuliokwaruzana tusameheane, lakini tuendelee kukata ishus hapa maana taifa letu liko njia panda sana.

Salaam kwa ndugu zangu wote hapa JF, huu ni wakati wa kupumzika kidogo na ku-reflect, kabla ya kurudi tena na kuanza upya.

Idumu JF na Mungu Aibariki Tanzania.
 
Asante sana management ya Jamii forum, kwa kweli kazi mliyofanya ni kubwa sana pamoja na wadau wote humu JF.

Nawatakia wote kheri ya Xmas na Mwaka mpya

Bye,
 
Nawatakieni nyote sikukuu na mapumziko mema. Binafsi naanza likizo leo na naamini wengi wetu tutakuwa na likizo fupi kwa ajili ya sikukuu hizi.

Kwa wanaosafiri nawatakia safari njema mwendako na tukutane mwakani, wale ambao tutaendelea kuwepo nawatakia kila la heri.

Tumekuwa pamoja kama familia, tuliokoseana tusameheane na tujitahidi kusamehe na kuchukuliana kibinadamu.

Mwaka 2008 umekuwa na mengi ambayo hatukuyatarajia mwaka 2007, vivyo hivyo mwaka 2009 utakuwa na mengi ambayo hatukuyatarajia mwaka huu.

Kisiasa taifa letu limejikuta likiingia katika historia nyingine kabisa. Binafsi naipongeza serikali iliyoko madarakani (serikali kama serikali na si chama cha siasa) kwa hatua iliyofikiwa na napenda kuwatia moyo kuwa kuna kinachoonekana, na wote wanaosaidia kuhakikisha kinaonekana basi Mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu kwani vita iliyo mbele yao ni kubwa. Ninawaombea mwaka unaofuata wafanikishe zaidi ili taifa letu lisonge mbele zaidi.

Kisoka Tanzania imesonga mbele, na bado inaendelea kuonyesha ishara za mafanikio.

Kuna mengi zaidi ya kuongelea ambayo tumeona ufanisi kama taifa. Tulikoangukia pua tusilale na kusikilizia maumivu, tujipanguse na kuendelea kupigana kiume. Kwa pamoja tutafika.

Mac
 

Ni mimi tu au ni vipi?? maana sizioni Zilipendwa, bongo fleva, injili, kama ilivyokuwa mwanzo??

mmeambiwa hadi tarehe tano mtarudishiwa kama ilivyokuwa,,,,, hata hivyo ni vyema watu mkajenga utamaduni wa kununua pia vitu mnavyopenda sio kusubiri vya bure tu, kama hivi wametoa kidogo tu mnaanza kukwazika.


all in all MERRY CHRISTMASS KWA WOOOTE WANA JF (damu) Na Watanzania Wazalendo (tu)
 
....kuna angalizo limetolewa ni muhimu kulitekeleza. Kwamba kuepuka ubaguzi ni vizuri na Sikukuu za Eid, JF ibadilishe muonekano kama ilivyokuwa sasa.

Ni kweli, ila Mkuu rangi za sikukuu ya Eid ni nini tena? ni vyema ukatuambia mapema ili siku wakibadilisha tujue mapambo ya Eid tusianze kushangaa, au nayo yatakuwa (ya kipagani?)



X-Paster rangi ya Eid na mapambo ya Eid (dedicated)ni nini mpendwa wangu?

mbarkiwe
 
Asalam aleykum,

Ama baada ya salamu za kiungwana ni matarajio yangu kwamba tunajiandaa ipasavyo kufunga mwaka wa Kirumi na Kiislamu ipasavyo. Nategemea wote tutakaa na kuanza kujitathmini sisi wenyewe kwa kujiuliza swali moja kuu: 'Je, nimeifanyia nini Tanzania 2008 na ni kitu gani niifanyie Tanzania na Watanzania 2009!~'

Krismasi nafuu, na mwaka mpya wenye matumaini mapya 2009. Maisha ni mapambano na kuhangaika na tusichoke kupambana na kuhangaika!

Hali kadhalika sote tusherehekee miaka yote mipya na hata ile ya KIchina kwa matarajio kwamba: WE LIVE, AND LET OTHERS LIVE!
 
Kwenu mabibi na mabwana vijana, wazee na wakulu wa jf,
heri na fanaka ya noeli na mwaka mpya 2009! zidumu fikara......!
 
Kheri ya Mwaka Mpya. Merry Christmas wengine. Bila shaka mambo yatakuwa sawa sawa tu mwakani au yaweza kuwa zaidi.
 
Thank you Invisible and your crew for the good job done in 2008. We wish you all the best in 2009. We hope to see more comments and contributions in the coming year. For me, JF has become my information base. I thank all who have contributed to this forum wisely.

MERRY CHRISTMAS AND A HAPPY NEW YEAR TO ALL JF MEMBERS AND NON-MEMBERS.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…