Hapa nahitaji Ushauri wa kunitoa shimoni

Hapa nahitaji Ushauri wa kunitoa shimoni

nzovwe

Senior Member
Joined
Aug 15, 2013
Posts
118
Reaction score
31
Habari wadau,

Mimi ni graduate wa 2012 pale SUA (BSc. Agricultural Economics and Agribusiness), nipo hapa Dodoma nikifanya kazi ya mtu stationary karibu na SJUT. ofisi hii ni ya Mhadhiri mmoja wa pale UDOM.

Wakati ananiomba nimsaidie kazi hii, nikampa masharti kuwa nikipata kazi niliyosomea mda wowote nitatoka ofisini kwako akanijibu hakuna shida. Baada ya mda mfupi akaniomba CV yangu, nikampatia, katika hiyo Cv akaniambia kwasasa nisichague kazi bali kazi atanitafutia yeye mwenyewe na ninatakiwa nisichague maeneo ya kufanya kazi.

Baada ya mwezi mmoja akaja na kazi za aina mbili (Accountant na moja ya kilimo) na akasema kazi hizi zote zinapatikana vijijini hapahapa Dodoma na yeye ndiye anayehusika kutafuta watu, kwa hiyo nijiandae kwa kazi moja wapo. Baada ya kuona mda unaenda na hamna kinachoendelea nikaamua kuacha kazi yake pale Stationary. Wafanyakazi anaowapata hawakai zaidi ya miezi sita kwasababu ofisi ipo bize sana na malipo hafifu.

Kwasasa wafanyakazi wote wamekimbia kazi na ameniomba nimsimamie tena mpaka atakapopata wafanyakazi wengine, nami nmeacha shughuli zangu na kumsimamia kwa mara nyingine tena ila kufikia hapa nimechoka na nataka niendelee na mambo yangu maana hata mimi nina PC mbili.

Dilema yangu ni kwamba amerudia tena mambo kama ya mwaka juzi: Ameniomba CV tena na akasema nimtumie mtu mmoja hivi nami nikafanya hivyo na nikaahidiwa tar 27 Febr 2014 nitaitwa kwa interview lakini mpaka sasa hakuna kitu. Wizara ya kilimo nayo haijatuchagua kuhudhuria interview kwa kozi yetu ingawa tangazo la tar 27 Nov 2013 katika kitengo cha Agricultural Research offiser II na Agro officer II ingawa waliweka kwamba waliosoma Agribusiness/ Agricultural Economics nao wanaweza kuapply.

Kwasasa naamua kujiwekea limit kwamba nitafanya kazi ya mtu ambaye yupo tayari kunilipa kuanzia Tshs 450,000/= kwa mwezi otherwise nikijiajiri naweza kujilipa zaidi na nilijaribu nikaweza kujilipa mpaka laki 6 kwa mwezi nikiwa na PC zangu hizo Mbili. Huyu bosi wangu wa hapa chuoni hana uwezo wa kunilipa hizo pesa na ananihitaji sana ingawa nimejaribu kumpa ushauri kwamba awachukue wale waliosomea Stationary lakini naona anapiga chenga anasema wanasumbua, kwa siku namuingizia kuanzia 150,000-300,000 kwa bei ya photocopy Tshs 30/= na Printing 100/= Binding 1000-1500 na mengineyo hapa SJUT mazengo.

Naombeni ushauri:

Je anaweza akanipatia kazi kwenye makampuni mengne ingawa ofisini kwake wafanyakazi hawakai?, Je nifanyeje na mimi nahitaji kazi nyingine na kodi ya kujilipia chumba cha biashara kwasasa sina?

Yeye ndiye anayeombwa mara kwa mara kuwa-interview watu ambao wanataka kuajiliwa kwenye makampuni mbalimbali kwa hapa Dodoma.

Please naombeni ushauri, Intellectual mwenzenu.

Be patient!, be Critical thinker
 
Pole dogo.

Ila ukijaribu kutulia na kusoma tena na tena ulichoandika,utaliona jibu unalolitafuta.

Nakuhakikishia lipo,mi nimeliona.ila ukiona mwenyewe ndio itakuwa na tija zaidi.
 
Bosi hapo nmeshndwa kupata jibu, thus y nmelileta kwenu kwa ushirikiano
 
fanya kaz kwanza ili upate kod ya chumba, ungekua dar tungefanya wote kwan na mm nataka nifanye ktu kama hicho
 
Pamenichosha mkuu, watu wa kusaidiana nao kazi ninaoletewa nakuwa kama naanza kuwafundisha kazi. Mda huohuo ofic iko bize sana na unaletewa mtu wa kumuelekeza kila kitu. Ndio nazidi kuchoka zaidi
 
Back
Top Bottom