Hamad Rashid kuanzisha chama kipya!

Aanzishe Mara ya ngapi? ADC cha kwako ama?
 
Mbona hii ipo kitambo chama kishaanza chaitwa ADC juzi kulikuwa na mkutano wa CUF kule jimboni kwakwe wanachama wake wote wamerejesha kadi hadi ndugu zake baba mmoja mama mmoja wamechana bendera za ADC, Mwaka jana alileta milioni 10 jamaa wakazichangamkia wakaweka bendera ya ADC lakini hamadi alipopanda ndege tu kurudi Tanganyika bendera ikapachuliwa ikaekwa ya CUF.

Hamad Rashid hana mvuto tena kisiasa, mkakati uliopo ni kuendeleza hicho chama lakini sio kushika dola lengo ni kupunguza idadi ya wapiga kura wa CUF kule Zanzibar.
 
Lengo la Hamad Rashid ni ili apate madaraka na si kutetea wananchi kama anavyodai
Tatizo la watanzania hatuna kumbukumbu, tafuteni taarifa za Hamad Rashid Mohamed alipo kuwa naibu waziri pale wizara ya mambo ya ndani chini ya Maj Gen Kimario na Abdala Natepe.
Kama hamna hizo kumbukumbu nitafuteni.
 

Si tuliambiwa kuwa ni mwenyekiti wa ADC? Anataka kuanzisha kingine?
 
Kama walivyofanya ACT Tanzania kwa kujaribu kupunguza wafuasi wa chadema ili Ccm washinde kirahisi ndivyo hamad rashid anavyojaribu kufanya zanzibar.lengo lao ni kugawana wafuasi wa cuf ili ccm ishinde.kutokana na influence hamad rashid aliyokuwa nayo cuf alijua akiondoka lazima aondoke na kundi la wafuasi wa cuf na kwa kufanya hivyo angepunguza makali ya cuf zanzibar.kama anavyo jaribu kufanya MM wa chadema anayetarajiwa kwenda act tanzania.be blessed!
 
Si tuliambiwa kuwa ni mwenyekiti wa ADC? Anataka kuanzisha kingine?
Angalia tarehe ambayo hii thread iliwekwa. Kwa wakati huo, hiyo ADC ilikuwa haijaanzishwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…