Hamad Rashid, Zitto Kabwe na Mwigulu Nchemba (Comparative analysis)

Hamad Rashid, Zitto Kabwe na Mwigulu Nchemba (Comparative analysis)

Ilongailunga

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2012
Posts
1,388
Reaction score
896
Leo nimeona ni vema kuwafanyia mjadala wanasiasa hao watatu, sit tu kwa sababu ya majina yao makubwa na mchango wao kwenye siasa za Tanzania bali pia mienendo yao na harakati zao kisiasa. Kwa maoni yangu kuna vitu ambavyo vinawafananisha sana lakini pia yapo mengi yanayowatofautisha.

Hamad Rashid yupo kwenye mgogoro na "chama chake" cha Cuf toka mwaka 2012 na hatimaye kufukuzwa chamani na yeye kwenda mahakamani kupinga kufukuzwa kwake, mpaka leo amebaki na ubunge kwa amri ya mahakama tu, Zitto Kabwe naye ni vivyo hivyo kwa upande wa Mwiguru Nchemba ni hivi majuzi tu ameingia kwenye msuguano na Katibu wa chama chake, yeye amepigwa marufuku kufanya mikutano na au ziara mbalimbali za kichama. Sababu zilizopelekea migogoro na wakubwa wao ni moja, madaraka.

Wakati Hamad Rashid akitajwa kufanya kampeni chafu tena zenye kuratibiwa na baadhi ya makada wa ccm ili kuchukua nafasi ya Katibu mkuu, Zitto anatuhumiwa kutaka kuchukua nafasi ya M/kiti wa CDM kwa ufadhiri wa wasaliti na baadhi ya vigogo wa serikali, huku Nchemba akituhumiwa na katibu wake kufanya ziara na mikutano ya hadhara kwa lengo la kimarisha kampeni zake za kuteuliwa na CCM kugombea urais octoba mwaka huu kwa kuungwa mkono na baadhi ya makada wa chama chake.

Sababu hizo za migogoro na vyama vyao na hali halisi ilivyo sasa hivi inatoa taswira sahihi nini kiliwasababishia migogoro na ni kwa kiwango gani tuhuma dhidi yao ni sahihi au sio sahihi. Hamad Rashid Mohamed mjenga hoja imara na mkosoaji mkubwa dhidi ya mfumo wa serikali mbili, mpiganiaji wa maslahi ya Zanzibar dhidi ya "unyonyaji" wa Tanganyika mara tu baada ya kufukuzwa uanachama akatangaza kuunda chama chake huku akienda mahakama kupinga kuvuliwa uanachama (inachekesha).

Lakini ghafla mtazamo na falsafa yake ya mambo ikabadilika, Imani yake ya kisiasa ikabadilika pia, mtazamo wake kisiasa, falsafa na imani yake kisiasa ikawa ni sawa kabisa na ile ya Chama cha mapinduzi, hili lilionekana wazi katika bunge la katiba. Badala yake Hamad akawa political ankerman wa chama cha mapinduzi.

Zitto Kabwe atasikitikia uamuzi wake wa kufuata ushauri wa maswahiba zake kisiasa, kwa bahati mbaya wengi wao hawana uzoefu mkubwa kama yeye katika practical politics bila kuwa na uelewa mpana wa siasa za ndani ya vyama wakataka kumkweza na kumuweka juu ya chama hivyo kuzua migogoro na waasisi na baadhi ya wanachama wa muda mrefu. Mara tu baada ya kufukuzwa uanachama yeye na wenzake, Zitto akaenda mahakamani kuweka pingamizi lakini kama ilivyo kwa Hamad naye anahusishwa na chama kimoja cha siasa.

Hamad na Zitto wanatofauti kubwa katika harakati zao kisiasa.

Zitto bado anaamini na ameonyesha bado anasimamia misingi ileile aliyokuwa nayo Chadema. Ikumbukwe kuwa Hamad hakutoka CUF kwa sababu ya kupinga misingi au falsafa ya chama bali mgogoro wa kiungozi( tofauti na Himid aliyepinga sera na falsafa ya CCM), Kwa upande wake Zitto ameonekana kuwa bado ni mpinzani, kinadharia bado ni mwana chadema, ni mwana ukawa. Mwiguru Nchemba katika miaka hii miwili amefanya mabadiliko makubwa (self-political evolution) katika harakati zake za kisiasa kutoka siasa za kushambulia wapinzani hadi siasa za kitaifa, amebadilika mno.

Sasa amekuwa akijitokeza kama mtaifa mwenye kuangalia maslahi mapana ya taifa kuliko ya chama chake. Mwenendo huu mpya haujawafurahisha wengi, muongozo wake na michango yake katika bunge la katika uliwaudhi wengi katika chama chake, uchangiaji wake katika sakata la escrow uliwafurahisha wachache sana. Lakini kwa wanachama wa kawaida wakulima na wafanyakazi akaoneka ni kiongozi mpya waliyekuwa wanamsubiri.

Ghafla akaanza kuwa maarufu miongoni mwa wanachama wa kawaida. Umaarufu huo ukaanza kujenga hofu kwa baadhi ya makada kuwa anaweza kugombea urais hivyo ziara zake ni jitahada zake kutaka urais.

Hamad Rashid amekuwa ni kielelezo cha viongozi ambao wamo ndani ya chama lakini hawajui au hawaamini ilani au sera za vyama vyao wako tayari kutumikia sera au chama chochote pale fursa itakapojitokeza, Zitto ameonyesha ni mwanasiasa anayeamini na kuthamini anavyoviamini hata katika mazingira magumu ya kisiasa, Mwiguru ni mfano wa kiongozi na mwanasiasa anayeweza kufanya mabadiliko makubwa ya kimsimamo katika ujenzi wa siasa mpya.

Natamani kuona wananasiasa angalau wanakuwa kama hawa wawili wa mwisho. Wakati Hamad anafukuzwa CUF mimi nilikuwa na mtu ninayeandika na kuingia katika mijadala mbalimbali kuonyesha kuwa Hamad alionewa ( japo si mwanachama wa CUF), nilikuwa mtetezi wake, lakini sasa kila nikiyatazama nayaonea aibu maandiko yangu, sitaki hata kuyatazama.

Inasikitisha sikujua watu walio nyuma ya Zitto lakini baada ya kuwaona wana uzoefu mdogo wa kisiasa kuliko Zitto nikabaki namsikitikia. Niliposikia Mwiguru amepigwa marufuku kufanya ziara nilijiuliza ni kikao gani, lini alipewa onyo. Natamani siku moja Hamad "arudi" CCM, Zitto abaki Chadema na Mwiguru ashike parachuti.

good analysis nafikiri hao ndio wanasiasa wakuigwa japo wanaonekana kama wasaliti hivi
ila kwa mtu mwenye upeo mkubwa utatambua kuwa wanasifa za kuwa viongozi kwenye taifa letu
 
Mara nyingi viongozi wa kiafrika hawataki watu wenye uwezo na upeo mkubwa wanaogopa kufunikwa au kunyanganywa vyeo vyao
 
Mwiguru Nchemba katika miaka hii miwili amefanya mabadiliko makubwa (self-political evolution) katika harakati zake za kisiasa kutoka siasa za kushambulia wapinzani hadi siasa za kitaifa, amebadilika mno. .
Mwambie huko aliko ana tuhuma nyingi mno za kujibu kuanzia kule Igunga, na Arusha, Pamoja na ile video yake ya UGAIDI wa CHADEMA - asifikiri tumesahau.

Hawezi kuzifikia siasa za kitaifa bila kujisafisha, na njia pekee ni kuja kutubu kwetu sisi wananchi na kwa mwenyezi Mungu.
 
Inasikitisha sikujua watu walio nyuma ya Zitto lakini baada ya kuwaona wana uzoefu mdogo wa kisiasa kuliko Zitto nikabaki namsikitikia. .

Pamoja na kuwalaumu washauri wake kwa kiasi kikubwa, yeye mwenyewe pia amecheza nafasi kubwa sana kujimaliza kisiasa. Huyu hatumwonei huruma hata moja.
 
Mwambie huko aliko ana tuhuma nyingi mno za kujibu kuanzia kule Igunga, na Arusha, Pamoja na ile video yake ya UGAIDI wa CHADEMA - asifikiri tumesahau.

Hawezi kuzifikia siasa za kitaifa bila kujisafisha, na njia pekee ni kuja kutubu kwetu sisi wananchi na kwa mwenyezi Mungu.

mkuu, kama umemwelewa vizuri mjenga hoja MWIGULU keshaonyesha kupevuka, hizo hadithi za nyuma unazotaka kuzirejesha hazina maana tena.
 
Nami natamani Mwigulu abaki ccm,Hamad abaki ccm na Zitto pia abaki ccm.

nimeandika for the sake of arguement
 
mkuu, kama umemwelewa vizuri mjenga hoja MWIGULU keshaonyesha kupevuka, hizo hadithi za nyuma unazotaka kuzirejesha hazina maana tena.

Nini hakina maana tena! Tabia ya mtu haina maana? Hebu wacha tusikutukane bure. Huyu huyu Mwingulu amesbabisha watu kuwekwa rumande kwa makosa ya kutengeneza, huku yeye akisimama majukwaani na kutukana matusi mazito unatuambia tabia zake chafu hazituhusu? Huyu huyu ameona uchaguzi unakaribia anajifanya eti kuvaa mpaka underwear ya bendera ya taifa (akifikiri utaifa ni mavazi) unatuambia tabia yake mbovu sana haina maana kwetu? Huyu huyu asherati mkubwa alikutwa na mke wa mtu huko Igunga unatuambia tabia yake ya uasherati haina maana kwetu? Tafadhali bwana mdogo... wengine majeraha bado mabichi... usiyatoneshe!
 
mkuu, kama umemwelewa vizuri mjenga hoja MWIGULU keshaonyesha kupevuka, hizo hadithi za nyuma unazotaka kuzirejesha hazina maana tena.

hazna maana??? pumbavu!!!!!!!!! yan kaua ndugu zetu halafu unasema hazina maana
 
Pamoja na kuwalaumu washauri wake kwa kiasi kikubwa, yeye mwenyewe pia amecheza nafasi kubwa sana kujimaliza kisiasa. Huyu hatumwonei huruma hata moja.

kwani chadema ni ya baba yako?
 
Nini hakina maana tena! Tabia ya mtu haina maana? Hebu wacha tusikutukane bure. Huyu huyu Mwingulu amesbabisha watu kuwekwa rumande kwa makosa ya kutengeneza, huku yeye akisimama majukwaani na kutukana matusi mazito unatuambia tabia zake chafu hazituhusu? Huyu huyu ameona uchaguzi unakaribia anajifanya eti kuvaa mpaka underwear ya bendera ya taifa (akifikiri utaifa ni mavazi) unatuambia tabia yake mbovu sana haina maana kwetu? Huyu huyu asherati mkubwa alikutwa na mke wa mtu huko Igunga unatuambia tabia yake ya uasherati haina maana kwetu? Tafadhali bwana mdogo... wengine majeraha bado mabichi... usiyatoneshe!

Ni kwel ila mtu anaweza kutubu na kuanza upya kwa hyo ondoa Shaka juu ya hilo
 
.. ila hamad rashid in mtu wa siasa za KUSAKA TONGE,
 
ila hamad rashid in mtu wa siasa za KUSAKA TONGE Mwenendo wake kisiasa unamdhalilisha mno
 
Nani kakuambia kuna naisha bila historia. Kuna msemo nwana asili haachi asili.
 
Hamad wakati kiongozi wa upinzani bungeni, si alikuwa anampa PM maswali atakayoulizwa. Ni mjinga sana mtu wa zenji yule, alifikiri atakuwa kiongozi tena hakujua kila zama zina mfalme wake.
 
Back
Top Bottom