Hapi akabidhi tani 5 za saruji kambi ya polisi Msimbazi

Egnecious

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
875
960
HAPI AKABIDHI TANI 5 ZA SARUJI KAMBI YA POLISI MSIMBAZI

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Ally Hapi leo ametembelea kituo cha Polisi cha Msimbazi jijini Dar es salaam ambacho kilipatwa na ajali ya moto siku za hivi karibuni na kutoa msaada wa mifuko 100 ya cement sawa na tani 5.

Katika ziara yake kwenye kituo hicho, Mh. Hapi ametembelea kambi ya makazi ya askari na familia zao iliyoko nyuma ya kituo hicho ambapo amekabidhi mifuko hiyo ya Saruji kwa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala Ernest Matiku na kuagiza kuwa saruji hiyo itumike kwa ukarabati wa jengo zima la kambi hiyo ambayo inakaliwa na familia 72 za askari.

Kaimu Mkuu wa Mkoa ameeleza kuwa Polisi wanafanya kazi kubwa ya kulinda amani na usalama na hivyo jamii haina budi kuwaunga mkono.

Kwa upande wake Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi Ilala Ernest Matiku ameeleza kuwa wanamshukuru Kaimu Mkuu wa Mkoa kwa msaada huo kwani jengo lao limechakaa sana hali inayohatarisha usalama wa askari na familia zao.
Hivyo wataanza ukarabati mara moja vifaa vitakapo kamilika na kila kitu kitafanyika kama ilivyo kusudiwa.
1483796502901.png
 
Back
Top Bottom