Hapa Tibaijuka amechemka

Hapa Tibaijuka amechemka

Geza Ulole

Platinum Member
Joined
Oct 31, 2009
Posts
76,474
Reaction score
108,180
[h=1]Maeneo ya wazi ni ruksa kutumika-Wizara ya Ardhi[/h]
anna_tibaijuka.jpg
Waziri wa ardhi na Makazi,Profesa Anna Tibaijuka.
KWA UFUPI
“Tunajua halmashauri zetu hazina uwezo wa kuyatunza maeneo hayo, maana mengine yameanza kuonekana vichaka, kinachotakiwa ni kufuata taratibu zilizopo ili ufanye biashara eneo hilo,” alisema Burra.


WIZARA ya Ardhi, Nyumba na Makazi imekubaliana na hatua ya maeneo ya viwanja vya wazi (open space) kutumika kwa shughuli za kibiashara ili kuyaweka mazingira ya viwanja hivyo kuwa safi wakati wote.
Kauli hiyo imefuatia baada ya maeneo hayo kukosa matunzo na badala yake kugeuka vichaka na maeneo ya kutupia takataka katika baadhi ya maeneo hususan jijini Dar es Salaam.
Awali Serikali ilifanya oparesheni katika maeneo hayo na kuwaondoa wakazi wote waliokuwa wamevamia maeneo hayo na kuwataka waondoke mara moja kwa mujibu wa sheria.
Akizungumza na Mwananchi ofisini kwake, Mkurugenzi wa Mipango na Miji katika wizara hiyo, Albina Bura alisema kuwa, Watanzania wanayo fursa ya kutumia maeneo hayo kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Serikali kupitia nakala ya Serikali (Government notice) ya mwaka 1994.
“Tunajua halmashauri zetu hazina uwezo wa kuyatunza maeneo hayo, maana mengine yameanza kuonekana vichaka, kinachotakiwa ni kufuata taratibu zilizopo ili ufanye biashara eneo hilo,” alisema Burra.
Burra aliongeza kuwa shughuli za kibiashara katika maeneo hayo lazima yazingatie vigezo vyote na hakuna gharama zozote atakazotozwa mtu, lengo ni kufanya mji uonekane safi. Alisema kinachotakiwa ni kuwasiliana na uongozi wa Serikali za mtaa wa eneo husika pamoja na halmashauri hiyo ambayo itakupatia mkataba wa kuendesha biashara hiyo.
“Utakapokuwa umefanikiwa kuingia makubaliano hayo na halmashauri,hutakiwa kubadilisha, maana mwingine anaweza kusema anataka kufanya biashara ya vinywaji na sehemu ya kupumzikia lakini baadaye utakuta amefungua gereji au biashara nyingine ambayo haikubaliki,” alisema Burra.
Baadhi ya vipengele vinavyoeleza juu utaratibu wa kufanya biashara katika eneo hilo ni pamoja na mfanyabiashara kuhakikisha mazingira ya eneo husika yanakuwa safi wakati wote.
“Pia makubaliano ya kufanyabiashara katika eneo hilo yatafanyika kwa kipindi cha miaka mitano tu baada ya hapo kama atapenda kuongeza muda ataingia makubaliano tena,” alisema Burra.
Maeneo ya wazi ni ruksa kutumika-Wizara ya Ardhi - Kitaifa - mwananchi.co.tz


Kwa kukuhakishia tu watu watajenga fremu permanent za biashara kabla ya kugawana! Sasa sijui utamlilia nani? Hivi kazi za halmashauri ni nini? Hivi kweli yule Waziri Mkuu wetu aliyejeuka waziri Mkuu wa Mkoa Katavi anashindwa kuamrisha ununuzi wa majengo kuu-kuu na kuyavunja na kuyafanya ya biashara? Watu wa mipango miji wako wapi? Au hii ni opereshani ya kumkwepa Lema Arusha?
 
ngoja nikalikabe lile eneo karibu yangu, kumbe ruksa?
 
Kutumika kwa shughuli za kibiashara kwa vipi hasa? Vipi, Halmashauri zimeshindwa kutunza hivyo viwanja au wanatumia hela kushonesha majoho ya madiwani pamoja na kulipana posho?Nina hakika serikali ingetoa 'ultimatum' kwa kila Halshauri kuweka viwanja vya wazi safi ndani ya mwezi mmoja, ama Mameya na wakuregenzi kuachia ngazi, tungeona kila mahali kuna maua. Halmashauri zetu wana uwezo kabisa wa kutunza viwanja vya wazi, tatizo hii nchi kila kitu kinafanywa na serikali kuu, na matokeo yake Mayor, wakuregenzi au hata wakuu wa mikoa/wilaya wamebakia kuwa wauza sura!
 
Sasa huu ujinga mwingine serikalini. Tunarudi kule kwenye nyumba za serikali na Magufuri mwisho wa cku watoto wachezee wapi. Hayo mnayosema majengo ya muda watajenga magorofa hapo hapo baada ya miaka kadhaa anamilikishwa. Na hii itakuwa biashara ya Mafisadi na Majizi ya CCM.
 
Kweli naona anafuata nyayo za LOWASA kipindi kile yuko wizara hii hii....GAMBA NI GAMBA tuu..........
 
Kama zinaweza kutumika kwa biashara basi hizo siyo sehemu za wazi tena, ni viwanja vya baishara. Je, ni nini ilikuwa sababu ya kuyaacha maeneo hayo wazi? ili watu waje kufanyia biashara???
Kwa kauli hii, jijini hakuna eneo litakaloaki wazi...
 
Back
Top Bottom