Hapana, hapana, hapana.

Hapana, hapana, hapana.

Ishebo

Member
Joined
Apr 17, 2013
Posts
78
Reaction score
18
Tumekosea wapi? tulianza lini kukosea? tutatubu lini? je ni watanzania wote waliokosea? ni nini hatma ya kukosea kwetu kwa kizazi cha kesho? uliza maswli uwezavyo kadri ya uwezo wako huwezi kupata jibu la moja kwa moja.

Haturudishani darasni lakini ni vyema kutambua kasi ya maendeleo ya Tanzania kati ya miaka ya 1961-1980. Kwa wanaotaka kujua kulikoni miaka hiyo wanaweza kusoma kitabu kilichoandikwa na Baba na wa taifa kiitwacho 'WE MUST RUN WHILE THEY WALK' lakini pia kitabu kingine ni 'FREEDOM AND DEVELOPMENT'.

Hoja yangu siyo kurudishana darasni, yametokea mengi, juzi juzi wamesikika baadhi ya watanzania na baadhi ya vyombo vya habari vilisikika vikisema ujio wa Rais Obama wa Marekani kuwa ni 'KUITAMBULISHA TANZANIA KATIKA ANGA ZA KIMATAIFA'. Hapo hapo TBC1 wakaweka historia kati ya Tanzania na Marekani enzi za Baba wa taifa na Rais John F. Kennedy. Ninashindwa nizungumzie nini maana taifa limeanguka "HALIJATELEZA" ninajitahidi kujaribu kuondoa ushabiki wa kisiasa, tofauti na vijana wengi tunavyochanganya ushabiki wa kisiasa na maslahi ya kizazi cha kesho.

Leo najikita pamoja na mambo mengine UDHALILISHAJI ULIOFANYWA NA BALOZI WA CHINA NCHINI' Nina hakika jambo lililofanywa na huyu Balozi wa China ni fedheha kwa taifa letu. Kwa uelewa wangu mdogo juu ya mahusiano ya taifa moja na jingine katika masula ya kidiplomasia 'THE VIENNA CONVETION ON DIPLOMATIC RELATION'. Pamoja na mambo mengine, sheria hiyo inakataza mabalozi kushiriki moja kwa moja katika masuala yanayolenga itikadi ya kiundi lolote.

Sina uhakika na elimu ya huyu balozi wa China nchini, lakini pia sina shaka na elimu ya China, na kama hivyo ndivyo, huyu balozi wa China nchini alikuwa anafanyaa hivyo kwa maslahi ya nani? hap lazima twende mbali juu ya ujio wa Rais wa China nchini ambapo mikataba yake na Tanzania imekuwa ya usiri mkubwa, lakini pia China itambue kuwa sintofahamu yake kuhusika katika mchakato wa gesi ambapo mpaka leo hii bado hakuna majibu ya kutosha.

Angalizo, serikali inatakiwa itambue mabadiliko makubwa ya kifikra ambavyo kwa vyovyote vile kuyazuia hayo mabadiliko ni ndoto za mchana kweupe. Niliianza kwa kusema je tulikosea wapi? jibu rahisi ni mfumo kiziwi, wala hatuwaijbiki kuendelea nao, tafsiri ya mfumo ni kuiondoa CCM madarakani, nalazimika kuongelea siasa kwani hamna jinsi unavyoweza kuongelea hatma ya TANZANIA bila kuongelea madudu ya CCM.

Moja ya hotuba za baba wa taifa alizowahi kuzitoa, moja inaendana na hali halisi ya tanzania kwa sas, hiyo hotuba inajulikana kama ' THE SECOND SECRUMBLE FOR AFRICA'. Hii serikali imechoka kama alivyokili waziri mkuu wetu.

STAND STRONG FOR TANZANIA.

Kila la kheri
 
Back
Top Bottom