SHIEKA
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 8,240
- 4,265
Tarehe 3/3/2016 binti yangu anayesoma mawenzi sekondari moshi alirudishwa nyumbani akiwa na barua ya uongozi wa shule iliyonihitaji niende shuleni hapo kujadiliana na waalimu juu ya maendeleo na nidhamu ya mwanangu. Sikuielewa kabisa hiyo barua, ikabidi nimuulize kijana kuna nini.Alinijibu kwamba shuleni kulikuwa na operesheni kali ya kukamata simu za wanafunzi.
Nikamwuliza na wewe ulikamatwa na simu? Nilimwuliza kwa sababu mie sijawahi kumnunulia hata kinokia tochi. Jibu alilotoa ni kwamba eti katika ile patashika ya kamatakamata mwanafunzi mmoja kwa kujihami alitupa simu kwenye kitanda chake hivyo simu ikaonekana ni yake (ya binti yangu)
Mazungumzo kati ya wazazi na uongozi wa shule yalifanyika 10/3/2016.Uongozi wa shule ulituonesha simu na vifaa vya mawasiliano walivyovikamata.Si ma-iphones, ma-ipads ma-samsung galaxy, na masimu ya ajabuajabu ambayo hata majina yake sijui.
Ilitushangaza sana jinsi watoto walivyokazania simu kuliko kitabu.
Iliamuliwa kwamba vikochokocho vyote viharibiwe na uongozi wa shule ukasema utachukua jukumu hilo.
Ni kweli simu ni chombo muhimu kwa mawasiliano lakini kwa upande wangu si chombo cha manufaa kwa mwanafunzi aliye shuleni.
Pongezi nyingi uongozi wa mawenzi sekondari moshi kwa kuwaweka watoto kwenye mstari mzuri wa maadili.
friend wangu Amavubi, vipi, ulikuwepo?