Hamasa ya chanjo ya Homa ya Ini

Hamasa ya chanjo ya Homa ya Ini

Dr Rutagwerera Sr

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2011
Posts
5,872
Reaction score
11,661
Hello wanabodi!

Nimeona nianzishe uzi wa kuhamasisha wanaJF kufika vituo vya afya kwa ajili ya kupata chanjo ya Homa ya Ini ambayo ni hatari kuliko hata baadhi ya maradhi. Ikumbukwe Homa ya Ini inasambaa kwa urahisi hata kwa mguso wa jasho la mwenye ugonjwa. Watu wanaojamiiana ni rahisi kuambukizana kama mmoja akiwa na ugonjwa huo.

Hivyo ni rai yangu kukumbushana. Kumbuka ugonjwa huu ni hatari na unaua haraka.
 
Shida IPO kwenye gharama mbaya zaidi hata bima haihusiki kwenye hiyo chanjo.Serikali ingetilia mkazo Sana kwenye hi chanjo no muhimu Sana.
 
Mbona mnatoa taarifa nusu nusu,tajeni gharama zake au hata bima na hosp zinazotoa chanjo.
Gharama zinatofautiana baadhi ya hospitali.
Ila ni vema kufika hospitali kupata taarifa zaidi. Kuna sehemu kupima ni elfu 10 wakati kwingine 15. Chanjo ipo ktk awamu tatu. Kuna sehemu elfu 15 kwa kila chanjo, sehemu zingine elfu 25 na wengine mpaka elfu 30. Utafiti muhimu zaidi!
 
Na mimi nasubiria

Sent from my iPhone using JamiiForums
Za serikali na binafsi. Bahati mbaya bima hawafanyi coverage kwenye hili. Kupima unaweza kutumia bima. Ila chanjo unalipa kwa cash.

Kwa hospitali binafsi ni zote kubwa na hata pale Mwenge Marie Stopes wanatoa chanjo pia. Kwa za umma kuna uhaba sijajua kwa sasa kama huduma zimerudi kama awali.
 
niliambiwa kwamba ili upate chanjo ya homa ya ini lazima upime kwanza UKIMWI , je kuna ukweli gani hapo?
 
Gharama zake ni Tshs 30,000 ambayo unailipa mara 3 yaani elfu 10 kwa sindano moja

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hiyo ni bila gharama za kupima.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu mim nilipima mnazimmoja hospitali mwezi huu gharama za kupima ni 10k na baadda ya kupima chanjo ni sindano tatu ambazo unachoma ya kwanza baada ya kupima na baada ya mwezi mmoja toka uchome ya kwanza unachoma ya pili na baada ya miezi sita tangu ulivyochoma ya pili unachoma ya tatu hapo dozi inakuwa imekamilika kila sindano kwa mnazimmoja ni 15k.

Baada ya miaka mitano chanjo inaisha muda wake.
 
Mkuu una undugu na dada Seko Shamte Tingitana?
 
Back
Top Bottom