Hana mikono/miguu lakini anaendesha gari........ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hana mikono/miguu lakini anaendesha gari........

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Sikonge, Jan 15, 2012.

 1. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #1
  Jan 15, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Hii ni video maalumu kwa wale wote walioanza kuweka vimaneno vya kishamba humu ndani.

  Sintawataja ila wanajijuwa na wanafahamu kabisa hayo maneno wameyaandika wapi.

  Wamekuja na vijiswali vya kujifanya wanafahamu sana kumbe hawajui kitu.

  Haya sasa, angaalieni hii video na tusikie mtasema nini....... Anaitwa Barbara Guerra.  Ukisiliza 1:40, inasemwa wazi kabisa kuwa, gari halina modifiication yoyote kwa ajili ya Vilema (Disabled).


  Mwingine huyu hapa, now what????
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #2
  Jan 15, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Fanya ed. ya ile nomino inayoanza na vi-, tafadhali. Last but one para
   
 3. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #3
  Jan 16, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Hujaeleweka Mkuu wangu. Hivi neno, Kilema/Vilema lina ubaya? Au ulimaanisha kuweka herufi kubwa?

   
 4. chapaa

  chapaa JF-Expert Member

  #4
  Jan 16, 2012
  Joined: Feb 19, 2008
  Messages: 2,355
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  hujafa hujaumbika
   
 5. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #5
  Jan 16, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Ukweli mtupu Mkuu.

  Mtu ukilalamika kuwa wewe ni masikini wakati una viungo vyote salama, basi ujuwe una matatizo.

   
 6. r

  ral Senior Member

  #6
  Jan 16, 2012
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 126
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Sikonge,

  bila kuficha hisia video ya huyo dada imenitoa machozi, ama kweli hujafa hujaumbika

  Sikonge;3140863]Hii ni video maalumu kwa wale wote walioanza kuweka vimaneno vya kishamba humu ndani.

  Sintawataja ila wanajijuwa na wanafahamu kabisa hayo maneno wameyaandika wapi.

  Wamekuja na vijiswali vya kujifanya wanafahamu sana kumbe hawajui kitu.

  Haya sasa, angaalieni hii video na tusikie mtasema nini....... Anaitwa Barbara Guerra.  Ukisiliza 1:40, inasemwa wazi kabisa kuwa, gari halina modifiication yoyote kwa ajili ya Vilema (Disabled).


  Mwingine huyu hapa, now what????
  [/QUOTE]
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #7
  Jan 16, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Kwani sheria za udereva zinasemaje kuhusu walemavu?
   
 8. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #8
  Jan 16, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  RAL,

  Nafikiri ni kumshukuru Mungu kwa kumpa huyu dada uwezo wa kufanya mambo kwa kutumia miguu na si mikono.

  Ndiyo maana wanasema binadamu ana SIX SENSE ila hiyo ya sita huwa imejificha sana. Mtu ikibidi kuitumia, basi unaweza kuiamsha na ukaanza kuitumia. Ndiyo maana watu wanasema ukikutana na Steve Wonder mara kadhaa, atakukariri hatua zako na unapokuja tu kwake, atakuita jina.

  Wa-Asia hasa wacheza Martial Arts, huwa wanaziamsha hizi hisia na anaweza kupigana na wewe hata kama amefumba macho. Pia wanaweza kujua kama kuna fujo, mtu gani ni hatari na yupi si hatari. Steven Segal amekuwa mtu anayewafundisha Polisi wenzake jinsi ya kung'amua vitu kama hivyo.

  Nafikiri inabidi kuwatia moyo hata vilema wengine kuwa akiwa kilema si mwisho wa dunia. Anaweza kufanya kila kitu na hata kuwazidi walio wazima. Kuna yule Profesa nimemsahau, anayeongea kwa kutumia misuli ya uso. Jamaa ni mkali mno na heshima juu kama Msomi na uprofesa wake wa darasani.

  Kuna dada mwingine nilimsoma, yupo Sweden na yeye anafanya kila kitu kwa miguu tu. Ila yeye ilikuwa ni makosa ya dawa za kuzuia mimba zilizotengenezwa miaka ya 60 na kampuni ya German. Akina mama wote waliotumia hizo dawa na baadaye kuacha ili washike mimba, wengi walizaa watoto vilema.

  kilema kibaya na ambacho mtu inabidi ulie ni KILEMA CHA AKILI.
   
Loading...