Hamis wa BSS - Hata kama umedhulumiwa, sio busara kuwatukana waandaaji wa BSS

kibaravumba

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
6,635
7,005
Nimesikitishwa sana na maneno ya matusi dhidi ya BSS yaliyotolewa na kijana aliyeonekana yuko humble sana na kumbe hayuko hivyo.

Hamis bado una safari ndefu ambayo ndio kwanza ulikuwa unaianza.Unatakiwa ujifunze kuwa positive kila Siku ili ufanikiwe.

Pamoja na kwamba unaamini ungepaswa kuwa mshindi kwa kura za wananchi, unapaswa kujua pia waandaaji wa shindano hilo nao wana vigezo na masharti yao.Binafsi nilikuwa navutiwa sana na uimbaji wako,lakini bado sikuwa tayari wewe ndio uwe mshindi na kubeba brand ya BSS.Nilochoona mimi,ungekuwa mvumilivu,huenda ungejaribu kushiriki tena,ungefanikiwa.

Una bahati sana pia kuonekana kupitia BSS.Hiyo ilitosha kukufanya ushukuru sana kuliko kutupa maneno makali na kuwaita akina madam Ritta "washenzi!"

Huenda kuna changamoto wanazopitia BSS ambazo hawajaamua kuziweka wazi, hadi wakashindwa kuwalipa ninyi.

Ni bora ungekuwa mvumilivu na mwenye busara katika kutoa maoni yako. Maana najua, hata kama kuna mtu mwingine alikuwa na shauku ya kukusaidia, lazima atasita kwa utovu wa nidhamu uliouonesha. Ingekuwa bora ukatumia njia halali kama alivyofanya Meshack kudai haki yako, kuliko kuongea kashfa na matusi katika media.

Nimeongea tu kukushauri sina uhusiano wowote na Madame Rita. Ila ni mpenzi wa BSS.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni washenzi ndio [in Hamis's voice].

Mwanzo dogo alivyokuwa anafuatilia alikuwa anapewa majibu ya "mpaka mwezi ujao", mwezi unaofuata tena anaambiwa "mwezi ujao".

Ndipo akaamua kwenda wizara husika. Madam Ritha akaandikiwa barua, akatoa utetezi wa kwamba wadhamini ambao ni Star Times eti hawajatoa pesa ya mshindi.

Star Times kusikia hivyo ikabidi watoe ukweli wote kwamba walishalipa kila kitu mpaka zawadi ya mshindi.

Sasa ebu niambie huo sio ushenzi ni nini?

Unforgetable
 
Kwani alikuambia ana mpango ws kuendelea na muziki? Yeye kaja kwenye shindano, kaibuka mshindi basi mpeni chake asepe. Mambo ya kusema sijui angalia future yako ni kumtisha dogo asidai chake.
Unforgetable
 
Ni washenzi ndio [in Hamis's voice].

Mwanzo dogo alivyokuwa anafuatilia alikuwa anapewa majibu ya "mpaka mwezi ujao", mwezi unaofuata tena anaambiwa "mwezi ujao".

Ndipo akaamua kwenda wizara husika. Madam Ritha akaandikiwa barua, akatoa utetezi wa kwamba wadhamini ambao ni Star Times eti hawajatoa pesa ya mshindi.

Star Times kusikia hivyo ikabidi watoe ukweli wote kwamba walishalipa kila kitu mpaka zawadi ya mshindi.

Sasa ebu niambie huo sio ushenzi ni nini?

Unforgetable
Dahh kazi kweli kweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu naye hana lolote. Shindano lile hakustahili kuingia top 20, walimbeba. Afunge domo lake.
 
Back
Top Bottom