Mzee wangu MohammedNkuba25,
Si kama hayo yalifanywa kwa bahati mbaya.
Kuna watu hawakuitaka historia hii.
Historia hii ilikuwa inawatisha sana na ndiyo
kisa cha kuja na historia ya Kuvukoni College.
Kolorama,Mzee Wangu Mohamed Said asalaam alaykum. Nimekuwa kimya kwa muda ila uzi haujanipita. Nakushukuru nimepata vitabu kwenye duka la ibn hamza. Hakika haya ni madini kama wasemavyo watoto wa mjini. Mungu akupe uhai mrefu uzidi kutupa ilm sisi vijana wako na wengine wengi ambao wanasoma kimyakimya
Marehem Ngariba alikuwa anapenda kutumia aya hii kabla hajaanza mihadhara wakati wa uhai wake allah amsameh makosa yake na amuweke ktk Firdaus.Kolorama,
Furaha yenu ndiyo furaha yangu.
''Elimu bila khiyana,'' chembelecho Maalim Faiza.
And say, "Truth has come, and falsehood has departed."Marehem Ngariba alikuwa anapenda kutumia aya hii kabla hajaanza mihadhara wakati wa uhai wake allah amsameh makosa yake na amuweke ktk Firdaus.
WAKUL JAA LHAKU WAZAA LHAKKU INNALBAATILA KANA ZAHUKA......
Kolorama,Marehem Ngariba alikuwa anapenda kutumia aya hii kabla hajaanza mihadhara wakati wa uhai wake allah amsameh makosa yake na amuweke ktk Firdaus.
WAKUL JAA LHAKU WAZAA LHAKKU INNALBAATILA KANA ZAHUKA......
Ammarito,Al Habiby Sheikh Mohamed Said, nashukuru sana kwa kutuelimisha, habari hii imenifurahisha zaidi baada ya kumzungumzia Mama Daisy (Sisi tulikua tunamuita , Bi.Dezi), sikujua asili ya jina hilo kabla ya kusoma hapa.
Bibi huyu ametulea sisi pale temeke nyumbani kwake mtaa wa mjimwema mpaka mwisho wa maisha yake (Allahu marhamhu), nakumbuka maziko yake tumeyafanya pale katika nyumba yake mtaa wa Likwati.
Kama utakua na picha nyingine naomba unitumie.
Shukran
Mkunyegere,Hongera ni historia nzuri
17:81 wa qul jaa-al Haq-qu wa zahaqal baaTil* in-nal baaTila kaana zahuuqaa.Marehem Ngariba alikuwa anapenda kutumia aya hii kabla hajaanza mihadhara wakati wa uhai wake allah amsameh makosa yake na amuweke ktk Firdaus.
WAKUL JAA LHAKU WAZAA LHAKKU INNALBAATILA KANA ZAHUKA......
Maalim Faiza,17:81 wa qul jaa-al Haq-qu wa zahaqal baaTil* in-nal baaTila kaana zahuuqaa.
Maalim Faiza,
Allah akujaze kheri.
UKIPUNGUZA UDINI UTAKUWA MWANDISHI MZURI SANA KAKA!Mkunyegere,
Hakika historia ya TANU na harakati za kudai uhuru ni kisa khasa.
Bi. Titi Mohamed anaghadithia anasema wako Tabora 1958 wakati
wa Kura Tatu.
Hali ilikuwa tete kupelekea TANU kumeguka pande mbili.
Baadhi ya wanachama wamekataa kata kata kuingia katika uchaguzi
ule wenye masharti ya kibaguzi.
Mwalimu Nyerere ameingiwa na hofu ana wasiwasi chama kitavunjika.
Wapinzani wa Kura tatu ni watu wenye nguvu katika chama wakiongozwa
na watu kama Jumanne Abdallah, Bhoke Munanka, Sheikh Suleiman
Takadir na wengineo.
Mwalimu Nyerere akawa hana hata hamu ya kula chakula anashindia maziwa.
Bi. Titi akimmudu sana Mwalimu Nyerere na watu wengi hawajui hili jina la
Mwalimu Nyerere alipewa na Bi. Titi.
Bi. Titi kamfuata Nyerere anamwabia,'' Nini wewe nasikia hutaki kula. Unaogopa
kufungwa? Mwenzako Kenyatta yuko jela nini wewe unaogopa kufungwa?''
''Sikiliza Titi si lazima nende jela...''
Mwalimu alijibu kwa unyonge kabisa.
Ukipenda kukijua kisa cha Kura Tatu ingia hapo chini:
Mohamed Said: UCHAGUZI WA KWANZA TANGANYIKA ''UCHAGUZI WA KURA TATU'' 1958 KUTOKA KUMBUKUMBU ZAKE SHEIKH SEMBE
Mkuu mzee Muhamed hana udini hata chembe.UKIPUNGUZA UDINI UTAKUWA MWANDISHI MZURI SANA KAKA!
Gangogine,UKIPUNGUZA UDINI UTAKUWA MWANDISHI MZURI SANA KAKA!
Kenge...Mzee Mohamed Said naweza kupata namba yako ya sim?
Disguise,Ndugu Mohamed Said, napenda kusikia japo kidogo tu historia iliobeba jina la hii thread, Historia ya Chief Lukumbuzya! Bibi yangu alikua akiutaja sana huu ukoo wa kichifu!
Unachoambiwa una udini ni kuona kwamba Waislam wanaonewa japo walipigania uhuru wa Tanganyika pengine kuliko dini zingine. Hutaki kuona sababu za ndani zinazorudisha nyuma harakati za Waislam kupiga hatua ambazo zinatokana na wao wenyewe!Gangogine,
Mimi naandika historia ya uhuru wa Tanganyika ambayo kwa
bahati mbaya kwako imetawaliwa na Waislam na hivyo ndivyo
ilivyokuwa
Ikiwa wewe unaona kuwa huo ni ''udini,'' hii ni bahati mbaya
sana kwako.
Nimeandika kitabu cha Abdul Sykes naamini unakifahamu na
kilifanyiwa mapitio na mabingwa wa historia ya Afrika.
Hakuna hata mmoja kati yao aliyenishutumu kwa udini.