Hamad Rashid, Zitto Kabwe na Mwigulu Nchemba (Comparative analysis)

Hamad Rashid, Zitto Kabwe na Mwigulu Nchemba (Comparative analysis)

Mwigulu ameua watu, wewe unasema 'hadithi za nyuma', mzima wewe? Hivi wale waliouawa wangekuwa ni mama zako, baba zako au dada zako, ungethubutu kutamka ujinga huu? Wauaji huwa wanatafutwa hata kwa miaka hamsini, wanapobainika wanakamatwa na kunyongwa au kufungwa maisha. Mwigulu pamoja na wenzake wote waliohusika katika mauaji mbalimbali, wasubiri, muda ukifika watasimamishwa kizimbani, hata kama ni miaka 20 ijayo.

Hatutampa uongozi muuaji katika nchi hii hata angekuwa na maneno matamu kiasi gani. MWIGULU IS A MURDERER, THERE IS NO CHANCE FOR A MURDERER TO BECOME A LEADER, A PLACE IS RESERVED FOR HIM AT KEKO.

mkuu, kama umemwelewa vizuri mjenga hoja MWIGULU keshaonyesha kupevuka, hizo hadithi za nyuma unazotaka kuzirejesha hazina maana tena.
 
MAZITO YAVUJA KIKAO CHA WENYEVITI WA MIKOA CCM,BARUA YA KINANA YAKOSOLEWA.

Katika kikao cha wenyeviti wote wa CCM wa mikoa kilichofanyika katika ofisi ndogo za Lumumba jijijin Dar es Salaam jana tar.24. Wenyeviti hao wakiwa katika kikao chao kilichokuwa kinajadili mambo mbalimbali ya chama na utekelezaji wa mambo ya Uchaguzi, walipofika kwenye agenda ya ujenzi wa chama walionekana kusikitishwa kwao kwa katazo alilopewa Naibu katibu Mkuu wa CCM ndg Nchemba huku akiwa ametokea kufanya kazi nzuri ya uimarishaji wa chama.

Akiwa wakwanza kuchangia hoja hiyo mwenyekiti wa Manyara Ole Muksi alisema "tumeshangazwa sana na Barua ya Katibu Mkuu kwenda kwa Naibu wake, Kwanza Mwigulu alikuja Wilaya zote za Mkoa wangu wa Manyara, Kote alikopita tumeshinda kwa kishindo, tumeshinda mpaka karatu mwenyekiti, tumepata vijiji kwa ushindi mbulu, Hydom, kubwa zaidi Mwigulu hakuongelea mambo ya Urais wala kutaja jina lake wala kusema na mjumbe yeyote.
Kumwandikia barua kwa fitna itavunja moyo watu wanaojitolea kujenga chama. Binafsi sikuona kama sababu ni urais labda sababu ni kukubalika kwake, sasa hili pimeni kama linakijenga chama au tunabomoa chama.
Alipokuaja tulipata watu zaidi ya elfu sita saa tatu asubuhi na zaidi akamng'oa katibu wa CHADEMA wilaya ya Karatu, haijawahi tokea. Chama inabidi itathimini upya katazo hilo. Chama hakiwezi kujengwa na Nape na kinanan pekee yake,Kama shida ni unaibu wamtoe unaibu lakini sio kumzui kazi za unaibu.

Naye Mama Buhiye mweneyekiti wa CCM kagera alisema "Mwigulu alitusaidia sana, tena tunaomba aje tena, kwa kweli hakuonesha wala kuongelea Urais. Pia hakukutana na kiongozi yeyote wa kagera. Tofauti na wengine yeye alikuwa akimaliza mkutano anaruka kumaliza na kuruka na jion hata chakula cha pamoja hakikwepo. Wasimwone kiasi hicho. "
Wakati huo huo Dr Kaburu mwenyekiti wa Mkoa wa Kigoma alisema "CCM isitengeneze chuki na vijana, mpaka sasa uraiani inasemekana kuwa sisi tunamziba mdomo kijana ambaye hajui kupendelea kitu , kisa alisemea kuwa wezi wa escrow wafilisiwe, kisa alisema kodi kwenye escrow irudi ni ya umma. Kisa aliongea kwenye katiba, kisa anakemea uovu wa baadhi ya watendaji wa serikali.Picha hii sio nzuri kwa Chama na watanzania, kumzui kufanya mikutano mtu ambaye amekua bega kwa bega Kuimarisha CCM . Sisi tumemwalika tangu mwezi wa tisa mwaka jana kwa kikao cha kamati ya siasa, nimeambiwa tanga walimwalika tangu mwezi wa kumi, kama ilvyo mara na shinyanga tena kwa barua, waache kugawa chama. Mimi nimempigia Kinana kumlalamikia hili, hata yeye halmjengi. Tunaomba makao makuu iangalie upya katazo hilo. Huyu ni naibu katibu mkuu sio personal assistant."

Hali iliendelea kuwa ya utulivu zaidi baada ya Saanya Mwenyekiti wa Mara aliposema makamanda wake walikataa kuapishwa na mtu mwingine na tulimwalika tangu mwezi wa nane. "Wananchi mara wamerudisha imani kwa Chama hivi majuzi baada ya Mwigulu kuweka mambo sawa pale Msoma,watu waache wivu, Mwigulu hakuongelea mambo ya Urais alikijenga chama.

Msukuma Mwenyekiti wa Geita aliyekuwa kwenye mizunguko na Mwigulu alisema "helkopita isiwe nongwa, Nilimkaribisha Mwigulu, tulishatumiaa helikopita hiyo na Dialo wilaya zote za Mwanza, na Makonda wilaya zote, na Mama Tibaijuka kagera yote, na Lameck Airo jimbo lake lote. Hii isiwe nongwa. Kijana anakubalika, anajenga chama tuache wivu na kusingizia helkopita. Sisi Geita tumeandika barua kumwita.
Dialo alithibitisha kuitumia helkopita hiyo. Ni kweli mwenyekiti nimetumia helkopita hii. Labda tuambiwe kama kwenye chama chetu ni kosa, wala sio kwa Mwigulu tu.

Kwa upande wake Kimbisa alisema jambo hili lilipaswa lipitie vikao kabla ya barua, sisi Kamati kuu hatujawahi kujadili jambo hilo. Baraua imeandikiwa Zanzibar hivyo nadhani utaratibu wa CCM hata kwa mpika chai uamuzi hufanyika kwa kupitia vikao. Nasubiri taarifa ije kamati kuu"
Wakati hayo yakiendelea,Baadhi ya wenyeviti walikuwa na sauti za chini kuwa CCM haijengwi na watu wawili tu,Chama kinajengwa na wanachama na Viongozi wote.

My take, Chama Cha Mapinduzi ni kikongwe na kinajua namna ya kudeal na Mambo madogomadogo kama haya,Urais kwa mwenendo huu utapelekea wananchama na Viongozi wasifanye kazi ya chama,CCM ni Zaidi ya Urais.
 
mwigulu ni suluhisho la matatizo ya nchi hii 2015 tumpe aongoze dola
 
Nina uhakika kuna siku tena utakuja kuyaonea aibu maandiko yako haya tena.

Zito na Hamad wanafanana sana katika jambo moja, wote ni 'great opportunists', wapo tayari kufanya lolote ili kupata madaraka na umaarufu. Ikitokea Zito akakosa hata ubunge, si ajabu ukamwona akifanya kwa uwazi kabisa siasa za CCM.

Zito na Hamad wote kwa pamoja ni watu wasioweza kufanya kazi na timu yoyote ile, wataanya kazi na watu wengine kama wao wapo kwenye uongozi wa juu. Wote ni wabinafsi, wote ni watu wasioamini kuwa kuna watu wana uwezo kama wao au zaidi yao.

Zito ana sifa ya ziada, yupo tayari kupokea hela yoyote kutoka kwa yeyote alimradi kama anajua kuwa hela hiyo itamsaidia katika kuyafikia madaraka. Ndiyo maana Zito alikuwa akichukua pesa toka CCM (mpaka leo hajawahi kukanusha).

Mwigulu is a murderer, muuaji hata kama atajifanya amebadilika kiasi gani, ni mhalifu na mahali pake ni gerezani. Kuna watu wamepoteza ndugu zao, mama zao, baba zao, dada zao, marafiki na majirani kutokana na mtu huyu. His name is not worth to be mentioned in an example of anything than cruelty.


Natamani kuona wananasiasa angalau wanakuwa kama hawa wawili wa mwisho. Wakati Hamad anafukuzwa CUF mimi nilikuwa na mtu ninayeandika na kuingia katika mijadala mbalimbali kuonyesha kuwa Hamad alionewa ( japo si mwanachama wa CUF), nilikuwa mtetezi wake, lakini sasa kila nikiyatazama nayaonea aibu maandiko yangu, sitaki hata kuyatazama.

 
Leo nimeona ni vema kuwafanyia mjadala wanasiasa hao watatu, sit tu kwa sababu ya majina yao makubwa na mchango wao kwenye siasa za Tanzania bali pia mienendo yao na harakati zao kisiasa. Kwa maoni yangu kuna vitu ambavyo vinawafananisha sana lakini pia yapo mengi yanayowatofautisha.

Hamad Rashid yupo kwenye mgogoro na “chama chake” cha Cuf toka mwaka 2012 na hatimaye kufukuzwa chamani na yeye kwenda mahakamani kupinga kufukuzwa kwake, mpaka leo amebaki na ubunge kwa amri ya mahakama tu, Zitto Kabwe naye ni vivyo hivyo kwa upande wa Mwiguru Nchemba ni hivi majuzi tu ameingia kwenye msuguano na Katibu wa chama chake, yeye amepigwa marufuku kufanya mikutano na au ziara mbalimbali za kichama. Sababu zilizopelekea migogoro na wakubwa wao ni moja, madaraka.

Wakati Hamad Rashid akitajwa kufanya kampeni chafu tena zenye kuratibiwa na baadhi ya makada wa ccm ili kuchukua nafasi ya Katibu mkuu, Zitto anatuhumiwa kutaka kuchukua nafasi ya M/kiti wa CDM kwa ufadhiri wa wasaliti na baadhi ya vigogo wa serikali, huku Nchemba akituhumiwa na katibu wake kufanya ziara na mikutano ya hadhara kwa lengo la kimarisha kampeni zake za kuteuliwa na CCM kugombea urais octoba mwaka huu kwa kuungwa mkono na baadhi ya makada wa chama chake.


Sababu hizo za migogoro na vyama vyao na hali halisi ilivyo sasa hivi inatoa taswira sahihi nini kiliwasababishia migogoro na ni kwa kiwango gani tuhuma dhidi yao ni sahihi au sio sahihi. Hamad Rashid Mohamed mjenga hoja imara na mkosoaji mkubwa dhidi ya mfumo wa serikali mbili, mpiganiaji wa maslahi ya Zanzibar dhidi ya “unyonyaji” wa Tanganyika mara tu baada ya kufukuzwa uanachama akatangaza kuunda chama chake huku akienda mahakama kupinga kuvuliwa uanachama (inachekesha).

Lakini ghafla mtazamo na falsafa yake ya mambo ikabadilika, Imani yake ya kisiasa ikabadilika pia, mtazamo wake kisiasa, falsafa na imani yake kisiasa ikawa ni sawa kabisa na ile ya Chama cha mapinduzi, hili lilionekana wazi katika bunge la katiba. Badala yake Hamad akawa political ankerman wa chama cha mapinduzi.

Zitto Kabwe atasikitikia uamuzi wake wa kufuata ushauri wa maswahiba zake kisiasa, kwa bahati mbaya wengi wao hawana uzoefu mkubwa kama yeye katika practical politics bila kuwa na uelewa mpana wa siasa za ndani ya vyama wakataka kumkweza na kumuweka juu ya chama hivyo kuzua migogoro na waasisi na baadhi ya wanachama wa muda mrefu. Mara tu baada ya kufukuzwa uanachama yeye na wenzake, Zitto akaenda mahakamani kuweka pingamizi lakini kama ilivyo kwa Hamad naye anahusishwa na chama kimoja cha siasa.

Hamad na Zitto wanatofauti kubwa katika harakati zao kisiasa.

Zitto bado anaamini na ameonyesha bado anasimamia misingi ileile aliyokuwa nayo Chadema. Ikumbukwe kuwa Hamad hakutoka CUF kwa sababu ya kupinga misingi au falsafa ya chama bali mgogoro wa kiungozi( tofauti na Himid aliyepinga sera na falsafa ya CCM), Kwa upande wake Zitto ameonekana kuwa bado ni mpinzani, kinadharia bado ni mwana chadema, ni mwana ukawa. Mwiguru Nchemba katika miaka hii miwili amefanya mabadiliko makubwa (self-political evolution) katika harakati zake za kisiasa kutoka siasa za kushambulia wapinzani hadi siasa za kitaifa, amebadilika mno.

Sasa amekuwa akijitokeza kama mtaifa mwenye kuangalia maslahi mapana ya taifa kuliko ya chama chake. Mwenendo huu mpya haujawafurahisha wengi, muongozo wake na michango yake katika bunge la katika uliwaudhi wengi katika chama chake, uchangiaji wake katika sakata la escrow uliwafurahisha wachache sana. Lakini kwa wanachama wa kawaida wakulima na wafanyakazi akaoneka ni kiongozi mpya waliyekuwa wanamsubiri.

Ghafla akaanza kuwa maarufu miongoni mwa wanachama wa kawaida. Umaarufu huo ukaanza kujenga hofu kwa baadhi ya makada kuwa anaweza kugombea urais hivyo ziara zake ni jitahada zake kutaka urais.


Hamad Rashid amekuwa ni kielelezo cha viongozi ambao wamo ndani ya chama lakini hawajui au hawaamini ilani au sera za vyama vyao wako tayari kutumikia sera au chama chochote pale fursa itakapojitokeza, Zitto ameonyesha ni mwanasiasa anayeamini na kuthamini anavyoviamini hata katika mazingira magumu ya kisiasa, Mwiguru ni mfano wa kiongozi na mwanasiasa anayeweza kufanya mabadiliko makubwa ya kimsimamo katika ujenzi wa siasa mpya.

Natamani kuona wananasiasa angalau wanakuwa kama hawa wawili wa mwisho. Wakati Hamad anafukuzwa CUF mimi nilikuwa na mtu ninayeandika na kuingia katika mijadala mbalimbali kuonyesha kuwa Hamad alionewa ( japo si mwanachama wa CUF), nilikuwa mtetezi wake, lakini sasa kila nikiyatazama nayaonea aibu maandiko yangu, sitaki hata kuyatazama.

Inasikitisha sikujua watu walio nyuma ya Zitto lakini baada ya kuwaona wana uzoefu mdogo wa kisiasa kuliko Zitto nikabaki namsikitikia. Niliposikia Mwiguru amepigwa marufuku kufanya ziara nilijiuliza ni kikao gani, lini alipewa onyo. Natamani siku moja Hamad “arudi” CCM, Zitto abaki Chadema na Mwiguru ashike parachuti.


I concur with u brother, ni analysis nzuri yenye ukweli mkubwa, nimeipenda, na ndivyo ilivyo, nilimchukia sana mwigulu the way alivyokuwa akiwashambulia wapinzani, na baada ya mchango wake wa ESCROW, niliandika ktk page yake ya fb kuwa kwa mara ya kwanza amenikosha, zitto nampenda na ameonyesha true color yake kwa kusimama ktk msitari mnyoofu, Hamadi ameonyesha wazi kuwa kweli ana uchu wa madaraka, lkn pia ukibaraka fulani kwa ccm, to me he is cheap politician!
Thanks!
 
I concur with u brother, ni analysis nzuri yenye ukweli mkubwa, nimeipenda, na ndivyo ilivyo, nilimchukia sana mwigulu the way alivyokuwa akiwashambulia wapinzani, na baada ya mchango wake wa ESCROW, niliandika ktk page yake ya fb kuwa kwa mara ya kwanza amenikosha, zitto nampenda na ameonyesha true color yake kwa kusimama ktk msitari mnyoofu, Hamadi ameonyesha wazi kuwa kweli ana uchu wa madaraka, lkn pia ukibaraka fulani kwa ccm, to me he is cheap politician!
Thanks!

Ni kweli mkuu mambo ya siasa inabidi kwanza uyakatae mapenzi yako kwa chama fulani ili uwe fair
 
neno uzalendo sasa linaanza kutumiwa vibaya, anyway it is nt monopoly of any group
 
Back
Top Bottom