Hamad Rashid; kielelezo cha Ubinafsi wa CUF | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hamad Rashid; kielelezo cha Ubinafsi wa CUF

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ibrah, Feb 2, 2011.

 1. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #1
  Feb 2, 2011
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Leo Mwanahalisi limekuja na habari "Hujuma dhidi ya CDM nje". Limekuja na taarifa kuwa kuna Mradi wa vyama vitatu vya upinzani unaolenga kupunguza nguvu ya Chadema bungeni. Kwamba aliyekuwa Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Hamad Rashidi (CUF) anaongoza mpango wa chini kwa chini wa kutaka mabadiliko ya kanuni za Bunge ili kuunda Kambi siyo Rasmi ya Upinzania Bungeni kufuatia tamko la Spika kuwa Kanuni hazitambui 'kambi isiyo rasmi'.

  Mwanahalisi linamtaja Hamad Rashi kuwa kinara wa kutunga kanuni za sasa juu ya kutambuliwa kambi rasmi mwaka 2005 baada ya kushindwa na UDP kwenye kura za uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) ili kuwaengua wabunge wa Vyama vingine vya Upinzania kutambulika/ kushika uongozi wa Kamati za Bunge.

  Baada ya kuonja adha ya kuwa nje ya Kambi rasmi ya upinzani Bungeni na kujikuta Kanuni alizoshininiza zibadilshwe mwaka 2005 leo zimemgeuka, sasa anapanga mkakati wa chini kwa chini ati kutengua sheria zile alizozishinikiza zitungwe 2005 ili kuwatenga wapinzani wenzake leo zimemrudi mwenyewe.

  Je, Hamad Rashid si kielelzo cha ubinafsi wa CUF katika siasa za Tanzania?
   
Loading...