Wakati wazanzibari wenye sifa ya kupigakura wakijiandaa kufanya maamuzi siku ya Jumapili Machi 20, Mgombea wa Urais wa Chama cha ADC, Hamad Rashid Mohammed ameongezewa ulinzi.
Mgombea huyo wa Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya ADC alianza kuongezewa ulinzi jana baada ya kupokea meseji kadhaa zenye vitisho wakimtaka kutoshiriki uchaguzi wa marudio wa tarehe 20 Machi, 2016.
"Katika taarifa iliyoripotiwa kwenye vyombo vya habari, inasema kuwa moja ya meseji inayodhaniwa kuwa imetumwa na wafuasi wa CUF ilinukuliwa ikisema "AMUA jambo moja, kubaki hai wewe na familia yako, ama kuingia kwenye Uchaguzi na kuwa Kiongozi bila kuwa na familia maana hatutobakiza hata paka mmoja"
Kwa hatua hiyo ya Hamad Rashid kuongezewa ulinzi imetafsiriwa kuwa ni ishara ya Umakamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, na hivyo historia ya Katibu Mkuu wa CUF, Seif Shariff Hamad kufutika kabisa katika siasa ya Zanzibar, ikiaminika kuwa Ahmad Rashid ni mtu mwenye ngome na anayekubalika Visiwa vyote vya Pemba na Unguja.
Pia, Taarifa ya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ya jana iliyotolewa na Mwenyekiti wake Ndugu Jecha imedai kuwa karatasi za kura zitaingia Zanzibar tarehe 17 Machi siku ya Alhamis na kwamba hali ya amani na usalama imeendelea kuimarishwa katika visiwa vya pemba na unguja.