Hapa nchini kuna bima za kampuni za nje?

Hapa nchini kuna bima za kampuni za nje?

Swet-R

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2018
Posts
5,694
Reaction score
8,283
Habarini humu ndani.

Nauliza kama kuna bima za makampuni ya nje? Mfano mtu anataka kuwekea shamba bima ya moto. Naona haya makampuni hapa nchini mengi ikifika kipindi umepata tatizo ulilowekea bima ulipaji wake ni mgumu sana,unaweza kusugua hata miaka kufuatilia kile ulichokikatia hiyo bima.

Mwezi uliopita tumepata hasara ya mashamba ya miti huko njombe yameungua moto heka nyingi. Kabla ya hiyo ajali nilikuwa na nia ya kuliwekea bima shamba hilo. Katika kuwashirikisha watu wakanikatisha tamaa kuhusu bima za hapa nchini.
 
Ooh pole sana mkuu, ila bora hata ungekatia bima tu leo ungekuwa na wa kuwadai
Ona sasa waliokukatisha tamaa wamekutia hasara.
Ngoja nikusaidie kuwatusi
Washenzi kabisa hao
 
Ooh pole sana mkuu, ila bora hata ungekatia bima tu leo ungekuwa na wa kuwadai
Ona sasa waliokukatisha tamaa wamekutia hasara.
Ngoja nikusaidie kuwatusi
Washenzi kabisa hao
Ni kweli kabisa mkuu. Mimi mwenyewe baada ya tukio nikafikiria bora ingekuwa nusu shari-ningeendelea kupambana nao kwa matumaini-kuliko hii shari kamili. Inabidi sasa sasa nikatie tu hiyo
 
Back
Top Bottom